Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Mmhh hizi sarakasi sasa amepigwa au ameanguka?
RPC wa DOM kwenye Nipashe leo, amethibitisha kushambuliwa sasa hayo mashaka yanatoka wapi? Tunahoji tu hata kama wengine si Wanasiasa..!
 
Ingekuwa kwa wenzetu uchunguzi wa kina ungefanyika maana kama ni eneo lenye ulinzi wa kutosha means hata CCTV zipo za kutosha ilanahakika Jeshi lapolisi litashindwa pata watuhumiwa, nakumbuka kipindi cha lissu alipiga sana kelele kuhusu gari inayomfatilia na hata plate number matokeo yake gari ilikuwa haijulikani,

Lissu alisema kuna CCTV ila nazo nahis picha zilifutika ... ifike mahali watawala waseme hawautaki upinzani basi lijulikane moja maana this is too much ni wangapi watapewa majeraha ya kudumu, wangapi watapewa ulemavu wa kudumu kama Lissu na wangapi watauwawa kisa siasa?
 
Saa 7 za usiku kiongozi mkubwa anaranda mitaani anatokea wapi?
Mbowe ana mlinzi,gari na dereva wa serikali,walikua wapi?
Kikosi cha ulinzi cha chadema kilikua wapi?
Kwa ninavyomjua mbowe,lazima alikuwa katoka kucheza nje cup!
Kuna maswali ya kujiuliza ndani wanachadema,kabla kunyooshea vidole serikali
Saa 7 usiku kiongozi unatakiwa uwe umelala au upo nyumbani,alikua anatoka wapi?
Red brigade walikua wapi?
Alikuwa kwa mchepuko Mkuya
 
Sawa halali, sasa alikuwa ana rudi kwa miguu?? Au kwa Gari, gate anafungua mwenyewe au anafunguliwa?? Hana cctv hapo kwenye gate na gari yake haina cctv
kwani kwa lisu cctv zilienda wapi
 
Jana nilipoziona tu zile Nondo Kali na zenye Mashiko za Mheshimiwa Tundu Lissu nilihisi kabisa kuwa ili kuwapoteza Watu na Kuyahamisha Mawazo yao katika Kukijadili au Kuyajadili yale aliyoyaandika ambayo yote ni mazuri basi ni lazima tu Spinning ya Hatari ingefanyika. Kilichofanyika ni kutaka Kufunika alichokifanya Lissu jana kuanzia leo Watanzania wote tujikite zaidi katika Kuzungumzia hili lililomkuta Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Na Kiutaalam zaidi ili kuonyesha kuwa hawa Wapumbavu ( Wahuni ) wanaolelewa vibaya na Idara ya Usalama nchini ( SSIT ) walijipanga ni kwamba itakuwa walijipanga tokea pale Taarifa za Mheshimiwa Tundu Lissu aliposema kuwa atazungumza na Watanzania hivyo hata Wao walishajipanga na walipoona Jana Mheshimiwa Tundu Lissu katoa Nondo ile Kabambe basi na Wao wakaamua Kulitekeleza hilo walilolitekeleza...
Mkuu hapo juu nimekuelewa ingawa siko 100% ktk mawazo yako.
 
Red brigedy nawalaumu sana kwenye matukio yote la TL na hili la Mbowe.
Mmeshindwa kulinda viongozi wa chama.
 
Jaribio la KUANGUSHA MWAMBA baada ya Mipango yote ikiwemo Manunuzi kushindikana. Kuumiza na Kuua viongozi wa CHADEMA hakutaifufua CCM ILIOJIFIA.
 
CHADEMA siku hizi kimekua chama cha kupika matukio sana. Kelele za Corona zimebuma sasa mnajivunja miguu na kuanza kusingizia MAGUFULI! Siasa za kijinga sana hizi....

Capo Dei Capi
 
miguu ya mbowe mibovu siku nyingi kuna wakati huwa anatembelea magongo ikipona inatulia kidogo inaanza tena isiwe imeanza tena akitembelea magongo isemwe imevunjwa msema kweli mpenzi wa Mungu abishe kama hakuna wakati huwa anatembelea magongo
We jamaaa bn ccm tambeni bana upinzani wenyewe umebaki mitandaoni Field hakuna tambeni bn nchi yenu hii
 
Mkuu hapo juu nimekuelewa ingawa siko 100% ktk mawazo yako.

Hivi unaposema umenielewa hapo juu (kwa nilichokiandika) halafu hapo hapo tena unaema ingawa siyo kwa 100% katika Mawazo yangu ndiyo unakuwa umesema nini sasa au nikueleweje au Wandugu hapa nao wakueleweje labda?

Ningekuona uko makini baada ya kusema kuwa siyo kwa 100% basi nawe pia ungetoa Maelezo yako yenye Mantiki na Tija ila bahati mbaya umejibu kama vile hapa ni Facebook au Instagram huko.
 
Mbowe si ana mlinzi?huyu mlinzi wake alikuwa wapi. Na huo mda wanasema kavamiwa usiku saa saba bado napata wasiwasi hao itakuwa vibaka tuu
 
Back
Top Bottom