Waongozaji 90 wa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamesusia zoezi la Sensa ya watu na makazi linaloendelea kote Nchini kwa madai ya kutolipwa fedha zao.
Waongozaji hao wa Makarani wamedai kuwa waliahidiwa kulipwa laki moja kwa awamu mbili lakini hadi kufikia Agosti 28, 2022 hawakuwa wamelipwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa wa Chemba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Samson Chacha alikutana na waongozaji hao wa makarani hao na kuahidi kuwa watalipwa kama walivyokuwa wamepangiwa.
Source: Azam TV