Dodoma ndio Jiji lenye modern real estate kwa Tanzania

Meja G. M. Kimario - CDA enzi hizo alifanya kazi ya kutukuka kuipanga Dom.
Tuliopata mapori enzi hizo, kwa sasa wajukuu wetu wanaomba tufe wauze makumi ya viwanja tulivyovipata vikiwa mapori.
Daah inanipa hasira hii kupishana na fursa, natamani sana kuwekeza kwenye real estate ila pesa bhana ndio kipengele.
Dodoma kweli ukiona juu kwa drone pamepangika vizuri sana, hasa hiyo mitaa ya washua yaani imechorwa na kupangwa kwa umahiri mkubwa.
 
Mkuu nunua hata ekari Moja inatoa viwanja 5,6vya sqmeter 600!
 
Uza kidogo, kidogo ya nini Shida!
Pale Mtumba kuna taasisi fulani zipo juu ya ardhi ambayo ilinunuliwa kama pori na Marehemu Mzee wangu, tulilifanya ni "runch" miaka hiyo.

Msalato kule airport mpya pia vile vile.

Mithali 19 : 14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
 
Mkuu umewaza mbali, ungekuwa na capital nadhani ungetimiza ndoto.

Kweli matajiri wa bongo bado hawajawa serious na dodoma.

Naona wachina wameanza kushitukia mchezo kwa kuanzisha Viwanda baada ya Bandari Kavu kukamilika, kuna Don mchina anaanzisha kiwanda cha Steel kikubwa Africa mashariki.

Dodoma ina maeneo mengi nje ya mji hayana muwekezaji hii ni Fursa kwa mtu anayeona mbele before its too late.
Kaka nimesoma hapo chuo napafahamu sana nimepiga harakati kibao sana, Arusha starehe zao weekend, nimeishi pale, Dodoma starehe zao kila siku alafu ni vibe mwanzo mwisho, Dodoma msanii anaweza piga show katikati ya week na akajaza Kwa kiingilio, Arusha weekend,

Vyuo vinaendelea kujengwa, vilivyopo bado ni vingi, changamoto ya Dodoma wamewekeza kwenye bar tu watasahau maeneo ya kupumzika raia mana Dom wenye kipato ni wengi tena si kidogo ni kikubwa, binge lilianza wabunge hawana maeneo ya kupumzika tofauti na hotelini basi, man made beach inge piga hela sana unakaba eneo hii ukitoka mji wa serikali kuelekea ihumwa hapo kati bado Kuna site japo ni ghali kaba maeneo hapo au chini huko
 
Kwanini unasema gharama za upkeep and utility services kwa dodoma ni ngumu kuliko Mwanza au Dar?
Dodoma ni eneo lenye ukame wa asili, gharama za kupata maji safi ni kubwa kwa sababu vyanzo vya maji viko mbali na vinahitaji miundombinu ghali ya pumping kupitia mabomba marefu.

Dar na Mwanza wana fursa kubwa ya vyanzo vya maji vya karibu na vya uhakika.
 
Pale Mtumba kuna taasisi fulani zipo juu ya ardhi ambayo ilinunuliwa kama pori na Marehemu Mzee wangu, tulilifanya ni "runch" miaka hiyo.

Msalato kule airport mpya pia vile vile.

Mithali 19 : 14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Vipi uliuza au ardhi ilitwaliwa kwa kulipwa fidia?
 
Dodoma ni eneo lenye ukame wa asili, gharama za kupata maji safi ni kubwa kwa sababu vyanzo vya maji viko mbali na vinahitaji miundombinu ghali ya pumping kupitia mabomba marefu.

Dar na Mwanza wana fursa kubwa ya vyanzo vya maji vya karibu na vya uhakika.
Dodoma maji yapo juu bwashee, nyumba nyingi saivi wanatoboa mwamba mita chache maji haya hapa.

Mwanza hiyo kila siku wanalia uhaba wa maji?
 
Daah inanipa hasira hii kupishana na fursa, natamani sana kuwekeza kwenye real estate ila pesa bhana ndio kipengele.
Dodoma kweli ukiona juu kwa drone pamepangika vizuri sana, hasa hiyo mitaa ya washua yaani imechorwa na kupangwa kwa umahiri mkubwa.
Jifunze kitu kimoja. Hakuna pori milele.
Waweza nunua eneo ambalo ni pori leo, lakini kesho lilaja kukupa thamani mara milioni moja ya uliyonunulia pori hilo.

Goba ilikuwa ni pori, hata mashamba ni wachache tulikuwa tunalima,leo hii kiwanja cha meter square 700 tunauza 70M ilhali pori lilinunuliwa kwa tsh 2400 - ekari 7.
 
Pale Mtumba kuna taasisi fulani zipo juu ya ardhi ambayo ilinunuliwa kama pori na Marehemu Mzee wangu, tulilifanya ni "runch" miaka hiyo.

Msalato kule airport mpya pia vile vile.

Mithali 19 : 14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Wewe tajiri mkuu,usilalamike Hali ngumu!
 
Jifunze kitu kimoja. Hakuna pori milele.
Waweza nunua eneo ambalo ni pori leo, lakini kesho lilaja kukupa thamani mara milioni moja ya uliyonunulia pori hilo.

Goba ilikuwa ni pori, hata mashamba ni wachache tulikuwa tunalima,leo hii kiwanja cha meter square 700 tunauza 70M ilhali pori lilinunuliwa kwa tsh 2400 - ekari 7.
Sahihi mkuu!
 
Dodoma maji yapo juu bwashee, nyumba nyingi saivi wanatoboa mwamba mita chache maji haya hapa.

Mwanza hiyo kila siku wanalia uhaba wa maji?
Hiyo groundwater mining ukiangalia kwa jicho la kitalaamu, sio suluhu endelevu kwa sababu.

Maji ya kwenye miamba ya Dodoma recharge rate ni ndogo sana kutokana na hali ya hewa ya ukame, huko kuchimba visima vingi vya watu binafsi ndiyo kunashusha water table na kusababisha hivyo visima kukauka baada ya muda mfupi.

Tatizo la Mwanza kulia na uhaba wa maji ni kutokana na infrastructure ,kushindwa kusambaza maji kutoka ziwani, Dodoma tatizo lao ni resource scarcity. Ni rahisi zaidi kujenga mabomba ya kusambaza maji kutoka Ziwa Victoria kuliko kutengeneza maji kwenye mji usio na vyanzo vya kudumu.
 
Back
Top Bottom