Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Tanzania’s leader of opposition in parliament attacked, beaten up, injured
9th June 2020
A group of unknown people have assailed, beaten up and injured the Leader of Opposition in Parliament in Tanzania, Freeman Mbowe, at his residence in Area D, Dodoma.

According to preliminary reports from Dodoma, Mbowe met his assailants on the steps of his flat this night, June 7, 2020., shortly before entering his residence.

“He didn’t manage to enter. They dragged him, threw him to the ground, and beat him up severely, warning him against criticising the president. Before neighbours came to his rescue, the damage has been done. He is in severe pain. One his legs has been badly twisted, and he fears it is broken,” a family source told SAUTI KUBWA. He was rushed to Benjamin William Mkapa Hospital.

Mbowe and other Members of Parliament are attending a parliamentary budget session in Dodoma City, two months before this year’s general election.

Under President Magufuli, Tanzania has been characterised by brutal and demagogic politics since he came to power in 2015. In September 2017, the opposition chief whip, Tundu Lissu, miraculously survived an assassination attempt by unknown people who shot at his car and injured him severely at his residence in Dodoma.

Source : Tanzania's leader of opposition in parliament attacked, beaten up, injured - Sauti Kubwa
The indication how the upcoming election will be

Jr[emoji769]
 
Pole sana.

Hapa swali la mlinzi wake alikuwa wapi na camera CCTV hakuna? lazima liwepo na lijibiwe.
 
Moja ya kauli maarufu zinazohusishwa na Ibrahimu Lincoln ni kuhusu udanganyifu, kwamba: Unaweza kuwadanganya watu wakati fulani na baadhi ya watu wakati wote, lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote - [You can fool all the people some of the time and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time.]

Hicho ndicho kinachoonekana kuwa wazi huko CHADEMA kwamba sasa ukweli unapaswa kujulikana kuondoa sintofahamu ya "wasiojulikana" kuendelea kufanya maovu.
 
Mbowe hana walinzi?

Kama hii habari ni ya kweli basi CHADEMA ni sikio la kufa lisilosikia dawa!

Una sababu njema tu kuwa na wasiwasi huu...

Lakini tufikiri kwa kwenda mbele kidogo...

"Wenye mamlaka" wakitaka kum-terminate mtu watazuiwa na walinzi binadamu mmoja au wawili?

Na kama wabunge wenye marupu rupu kibao kifedha, wananunuliwa na kusaliti nafsi zao, huyu mlinzi wa kulipwa laki 5 kwa mwezi atashindwa nini kumsaliti bosi wake akitengewa mzigo wa M30 mbele yake?

Haya maswali ni kuonesha tu kuwa walinzi ni kwa ajili vibaka wa kawaida mitaani lakini siyo kuzuia mpango wa kijambazi na kiuaji unaoratibiwa na wenye mamlaka....
 
Sasa ninaanza kuelewa kwa nini kila anayejiona 'kiongozi' kwa Tanzania yetu, awe kiongozi wa chama tawala, upinzani, na kiwe cheo chochote kile cha vijana au wazee, kiwe cha wanawake au wanaume, anakuwa na mtu anadimama nyuma yake (kama mlinzi)!

Enzi hizo ambazo kulikuwa na usalama wa kweli na viongozi kupendwa kweli kweli tulikuwa tukiona ni Rais tu alikuwa na mlinzi wa namna hiyo!

Tufike mahali tuelewe kuwa kuwa na ulinzi ni dalili kuwa uko mbali na watu unaodai wanakupenda na unawaongoza. Inashangaza sana watu kuanza kuhoji kwa nini kiongozi wa upinzani hakuwa na mlinzi/ulinzi badala ya kuhoji kwa nini haya yatokee katika jiji ambalo linatakiwa kuwa salama na kwa kiongozi mkubwa wakati kuna idara inayoshughulikia usalama wa raia!
 
