Dodoma: Mapokezi ya Alhad Musa Salum yazua Taharuki, Waislam Wamwandikia barua Mufti

Naona unataka kujaribu kuwafananisha viongozi wa kiislam na akina gwajima, mzee wa upako, mwamposa etc,, lkn inakataa.
Acha unafiki hebu tupia walau picha tuone huo msafara wa ving'ora na pikipiki na sie tuone. Huku kwenye uislam hakuna mbwembwe sijui za misafra mirefu na ving'ora na mapikipiki mengi kama huko kwenu hata uwe msafara wa muft.
Usibishe kitu usichokijuwa, video zipo kwenye page ya Maulid Kitenge Facebook, nenda kule halafu uje kubisha vizuri.
 
Kwani nje ya cheo alichokua nacho hana hadhi yake binafsi ? Amepokelewa kama Musa Salum hajapokelewa kama Sheikh wa mkoa hizi complications nyingine hazina umuhimu sana. Mtu amekabidhi ofisi mnataka aishi kinyonge ?
Polisi wanahusika vipi kwenye Mapokezi ya mtu binafsi?Tumia akili hata za kuazima
 
Wakuu hakuna mtu amenyumwa escort ya police ni pesa yako tu unaenda jeshi la polisi unalipia unapata pikipiki ya kuongoza msafara wako,kwa shekhe tuhoji wale waliompokea nani amewapanga au na wenyewe wanalipwa ili kuonyesha anapendwa?
 
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam , Musa Salum , ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki .

Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini .

Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito , yanasema hivi , KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU ? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe ?
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam , Alhad Musa Salum ni Mtu muhimu wa Serikali aka Usalama wa Taifa huyo. Alikuwa anafanya kazi zaidi 2 kazi ya bakwata na kazi ya Serikali
 
Usibishe kitu usichokijuwa, video zipo kwenye page ya Maulid Kitenge Facebook, nenda kule halafu uje kubisha vizuri.
Kwa maulid kitenge mimi nikafanye nini,,, habari nimeiona hapa kwa hiyo huyu mleta uzi ye ndo aambatanishe na picha,, la sivyo ni umbeya,, alafu sie wengine hiyo Facebook kuitumia nimesahau lini mara ya mwisho kuingia japokuwa ninayo account.
 
Wivu tu,mbona yeye alikuwa anaenda kusomea vichwa vya habari vya magazeti ulaya tena akiwa hata hasikiki vizuri na hakuna aliyemchongea kwa mabosi zake?

Alifikiri wasikilizaji walilipenda lile jambo?by the way naomba anayejua anifafanulie nini maana ya MAAMUMA?
MAAMUMA ni mfuasi au muongozwaji
Yani waislamu tukiwa msikiti Imamu ndo anakua kiongozi mkuu ambae anaendesha swala na walobakia ambao wapo nyuma yake wote wanaitwa Maamuma

Nadhani utakua ushanielewa mpka hapo
 
Wivu tu,mbona yeye alikuwa anaenda kusomea vichwa vya habari vya magazeti ulaya tena akiwa hata hasikiki vizuri na hakuna aliyemchongea kwa mabosi zake?

Alifikiri wasikilizaji walilipenda lile jambo?by the way naomba anayejua anifafanulie nini maana ya MAAMUMA?
(Maamuma) HADHIRA /MFUATISHAJI Waweza Kuwa Na Elimu Ila Ukawa Msimuliwaji Na Msikilizaji Japo Weng Wanatafsir Kama Ni Mtu Ambaye Huna Elimu Yoyote
 
Kwa maulid kitenge mimi nikafanye nini,,, habari nimeiona hapa kwa hiyo huyu mleta uzi ye ndo aambatanishe na picha,, la sivyo ni umbeya,, alafu sie wengine hiyo Facebook kuitumia nimesahau lini mara ya mwisho kuingia japokuwa ninayo account.
Hata kama ni umbeya utanifanyia Nini kima wewe?
 
