Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

99% ya bunge ni zao la udikteta ulioshamiri kwa miaka 5..

Ajabu tulipokuwa tukikemea wananchi waliaminishwa wapinzani ni vibaraka , wapambe wa mabeberu na wachelewesha maendeleo ilhali wapinzani waliongea vile alivyokua hataki kuvisikia dikteta...

Ok ni payback time ! Wote mlioshiriki kubariki udhalimu ule na kuutekeleza kuleni matunda yake sasa
 
naona kilicho mpeleka bungeni ni mshahara sio wanajimbo lake
nashauri tu ndugu zangu tuchague viongozi weny maono katika jamii zetu na sio wabinafsi wenye tamaa
maendeleo hayana chama
 
Yaani kwa huo mchango wake wa dakika kadhaa na kupiga kura kupitisha bajeti Jamaa kalamba 300K. Kwa nini asituone sisi malofa.
 
"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga

====

Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.

Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.

Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.

Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”

Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”

Chanzo: Mwananchi


HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
hizo pesa za kuwaongezea mishahara wazitumie kuajiri vijana walio na elimu zao za nguvu ambao bado wapo mitaani na serikali wanajifanya hawawaoni.
 
Habari za jioni Wana JF Mimi binafsi nimefedheheshwa,nimekelwa pia nimeumia baada ya kumsikia mbunge mmoja huko Dodoma akilalamika kwamba maslahi yao Ni madogo kwaio serikali iangalie namna ya kuwaongezea.Naamini hili swala limetushtua wengi tunaofuatilia Mambo ya kisiasa nje na ndani ya nchi hii ya Tanzania.Wote tunajua ubunge ndo nafasi ya kisiasa yenye mshahara,posho nzuri na marupurupu mengine.kwakua wananchi ndo tumewachagua wakatuwakilishe Kama wameona mishahara haitoshi basi waachie izo nafasi Mara moja maana mpaka Sasa hatulioni bunge Kama chombo muhimu kinachoisimamia serikali Kama nchi zingine zaidi ya kuona ubabaishaji tu ukiendelea huku Kodi za wananchi wa Tanzania zikiendelea kutumika vibaya.kwa vile Rais wetu alituambia tukikosoa tutoe na mapendekezo .Basi Mimi napendekeza kwenye dunia hii sayansi na teknolojia Basi utengenezwe utaratibu mzuri kila mtu awasilishe maoni yake kwenda kwa katibu tawala wa wilaya DAS then DAS atapeleka kwa RAS then RAS atapeleka kwenye wizara zinahusika kulingana na jinsi changamoto za wananchi zilivyo chambuliwa .maana wawakikishi ndo Kama ivyo tunaona wapo bize kupigania matumbo yao.
 
Mpuuzi sana huyu!!! Yeye kama milioni 11 kwa mwezi na rupurupu nene bado hatosheki anawaambia nini Wafanyakazi ambao hawapati hata robo ya mshahara wake?
Tena hiyo kidogo yenyewe , wafanyakazi hawajaongezewa mishahara kwa miaka 6.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mimi nashauri tuweme mechanism ambayo wananchi wanaweza kumrecall mbunge ambaye walimchagua lakini wanaona amekengeuka na hawakilishi Tena Interest zao.
 
Khahahaha,wakatwe kodi kwanza halafu waharishe huo uharo wa kijani.Kwa maoni yangu nadhani bunge ndo taasisi inayoongoza katika kufirisi nchi.Ukiacha dawa na ujenzi wa miundombinu.
 
INASIKITISHA SANA HII NCHI YETU, HAWA WASIOLIPA KODI NDIO WANADAI NYONGEZA YA MISHAHARA, WATANZANIA TUNGEKINUKISHA SIKU MBILI TU WATANYOOKA HAWA LIKKY
 
Wacha wee!
hii inafanana kama pale unapomkaribisha ngamia baada ya malalamiko makubwa kuwa mvua inamnyeshea hivyo umruhusu japo kichwa tu aweze kujistiri kwenye kibanda chako kidogo cha nyasi baadaye anajisahau anainuka na kuvunja kibanda.
tumewapa kura zetu zilizowasaidia kupata kula sasa mwalalamika haziwatoshi?
 
Back
Top Bottom