27.12.2019
Dodoma, Tanzania
Kamanda Muroto : Kifo Cha Mkurugenzi wa Shule ya Zamzam, Dodoma
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Muroto atoa taarifa rasmi juu ya tukio la mauaji la mmiliki wa shule ya Zamzam. Uchunguzi wa awali ni kuwa marehemu amefariki kwa moyo kushindwa kufanya kazi yaani heart failure na kwa vile alikuwa pekee yake ofisini alishindwa kupata msaada kuokoa maisha yake
Pia marehemu simu yake ilikuwa imezima kwa kuishiwa charge maana mara baada ya kuwasili kwa usafiri wa basi akitokea Dar es Salaam, alikwenda pamoja na mabegi yake moja kwa moja hadi ofisini kwake mjini Dodoma na ndipo mauti yalimfika. Marehemu alikuwa na umri wa miaka 62, mrangi jina Rashid Bura.
Kamanda Muroto ametoa angalizo kwa vyombo vya habari kuwa makini wanapotoa taarifa bila kuulizia vyombo rasmi kama Polisi au ripoti za Daktari. Akatoa mfano mmoja wa habari alizoona JamiiForums , Magazeti ya HabariLeo, NIPASHE, Mwananchi n.k kuhusu jinsi mauti yalivyomkuta marehemu Rashid Bura, ambazo siyo sahihi.
Source: Millard Ayo
Vyombo vya Habari vilivyoripoti kifo cha mkurugenzi:
https://www.habarileo.co.tz › habari
27/12/2019 - Habarileo
Slain Bura due for burial in Dodoma. DAILY NEWS Reporter in Dodoma. 27/12/2019. 0 Maoni. THE body of Rashid Bura, founder of Dalai Islamic Centre and ..
"Mwili bosi wa Zam Zam kuzikwa Dodoma, utata wagubika kifo chake - Mwananchi"
Mwili bosi wa Zam Zam kuzikwa Dodoma, utata wagubika kifo chake
"Former State House guard who died in office to be buried - The Citizen"
Former State House guard who died in office to be buried