Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Dodoma: Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe avamiwa, apigwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana

Ila vitu vingine jamani, inamaana Mbowe hana bodigadi,yaani anatembea bila walinzi?? Diamond ana bodgad sembuse Kub?? Tuache maigizo basi
kwa hiyo kilichotokea ni maigizo si ndio ? kuvunjwa mguu ni maigizo? kenge wewe
 
Unajua ana Mke na watoto, hivyo haiwezekani kimada au awe mchepuko, itakuwa ni "wahuni" hii kisiasa na kifamilia ndio inakaa vizuri zaidi.

Na zaidi ya hapo hakuwepo hapo Maisha club sababu ya lockdown ya nchi jirani maana sisi hatufuati who directives , watakuwa "wahuni" wamemleta hapo
Yaani kama ndio siasa hizi, hii chuki inayopandikizwa itatughalimu siku moja.
 
20200609_162155.jpg


Tumuombee Mh Mbowe apone haraka
 
Mkuu Elli nafikiri wewe sio msomaji wa mtandao huu wa JF au umeamua kukataa kitu ambacho kila mchangiaji wa mtandao huu anajua labda wewe tuu.

Ukitaka kuona matusi, maneno ya karaha, dhihaka, manyayaso hata kukufuru angalia michango ya uzi wowote ule ambao Chadema wanauona ni hasi kwao.
Naweza kuleta komenti zaidi ya 200 wacha moja ambazo zitathibitisha haya.

Kuna mabadilika ambayo nayaona yanakuja kidigo kidogo ambayo wachangiaji wa mrengo wa Chadema na CCM wanaelekea kutoshana nguvu.

Mbona unajilisha upepo ndugu bila sababu yoyote? Mbona una argue mambo kwa hisia (emotions) zako badala ya uhalisia...?

Kama wewe unaona "karaha" kutoka kwenye baadhi ya maoni (comments) ya watu humu kwa kuwa ziko "hasi" na "interests" zako, basi tatizo siyo comments hizo bali tatizo halisi ni wewe mwenyewe...!

Hebu nikuulize maswali kadhaa na ukiweza kuyajibu kwa usahihi bila kuidhulumu nafsi yako, itapendeza na kukusaidia sana;

Tuambie, una maana gani kusema unaweza kuleta comments "hasi" na zenye "karaha" na "matusi" za wana CHADEMA 200?..

Umetumia kipimo gani tusichokijua sisi kuwatambua members wote wa JF kwa "nembo" zao za vyama vyao vya siasa?

Au ni lini na kwa kutumia vigezo gani hasa umeweza kuwa - classify members wa JF wote kuwa huyu ni CHADEMA , huyu ni CCM, huyu CUF, huyu ACT Wazalendo, huyu CHAUMA, huyu TLP na huyu hana chama nk nk?

Hebu tuambie umewezaje ndugu? Umetumia vigezo gani?...

Je, kwa kutumia kigezo hiki unachosema; "comments au maoni HASI na yenye KARAHA na yenye MATUSI " dhidi ya CCM na Magufuli?

Kipimo na tafsiri ya jumla (si yako wewe peke yako) ya; u - HASI, u- KARAHA na u - MATUSI ni ipi?

Kama utajibu maswali haya kwa uaminifu na kwa dhati ya moyo wako bila kuidhulumu nafsi yako haki yake, utagundua kuwa "arguments" zako zinatawaliwa mapenzi na hisia mbaya na mbovu za kisiasa zilizovuka mipaka ya ustaarabu pasipo kuwa na uhalisia...!!

Nikuambie kitu kimoja tu kwa nia ya kukuelimisha kuhusu jambo moja muhimu sana ktk uhalisia wa maisha ya binadamu...

Kwamba, kutofautiana kimitazamo ni jambo la kawaida miongoni mwa wanajamii iwe ndani ya familia moja, kati ya wanandoa, wafanyakazi kwenye shirika ama kampuni moja na wanachama wenyewe ndani ya chama cha siasa...

Mfano, ndani ya CCM kwenyewe huwa kuna kutofautiana kimawazo. Lakini haiondoi ukweli kuwa wote hao bado wanakuwa wanachama wa chama kimoja...

Kama utakereka kwa kuwa tu mawazo yako hajaungwa mkono na wenzako, kama nilivyosema tangu awali kuwa, tatizo linakuwa siyo mawazo hasi ama yenye karaha ya wenzako. Tatizo halisi unakuwa ni wewe...!!

Mara nyingi watu wa dizaini yako, wasio na "kifua" cha kupokea mawazo ya kuwakosoa ama kuwapinga ama yaliyo kinyume na matakwa yao huwa ni wabinafsi (selfish) na mtu mbinafsi mara nyingi "option" yake ya mwisho akishindwa kwa hoja, ni kumdhuru mpinzani wake na kama ana uwezo atamuua kabisa...!

