Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Hiyo issue ya mbowe hata kama haihusiani na siasa ni lazima kwa MTU yoyote atahusisha na mlengo wa kisiasa kutokana na hali ya siasa dhidi ya upinzani toka aingie Baba jesca.
 
Hivi unaposema umenielewa hapo juu ( kwa nilichokiandika ) halafu hapo hapo tena unaema ingawa siyo kwa 100% katika Mawazo yangu ndiyo unakuwa umesema nini sasa au nikueleweje au Wandugu hapa nao wakueleweje labda? Ningekuona uko makini baada ya kusema kuwa siyo kwa 100% basi nawe pia ungetoa Maelezo yako yenye Mantiki na Tija ila bahati mbaya umejibu kama vile hapa ni Facebook au Instagram huko.
Nisamehe ndugu kwa kukuchanganya. Nilipoandika hayo nilikua na maana ila nna uhakika na baadhi taarifa ulizoandika na kinadharia inaezekana ila kuna maoni yako umeyatoa hapo ndo siko nawe kwani nami nna yangu.
 
Ningependa kuwauliza chadema au Kama watashindwa kujibu Basi itabidi tunasubiri Mbowe mwenyewe aje atupe majibu

Mwenyekiti Mbowe inasemekana kavamiwa na watu na kumjeruhi huku chadema wakidai kuwa ni shambulio la kisiasa kwa sababu walio kuwa Wana mshambulia walikuwa wanasema baadhi ya maneno mfano, Acha kumsema sema vibaya Rais

Kulingana na tukio lilivyo inaonyesha wazi kabisa kuwa chadema hii wamepanga wao ili kutafuta huruma kwa Wananchi

Mbowe anaweza kutuambia muda huo saa sita alikuwa anatoka wapi na walimshambulia akiwa wapi? Na Kama walimshambulia njiani alipokuwa anaelekea kwake Kwanini alisimamisha gari usiku Tena saa sita? Pia huenda mbowe atakuwa alivamiwa akiwa amesimama sababu Sio Rahisi mtu yupo ndani ya gari Tena usiku uweze kumshambulia ki rahis.

Na je Kama Mbowe alishambuliwa wakati amesimama alikuwa anafanya Nini ilo eneo na alikuwa anatoka wapi uo usiku?

Pia nimeona baadhi ya Uzi zinazidi kudhihirisha kuwa chadema hii wamepanga na kutaka kuleta lawama kwa serikali pale wanapo sema Mbowe kavamiwa sehemu yenye ulinzi mbona walinzi hawakuwepo? Hii ni point ya kijinga na fikirishi na inatoa picha ya kuwa chadema huwa wanafanya Mambo Yao kwa kutumia udhaifu wa serikali kwenye maswala ya ulinzi.

Huwa wanatafuta maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine lazima kuwe na ulinzi ili wakifanya matukio Yao waje kuhoji serekali ulinzi uko wapi na kuwatupia lawama ili ionekane serekali ndio imepanga na yenyewe ndio ilio toa ulinzi eneo lile

Ili tukio linaonesha dhahir kuwa hata lile la Tundu Lissu lilipangwa
Mmefanya haya ili kuzima mjadala wa tundu lissu, stupid idea!
 
Kwa mimi nilishaondoa credibility na vyombo vya dola katika kushugulikia mambo yanayohusu wapinzani! Kuna mlolongo mrefu sana wa matukio yanayowahusu wapinzani kuumizwa na hata kuuawa kama ilivyotokea kwa mdogoake Heche.

Tundu Lissu, Mawazo na sasa Mbowe, na wengine, lakini ukifuatilia namna vyombo vya dola vinavyoshughulikia hayo mambo, ni utata mtupu! ....

Huyo kamanda anasema kapata taarifa, means hajafika wodini, anapata wapi uhakika kuwa majeruhi anaendelea vizuri? Kupigwa hadi kuvunjwa mguu sio jambo dogo na wala si kitu cha kuongelea kwa mzaha, labda tu kama kuna mtu unataka kumfurahisha kwa kauli hiyo!....Anyway ipo siku haya yote yatakomeshwa!
 