Mimi sitetei uovu,natoa angalizo in future mjipange,,kama tukio la lisu halikuwafanya mjipange,,ina maana kuna uzembe,,mwenyekiti wa chama kitaifa,anatembeaje usiku wa manane mwenyewe?,
Huoni hapo,wamestudy movements zake na wanajua wapi pa kumbana akiwa alone,
Hii maana yake,ni kuwa wangetaka kumaliza,wangemaliza maana alijiweka easy target,,kama hamjifunzi kwa haya matukio,then hamko serious

Angalizo lako lina upogo...

Je, siyo jukumu la serikali kuhakikisha ulinzi na usalama wa RAIA na MALI ZAO?

Unaweza kuwa na walinzi hata 30 kuzuia vibaka, lakini kama "mamlaka batili ya kidola" imekusudia kuku - terminate au kukutia kilema, haitazuiwa na watu 30 wenye visu na virungu tu kukulinda...!

Fikiri vizuri kabla ya ku - argue....
 
So SAD why did Mbowe deserve this? WHY WHY WHY. This is a WAKE UP CALL for all Tanzanians who are FED UP with this CROOK and his PUPPETS
Nonsense, yaani aumizwe Kwa madhambi yake mseme Serikali.
 
Angalizo lako lina upogo...

Je, siyo jukumu la serikali kuhakikisha ulinzi na usalama wa RAIA na MALI ZAO?

Unaweza kuwa na walinzi hata 30 kuzuia vibaka, lakini kama "mamlaka batili ya kidola" imekusudia kuku - terminate au kukutia kilema, haitazuiwa na watu 30 wenye visu na virungu tu kukulinda...!

Fikiri vizuri kabla ya ku - argue....
Hakuna kibaka anaweza kurisk confrotationa ya watu zaidi ya watano wanaokulinda,,by kibaka i mean bad guy,,hiyo sasa itakuwa mapigano na wala siyo shambulizi(physical assault),je kuna mtu anaweza risk mapigano hata kama katumwa na mafia boss au crime syndicate yeyote?
 
Hii ni habari ya kushtua na kusikitisha lakini pia kwa jinsi ilivyoripotiwa inaacha maswali mengi. Tumwombee apone na tutafute taarifa za nini kimetoea badala ya mara moja kuelekeza mawazo ya watu kwenye jambo fulani.

Bila kuwa na facts hatujui ni "wahuni" au ni "watu wasiojulikana" na alivamiwa akiwa kwenye gari au alikuwa anatembea kwa miguu, akiwa na kina nani n.k ni muhimu tupate taarifa za uhakika. Dunia hii ina mengi sana... na siyo yote yako kama tunavyodhania au kuaminishwa...
Hutapata taarifa wataficha ukweli na kutunga mengine. What goes around always comes around. Shame mda huo alitoka wapi?
 
Hivi unaweza ku sacrifice mguu uvunjike just tu kwa ajili ya kuwin public sympathy?
Kwani amewaumiza wangapi ndani ya Chama?
Naunga Mkono hoja, ni wakati wake sasa kulipa.
Unalala na wake za watu, kila girlfriend wa mwenzio unamtamani, hutaki mtu akuguse.
 
Kwa mara nyingine tena, wale wale wanaohubiri amani, umoja na ushirikiano ndio hao hao wanaoongoza kwa maneno ya kejeli, dhihaka na dharau dhidi ya Mbowe. Niwakumbushe tu Mbowe ana familia, ana ndugu, ana wafuasi na kiongozi. Mbowe si mhalifu, Mbowe si jambazi, kumsemea maneno ya kejeli na dhihaka hivi sidhani kama ni sahihi.

Tanzania si mali ya CCM wala ya mtu binafsi, nashindwa kuelewa kama tukio hili lingetokea upande wa CCM na Pro Chadema wakasema chochote kile, wangejitokeza watu hapa na kudai kuwa Mwenyekiti anadharauliw ana blah blahblah kibao.

Niwashauri tu, kwa kile ambacho hamko tayari kufanyiwa basi msiwafanyie wenzenu, muda ni mwamuzi mwaminifu asiye na upendeleo.
 
Back
Top Bottom