"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga
====
Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.
Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22
“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.
Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.
Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”
Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”
Ushauri ni kuwa, atafute kazi yenye mshahara mkubwa. Maana kuna watu wengi hulalamika kuwa mishahara ni midogo. Wamechukua hatua ya kutafuta kazi sehemu nyingine.
Mbuge wa ajabu sana, Kama anataka fedha/hera jibu ni Kujitoa afanye biashara. Kazi yoyote ya Kuajiliwa haina fedha za Kutanulia. Hata hivyo kama anaona aliburge steps arudishe Jimbo watu ni wengi wa kuwatumikia watanzania. Mbuge wa ajabu sana, kumbe aliwaambia wananchi wake kuwa atarudi kwao na hera...bure kabisa sijui anatoka Chama gani???
Maganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, mkoa wa Geita. Ñinakushauri, kama mshahara haukutoshi nenda kachimbe dhahabu jimboni kwako. Vinginevyo 2025 nafasi hiyo utasikia radioni.
Mpuuzi sana huyu!!! Yeye kama milioni 11 kwa mwezi na rupurupu nene bado hatosheki anawaambia nini Wafanyakazi ambao hawapati hata robo ya mshahara wake?
"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga
Mbunge wa aina hiyo na wale waliomshangilia ndio wanategemewa kupigania maslahi ya wapiga kura wao majimboni, wakati wao wenyewe wanawaza matumbo yao, hawa walienda bungeni kutafuta maslahi, kama wanaona mshahara hauwatoshi kwanini wasiende kufanya biashara?