Dodoma: Mapokezi ya Alhad Musa Salum yazua Taharuki, Waislam Wamwandikia barua Mufti

Dodoma: Mapokezi ya Alhad Musa Salum yazua Taharuki, Waislam Wamwandikia barua Mufti

Focus kwenye siasa chuki zako binafsi za kidini acha,,,
Sijui kama umeelewa kilicholetwa hapa , yaani mimi nimeripoti tu yaliyoandikwa na Waislam, sasa labda useme siruhusiwi kuripoti masuala ya Waislam .

Lakini wewe ni nani wa kunipangia vya kuripoti humu ?
 
Sijui kama umeelewa kilicholetwa hapa , yaani mimi nimeripoti tu yaliyoandikwa na Waislam, sasa labda useme siruhusiwi kuripoti masuala ya Waislam .

Lakini wewe ni nani wa kunipangia vya kuripoti humu ?
Sijakupinga,, ila ripoti yako imekaa kiunafiki na wewe pia ni mnafiki,, kwani uislam na waislam wamekukosea nini wewe mwana chadema?? Na chadema wenzio kwa ujumla?
 
Hivi Kuna mufty yoyote aliyewahi kupata mapokezi Kama haya mahali popote hata kijijini kwake.?
Sheikh Mussa is a force to reckon with.
Mtamsema Sana lkn jamaa ana followers wengi Sana.
 
Barua ya Wazi

Assalaam Alaykum,

Sheikh Mkuu, Mufti wetu wa Tanzania, nimeguswa kukuandikia barua hii ya wazi ama kwa kuhoji na kutaka ufafanuzi, ama kwa kushangazwa na nilichokiona.

Kama nilivyoshangazwa, nimefuatilia kwa ndugu zetu wengi katika imani, ama kwa hakika, tukio ninalolileta kwako limejenga taharuki kubwa kwetu waumini.

Nimeona video mtandaoni ikimwonesha aliyekuwa Sheikh wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akipata mapokezi ya ving'ora vya polisi na msafara wenye magari na pikipiki, mkoani Dodoma. Na kulakiwa na waumini kama Sheikh mwenye darja.

Sheikh wetu, tukio hilo limetengeneza mshangao mkubwa. Hayajapita majuma mawili tangu ulipomwondoa Alhad Mussa kuwa Sheikh wa Dar es Salaam. Inastaajabisha anatokeza na mapokezi makubwa.

Waislam wana maswali matano. Alhad Mussa anafikisha ujumbe gani? Anataka kumaanisha yeye ni mkubwa kuliko mamlaka ya Mufti aliyemtengua? Msafara wenye ving'ora na pikipiki iliyomsafishia njia, amepewa kama nani, ikiwa yeye kwa sasa ni maamuma? Polisi ni serikali, kwa mapokezi hayo, serikali inamuunga mkono Alhad Mussa dhidi ya Mufti? Waislam waliompokea na kumkirimu Alhad Mussa mithili ya kiongozi wa darja kubwa lengo lao ni nini?

Kwa maswali hayo, Sheikh wetu, Mufti Abubakar Zuberi, huna budi kutoka na kuzungumza na umma wa Waislam na hata wasio Waislam, ujibu maswali hayo ili Watanzania na mamlaka zake zitambue haki anazostahili Alhad Mussa na ambazo hastahili.

Hitimisho la kila mjadala ni kuwa kitendo cha Alhad Mussa kutengeneza mapokezi yale ni utovu mkubwa nidhamu kwa mamlaka ya Mufti. Amelikosea heshima Baraza la Ulamaa la Bakwata na uongozi wote wa juu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata).

Nakuangukia. Shime Sheikh, toka uongee na umma. Tujue nafasi ya Alhad Mussa. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Amani. Nafasi hiyo aliipata sababu alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam. Sasa si Sheikh tena. Kwa nini ving’ora vya polisi na kumbatio la waumini tena msikitini?

Wabillahy Ttawafiq,

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakutu


View attachment 2517441
Huwezi jua labda mwenzao.
 
Kumbe ulidhamiria tu kunishambulia bila sababu , sasa nimeelewa , lakini sasa umechagua kunishambulia sehemu isiyo sahihi
Huna lolote mnafiki mkubwa wewe sio mara moja naona post zako una chuki dhidi ya uislam na waislam sijui hata wamekufanya nini,, eti taharuki, taharuki gani hiyo kama sio unafiki
 
Back
Top Bottom