Hawa watu hawana sifa ya kuwa viongozi ktk jamii. Wanapaswa kuwa viongozi wa kujiongoza wao wenyewe tu....!

Kwa hiyo kama mnatumia kigezo hiki kupiga watu risasi ama kuwateka na kuwapoteza na kuwajeruhi wengine kama ilivyotokea kwa Mh. Freeman Mbowe leo, mnafanya vibaya na mnaonea watu bila sababu....
 
Toka lini hospitali za Dar zimeanza kuaminika kuwa na ulinzi madhubuti wa kuwazuia wasiojulikana ili wasimdhuru zaidi Mwamba? mpelekeni mr. dj ubelgiji ili akatibiwe huko kama Lissu.
Ninaanza kuwa na woga hata kuandika. Ila tunakoelekea ni kubaya sana . tutaanza kuona visasi vikilipizwa kwa kuvizia na mwisho hatutakuwa na utulivu. Tuache kucheza na uhai wa watu
 
Mtu anajipiga mwenyewe kutafuta huruma ya wananchi tu, machadema mbona mna mbinu za kitoto sana!!
Wewe wazazi wako walipoteza mbegu zao,they wasted spam. Wasingepoteza muda kuzaa mtu kama wewe . nonsense
 
Mlinzi wa Mbowe alikua wapi au KUB wetu hana ulinzi? Chadema hawajapata somo kwa Lissu?mbona hiki chama wazembe hivi. Kiongozi kama Mbowe alitakiwa awe na ulinzi mkali
 
Regime hii inaenda mbali sana.
Natarijia MUROTO atawatafuta hao WAHUNI waliompiga MWAMBA.
Kama ni kwelii Basi Taifa limefikia hatua mbaya Sana Toka tupate Uhuru,
Mbowe amekuwa mtu wa busara busara nyiiiiingi hata mahali zisipohitajika/anapoonewa tofauti kabisa na Kina Lema na yule mbunge wa kule Nyamongo ambao wao ni watu wamisimamo kama ni mbaya iwe mbaya tu.

Sasa acha Mbowe apewe kichapo kidogo akitoka hosp. Nadhani atapnguza zile busara busara zake ambazo hua zinapelekea kuonewa bila mpango.
Mimi nina mashaka Inawezekana hizi ni njama ndani ya chama kumpoteza Mbowe ili kuwapokonya watu wa Kilimanjaro Chama chao.
Lissu hizo gharama za kukaa ulaya unataka kuzilipa kwa kuwapa mabeberu rasilimali zetu pale utakapoingia ikulu.
Hatukuhitaji mtu kama wewe awe rais
Unajua watanzania tunasahau kirahisi sana. Kumbukeni ule ujumbe wa Gwajima kwa wana-ukoo wake kuhusu kumlinda rais kwa hali na mali mtaelewa nini kinaendelea. Nchi imeharibiwa sana na hawa watu...
 
Ingekuwa kwa wenzetu uchunguzi wa kina ungefanyika maana kama ni eneo lenye ulinzi wa kutosha means hata CCTV zipo za kutosha ilanahakika Jeshi lapolisi litashindwa pata watuhumiwa, nakumbuka kipindi cha lissu alipiga sana kelele kuhusu gari inayomfatilia na hata plate number matokeo yake gari ilikuwa haijulikani,

Lissu alisema kuna CCTV ila nazo nahis picha zilifutika ... ifike mahali watawala waseme hawautaki upinzani basi lijulikane moja maana this is too much ni wangapi watapewa majeraha ya kudumu, wangapi watapewa ulemavu wa kudumu kama Lissu na wangapi watauwawa kisa siasa?
hata kama watapewa wengi majeraha ya kudumu usiku haukawii kucha. Tumekaribia sana mapambazuko
 
Kwanini kama Rais amekuwa Kimya juu ya Matukio haya ambayo yameota Mizizi hasa katika Awamu yake hii na wala hayakemei kabisa Ndugu?
Kweli aisee, kwa nini ameendelea kuwa kimya ilhali washenzi wachache wanamharibia sifa kitaa? Ukimya wake unamaanisha nini kwa watu wake hasa kwa matukio haya?
 
Unapo Muongelea Mbowe ni Mwenyekiti wa chama,Mbunge,kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,mwenye ukinzi,Gari na Dereva na nauhakika hata silaha ya kujilinda anayo,siyo mtu wa kawaida Kama mm na ww na wengine,Sasa eti anakamatwa na vibaka na kupigwa,na kuvunjwa miguu!saa sita usiku,kweli?Nchi yetu Ina usanii wakila aina jamani,Daaah
 
Back
Top Bottom