Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono hoja, aongezewe, lakini kabla ya kuongezewa atuoneshe ameongeza sh ngapi kwenye mfuko wa taifa: Ukiwa na akili timamu huwezi kumwambie bibi yako ukuongezee kiporo wakati unga uliopika kiporo ilikuwa Robo kiloHUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
Huyo Maganga ni mchimbaji kitambo ndo maana anaona mshahara wa wabunge ni visenti tuMaganga, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, mkoa wa Geita. Ñinakushauri, kama mshahara haukutoshi nenda kachimbe dhahabu jimboni kwako. Vinginevyo 2025 nafasi hiyo utasikia radioni .
Huyo Maganga ni mchimbaji kitambo ndo maana anaona mshahara wa wabunge ni visenti tu
Hawa walikuwa wanatumia ubunge kupitisha biashara zao za magumashi baada ya serkali kuwa macho ubunge sasa hauna maana kwa kuwa imekuwa kusubiria mshara na posho tu.Uyo hatoboi 2025...
Hizi ndiyo takataka mwendazake alizototuachia, wakati wafanyakazi wa Serikali wakilia kutokuongezwa mishahara kwa miaka sita dhalim alikuwa anawajibu kuwa kama wanaona mishahara haiwatoshi waende wakalime,lakini yeye katujazia vilaza Bungeni wanaoliopwa zaidi ya 12 kwa mwezi bila kukatwa kodi na bado wanaona hazitoshi. Hakika huko aliko dhalim lazima aongezewe adhabu"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga
====
Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.
Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.
Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.
Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”
Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”
Chanzo: Mwananchi
View attachment 1826321
HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
Na mataahira wenzake walikuwa wanamshangilia na kugonga meza kabisa.hawa wabunge wa CCM wameshajua watanzania wote ni wapuuzi.