Mkuu nawe tumia akili hata kama ana mlinzi, wakitokea hao vibaka 10 Huyo mlinzi 1 atafanya nini? Kuhusu swala la muda nayo ni hoja dhaifu.
Inasemekana ni mtu 3 tuu imemburuza ina maana alikuwa peke yake?na kama alikuwa peke yake mda huo bado kuna wasiwasi na kama alichelewa kurudi kazini lazma mlinzi alikuwepo.mbona sijasikia lolote kuhusu mlinzi.
 
Hatuna uhakika.
Ila haya mambo yanayotokea Yana mfelisha sana magufuli na kumpa sifa mbaya.
Kama una uhakika na uongozi wako KWANINI UYAFANYE HAYA?.
Mwisho wa siku ukiondoka watu watasema.
"Alitujengea barabara,alituwekea umeme alitujengea madaraja n.k. lakini pia alikuwa ni MTESAJI NA MUUAJI".
hyo sio sifa NZURI.
Magufuli hapo ana husika nini
 
Dodoma kama ilivyo Dsm pana matukio mengi ya kihalifu nyakati za usiku na hasa kuanzia saa 5.

Nakumbuka hata mbunge Moses Machali wa Nccr mageuzi wakati huo aliwahi kuchapwa chapwa bakora na majambazi wakati akirejea nyumbani kwake usiku mzito baada ya kazi ngumu ya kulijenga taifa.

Ni tukio la Tundu Lisu pekee ndio litabakia kuwa historia kwa sababu lilifanyika saa 7 mchana wakati akitokea bungeni siyo Night club.

Maendeleo hayana vyama!
 
View attachment 1472626
View attachment 1472650

Salaam,

Taarifa nilizozipata hivi punde toka chanzo changu kinanihabarisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman A. Mbowe amevamiwa na kikundi cha watu wasiojulikana akielekea nyumbani kwake usiku huu na kupigwa na wamemuumiza.

Tukio hili limetokea majira ya saa 6-7 usiku.

Mhe. Mbowe amekimbizwa Hospitali ya Ntyuka iliyopo jijini Dodoma.

Kamanda Muroto amesema wamepata taarifa kuwa kavunjwa mguu wa kulia na amelazwa Wodi namba 4 hospitalini hapo. Amesema taarifa zaidi zitafuata

MAONI YANGU:
Mh. Mbowe kuvamiwa na kupigwa eneo la Area D, jijini Dodoma, Mtaa wa Sengia; linalotajwa kuwa na ulinzi wa kutosha, kama ilivyotokea kwa Lissu kunaacha maswali mengi, je, hili linaweza kuwa limechochewa na Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa JMT October 2020? Ni hasira au kitu gani? No one knows.

Bado najiuliza; hivi kama Taifa kwa tabia hizi za kihuni tunaelekea wapi? Hawa wanaojichukulia sheria mikononi kila siku wanafanya hivyo kwa kutumwa na nani? Matendo haya yataendelea kwa viongozi wa upinzani mpaka lini?

We need to wake up, better late than never.
Facts-: 1)wasiojulikana ni usalama wa taifa.(by Malima-RC Mara)
2)Inafahamika usalama wa taifa wanariport kwa rais
3). Hakuna uchunguzi utakao fanyika.
4) watakao kwa karibu tukio hili ndo watakao wekwa ndani.
5). Mwana ccm atakaye onyesha wazi huruma kwa Mbowe atatengwa/fukuzwa uanachama.

6)Watakao fanya maombi kwa mgonjwa watakamatwa na kuswekwa ndani.
7).Itasemwa kuwa Chadema ndo wameyengeneza tukio ili waonewe huruma, ingawa hao "Chadema" hawatakamatwa.
..THE UNITED REPUBLIC OF GANGSTER...
 
Dodoma kama ilivyo Dsm pana matukio mengi ya kihalifu nyakati za usiku na hasa kuanzia saa 5.

Nakumbuka hata mbunge Moses Machali wa Nccr mageuzi wakati huo aliwahi kuchapwa chapwa bakora na majambazi wakati akirejea nyumbani kwake usiku mzito baada ya kazi ngumu ya kulijenga taifa.

Ni tukio la Tundu Lisu pekee ndio litabakia kuwa historia kwa sababu lilifanyika saa 7 mchana wakati akitokea bungeni siyo Night club.

Maendeleo hayana vyama!
Unataka kusema KUB alikuwa anatokea night club?
 
Unataka kuhalalisha unyama aliofanyiwa Mbowe, sometimes una akili ndogo sana.
 
Back
Top Bottom