Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwakilishi wa wananchi anataka afanane na wabunge wa nchi zingine kwa kulipwa pesa ndefu,na maslahi manono kama wabunge wa nchi zingine,hicho ndio kipaumbele chake,"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga
====
Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.
Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.
Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.
Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”
Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”
Chanzo: Mwananchi
View attachment 1826321
HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
HahahahaaaAkumbuke kuna mbunge mwenzake alsema hapa juzi juzi kuwa kwa utamu wa bunge anaweza hata akaua mtu.
Wabinafsi sanaWapumbavu hao wabunge. Hawakatwi chochote kwenye malipo yao halafu wanataka zaidi?Hivi hao wahuni wanatuona sisi zombies sio?
upinzani ulituchelewesha sana!Ni ombi lilioshangiliwa sana bungeni baada ya kutolewa na Mbunge wa Mbogwe akiwa amevaa suti ya ki-kongo, alisema mengi na nimeona mambo kadhaa:
1. Alishangiliwa na Bunge zima
2. Naibu spika naye aka-smile kwa wema wa mbunge
3. Mifano ya kuigwa ni nchi za Kenya na Afrika ya kusini
4. Anaomba walipwe kwa dola
5. Anaomba wabunge wasiwaogope wananchi
Wana JF hili linahitaji mjadala. Mbunge asiyewaogopa wananchi anawezaje kulisaidia taifa? Mifano ya malipo ya wabunge bila kutoa mifano ya malipo ya waalimu, madaktari, n.k anawasaidia nini wa-TZ? Binafsi nahisi ni ombi la makusudi, la kutengeza ndani ya Bunge na kumsukumia mmoja wao mwenye akili za hivyo, aseme.
Hofu yangu ni udhaifu wa rais wetu ambaye katika kutafuta support ya chama aonekane ni mwema kwa wenzake wa CCM, tutajikuta wameongezwa kimya kimya.
Mibunge ya Tanzania ni miradi sana... Haipo hapo kwa ajili ya Wananchi bali mitumbo yao."Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga