Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Hii ni kwa waliofika mitaa ya ushuani Dodoma kwa hivi karibuni.

Naishi dsm, lakini nimeishi dodoma 5 years back, nimekaa Arusha na Mwanza pia.

Sikatai Dar ndio baba lao kwa Tz kwenye vitu vizuri hasa Makazi.
Kama umefika Dodoma hivi karibuni au hata kuangalia insta, Tiktok utaona real estate ya Dodoma inakuja kwa kasi mno hata Dar ikasome kuanzia Apartments, hotels, AirbnB etc

Hizi ni baadhi ya sehemu ambazo ukitembelea utakubaliana na mimi.

1. Itega - ianshika namba moja kwa Dodoma, wanaishi wazito huu mtaa uliopo chini ya mlima kama unaenda gereza la isanga. Sharti la kujenga ni kuanzia ghorofa moja, kiwanja kuuzwa 1 billion sio jambo la kushangazwa kutokana na value ya eneo na kumepangwa kweli kweli hiyo Mijengo Mbweni JKT akasome.

2. Njedengwa- naipa namba mbili, huu mtaa upo chini ya mlima kama unaenda iyumbu kule Udom. Kuna makazi ya watu, taasisi za umma na binafsi kama Tume ya Uchaguzi HQ. Huku kuna balaa watu wamejenga hadi unasema pesa wamepata wapi. Kwa kuongezea kuna Hotel Mbili za Nyota tano zinajengwa, ile ya Bunge la Afrika kushirikiana na Bunge Tz pamoja na ile ya NSSSF ili kuendana na kasi ya Jiji lakini kuhost diplomats, UN guests and high profile foreigners watakao kuwa dodoma msalato international airport ikikamilika.

3. Mkalama/ Makulu Oyster bay
Huu mtaa una washua balaa, kina Biteko etc wameshusha vitu na apartments zile za modern luxury zinajengwa na zingine zipo tayari.

4. Ilazo - kumenyooka huku hamna slums ni vitu fulani hivi vya kishua na barabara kiwango cha lami kwenye mitaa yake.

5. Medeli - Huku ndio kuna shopping malls, restaurants, ofisi za umma na bifnafsi na hotels za kisasa, in short panakuwa kwa kasi sana. Kiwanja kuuzwa 2 billion sio maajabu huu mtaa.

6. Kisasa- huku ni kama Sinza ya Dar, kumechangamka sana yaani ni mtaa unajitosheleza karibia kila kitu, tofauti na sinza huku hamna slums, kumepangwa vizuri barabara za mtaa almost zote zina lami.

7. Mlimwa C - huku ndio kule kwa Waziri Mkuu, chini ya mlima watu wanashusha mansion kama uyoga ndipo kuna royal village.

8. Mtumba City - kwasasa kuna modern state of art ministerial offices, ila kwa baadae patakuwa kufuru kutokana na modern hotels, restaurants and apartments ambazo zipo underway.

Sehemu zingine kuna Iyumbu, Ntyuka, Tambuka reli street etc

Dodoma Uncle magu angekuwepo sijui tungekuwa tunaongea nini.

Kwasasa ndio Jiji la tatu linalokuja kwa kasi baada ya Dar na Mwanza, hivyo Mwanza kaa tayari kushika namba tatu by 2030
Tofauti nyingine ya Kisasa na Sinza ni kwamba Kisasa hakuna uhalifu wa kishamba shamba.
 
Basi tu hawa mabilionea zetu sijui akili zinaendaga wapi, nadhani Dom ndo mahala pa kutega.

Dom Wala Bata wengi vyuo vingi wana boom hivo pesa sio KESI, ila hakuna sehemu ya kupumzika weekend, nenda tafuta eneo nje ya mji hata km 40 kutoka city center dondosha man made beach ya kisasa wekeza pesa sana bonge Moja la beach na hotel za kisasa ikiambatana na zoo ya wanyama wachache, utanipa habari, hizi marathon vutia kule kwako beach kupatangaza, mkuu huo uwekezaji utakulipa mpaka wajukuu zako.
 
Dodoma ni Modern City, Dar ni old city with modern buildings and slums kitu ambacho dodoma hakipo.

Pia, Dar kunanuka sana jamani, hakujapangwa kuanzia makazi, barabara hamna hata city parks?
Mwambie hata watu kutoka Lagos wakija kufanya study tour Tanzania wanakuja Dodoma,hawaendi Dsm kwa sababu hakuna la maana la kijifunza.
 
Basi tu hawa mabilionea tunatakiwa, nadhani Dom ndo mahala pa kutega.

Dom Wala Bata wengi vyuo vingi wana boom hivo pesa sio KESI, ila hakuna sehemu ya kupumzika weekend, nenda tafuta eneo nje ya mji hata km 40 kutoka city center dondosha man made beach ya kisasa wekeza pesa sana bonge Moja la beach na hotel za kisasa ikiambatana na zoo ya wanyama wachache, utanipa habari, hizi marathon vutia kule kwako beach kupatangaza, mkuu huo uwekezaji utakulipa mpaka wajukuu zako.
Mkuu umewaza mbali, ungekuwa na capital nadhani ungetimiza ndoto.

Kweli matajiri wa bongo bado hawajawa serious na dodoma.

Naona wachina wameanza kushitukia mchezo kwa kuanzisha Viwanda baada ya Bandari Kavu kukamilika, kuna Don mchina anaanzisha kiwanda cha Steel kikubwa Africa mashariki.

Dodoma ina maeneo mengi nje ya mji hayana muwekezaji hii ni Fursa kwa mtu anayeona mbele before its too late.
 
Aaah kumbe mkongwe, kuna mshikaji wangu alinunua Kiwanja huko Zuzu karibu na kwa Pinda, saivi anasema vimepanda bei kwasababu lami imefika huko Zuzu
Eeh ni kweli,hata Mimi Kuna uncle huko ana heka15, anasema Kwa Sasa hea1 ni M20, Wakati Yeye akinunua elfu 50 Kwa Kila Hela,najuka kutonunua kipindi hicho mwaka 2000.
 
Harufu mbaya.

Dar hata uwe City center kunanuka vibaya sana
Michael Jackson aliziba pua aliposhuka tu Airport, Obama ilibidi wafagie na kupiga fumigation kuondoa harafu lakini wapi.
Yaani chemba zinatema balaa, hapa Sinza ukitokea kitambaa kuja mwenge kuna chemba zinamwaga uchafu barabara ya lami na haina mitaro ukipita unaziba pua
 
Back
Top Bottom