Dodoma: Mwanafunzi ashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kupiga na kutuma picha za ukosefu wa maji Chuo Kikuu Dodoma

Taarifa rasmi zinatakiwa kutolewa na vyuo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mawaziri na wabunge wa ccm hawajui matatizo ya taasisi kama hiyo na ni majuzi tu mwenyekiti wao alikuwa pale?
 
MWANAFUNZI MUYAGA TUNGU ANAYEDHANIWA KUPIGA PICHA ZA KUONYESHA TATIZO LA MAJI UDOM MIKONONI MWA POLISI DODOMA

Mwanafunzi wa mwaka wa pili anayesoma Sayansi ya Asili (Natural Science ) chuo kikuu cha UDOM , Mugaya Tungu alikamatwa Jan 21 mwaka 2020 akiwa chumbani kwake ndani ya bweni la Wanafunzi UDOM.

Mwanafunzi huyo alikamatwa na polisi bila kuambiwa kosa lake ni lipi na kwanini alikamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa kituo cha polisi chimwaga Dodoma.

Lakini pia rafiki yake wa karibu (jina lake limehifadhiwa) naye alifuatwa kukamatwa usiku lakini alishtukia mapema na hakuweza kulala chumbani kwake hivyo polisi walimtafuta na hawakumpata.

THRDC tumefuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi huyo na kupata taarifa kwamba mwanafunzi huyo anadhaniwa kupiga picha zinazoonyesha uhaba wa maji katika chuo kikuu cha Dodoma. Wanafunzi wanapata changamoto sana kuhusu maji hali inayowasababishia kupanga foleni muda mrefu na pengine kuchelewa masomo darasani, hivyo mwanafunzi Tungu anadaiwa kupiga picha za wanafunzi wenzake wakiwa wamepanga foleni muda mrefu na kwa wingi na hatimae kukamatwa kwake.

Wanafunzi wenzake walienda leo jan 22, 2020 mnamo sa saba mchana kwenye kituo cha polisi alipowekwa mwanafunzi Tungu lakini hawakufanikiwa kumuona. Wanafunzi wenzake baada ya kufika kituo cha polisi waliambiwa kuwa Tungu amepewa dhamana ya polisi lakini walipohoji endapo kuna mtu amemdhamini waliambiwa hayo hayawahusu.
Hata hivyo wanafunzi wenzake wamejaribu kupiga simu zake hazipatikani na mwanafunzi huyo hajaonekana bwenini mpaka sasa hivyo bado haijulikani alipo.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu kukamatwa kwa mwanafunzi Mugaya Tungu, na tutawapa taarifa kadri tutakavyobaini.

Imetolewa na
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania ( THRDC)
Jan 22, 2020
 
dah aisee hii inaumiza sana. serikali ya wanayonge hii kazi tunayo
 
jamaa atakuwa mfuasi wa kile chama nini?

Hawataki tujue kama kuna shida ya maji? mbona inajulikana na iko wazi kuwa hiki chuo kina changamoto kubwa ya maji. wanaficha nini sasa hapo?
 
Vitendo ambvyo vinafanya jamaa achukiwe na aonwe ni Mzalendo mav na pia mataifa mengine yamemstukia kuwa hafai kuwa kiongozi kwa sababu hata bad side ya uongozi wake uanikwe hadharani.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…