Barua ya Wazi

Assalaam Alaykum,

Sheikh Mkuu, Mufti wetu wa Tanzania, nimeguswa kukuandikia barua hii ya wazi ama kwa kuhoji na kutaka ufafanuzi, ama kwa kushangazwa na nilichokiona.

Kama nilivyoshangazwa, nimefuatilia kwa ndugu zetu wengi katika imani, ama kwa hakika, tukio ninalolileta kwako limejenga taharuki kubwa kwetu waumini.

Nimeona video mtandaoni ikimwonesha aliyekuwa Sheikh wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akipata mapokezi ya ving'ora vya polisi na msafara wenye magari na pikipiki, mkoani Dodoma. Na kulakiwa na waumini kama Sheikh mwenye darja.

Sheikh wetu, tukio hilo limetengeneza mshangao mkubwa. Hayajapita majuma mawili tangu ulipomwondoa Alhad Mussa kuwa Sheikh wa Dar es Salaam. Inastaajabisha anatokeza na mapokezi makubwa.

Waislam wana maswali matano. Alhad Mussa anafikisha ujumbe gani? Anataka kumaanisha yeye ni mkubwa kuliko mamlaka ya Mufti aliyemtengua? Msafara wenye ving'ora na pikipiki iliyomsafishia njia, amepewa kama nani, ikiwa yeye kwa sasa ni maamuma? Polisi ni serikali, kwa mapokezi hayo, serikali inamuunga mkono Alhad Mussa dhidi ya Mufti? Waislam waliompokea na kumkirimu Alhad Mussa mithili ya kiongozi wa darja kubwa lengo lao ni nini?

Kwa maswali hayo, Sheikh wetu, Mufti Abubakar Zuberi, huna budi kutoka na kuzungumza na umma wa Waislam na hata wasio Waislam, ujibu maswali hayo ili Watanzania na mamlaka zake zitambue haki anazostahili Alhad Mussa na ambazo hastahili.

Hitimisho la kila mjadala ni kuwa kitendo cha Alhad Mussa kutengeneza mapokezi yale ni utovu mkubwa nidhamu kwa mamlaka ya Mufti. Amelikosea heshima Baraza la Ulamaa la Bakwata na uongozi wote wa juu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).

Nakuangukia. Shime Sheikh, toka uongee na umma. Tujue nafasi ya Alhad Mussa. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani. Nafasi hiyo aliipata sababu alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sasa si Sheikh tena. Kwa nini ving’ora vya polisi na kumbatio la waumini tena msikitini?

Wabillahy Ttawafiq,

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakutu

View attachment 2517441
Shekhe mkuu aongee na dada mkuu huenda katoa ruhusa.
 
hii tabia inaletwa na unafq wa serikali masheikh watu hawa uwezo wa kuishi maisha haya wnayo hishi sababu maisha yao na vipato viao walikotoka tunapafahamu bora ije katiba mpiya na tume hulu ya uchaguzi kila mtawala ipate utawala kwa haki na viongozi wadini wale jasho lao
 
Aliyekuwa Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Salum, ametua Dodoma ambako amepata mapokezi Makubwa vikiwemo ving'ora vya Polisi huku akisindikizwa na msafara wa Magari na lundo la Pikipiki.

Haifahamiki ameenda Dodoma kufanya nini.

Bali Malalamiko ya Waislam waliomlima barua Mufti ya kutaka afafanue sababu hasa ya Musa Salum kupokelewa na msafara mzito, yanasema hivi, KWANINI MTU MAAMUMA ASIYE NA CHEO CHOCHOTE KUPOKELEWA KIHESHIMA NAMNA ILE UTADHANI NI KIONGOZI WA DARJA LA JUU? Je hii si dharau kwa Baraza la Ulamaa na Mufti Mwenyewe?
ccm kwa fitina hatari si ajabu wanamuandaa awe mkuu wa bakwata faifa
 
Back
Top Bottom