Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

Mbuge wa ajabu sana, Kama anataka fedha/hera jibu ni Kujitoa afanye biashara. Kazi yoyote ya Kuajiliwa haina fedha za Kutanulia. Hata hivyo kama anaona aliburge steps arudishe Jimbo watu ni wengi wa kuwatumikia watanzania. Mbuge wa ajabu sana, kumbe aliwaambia wananchi wake kuwa atarudi kwao na hera...bure kabisa sijui anatoka Chama gani???
1624379412366.png
 
"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga

====

Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.

Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.

Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.

Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”

Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”

Chanzo: Mwananchi

HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
Wananchi wampumzishe aende ziliko posho
 
Habari za jioni Wana JF Mimi binafsi nimefedheheshwa,nimekelwa pia nimeumia baada ya kumsikia mbunge mmoja huko Dodoma akilalamika kwamba maslahi yao Ni madogo kwaio serikali iangalie namna ya kuwaongezea.Naamini hili swala limetushtua wengi tunaofuatilia Mambo ya kisiasa nje na ndani ya nchi hii ya Tanzania.Wote tunajua ubunge ndo nafasi ya kisiasa yenye mshahara,posho nzuri na marupurupu mengine.kwakua wananchi ndo tumewachagua wakatuwakilishe Kama wameona mishahara haitoshi basi waachie izo nafasi Mara moja maana mpaka Sasa hatulioni bunge Kama chombo muhimu kinachoisimamia serikali Kama nchi zingine zaidi ya kuona ubabaishaji tu ukiendelea huku Kodi za wananchi wa Tanzania zikiendelea kutumika vibaya.kwa vile Rais wetu alituambia tukikosoa tutoe na mapendekezo .Basi Mimi napendekeza kwenye dunia hii sayansi na teknolojia Basi utengenezwe utaratibu mzuri kila mtu awasilishe maoni yake kwenda kwa katibu tawala wa wilaya DAS then DAS atapeleka kwa RAS then RAS atapeleka kwenye wizara zinahusika kulingana na jinsi changamoto za wananchi zilivyo chambuliwa .maana wawakikishi ndo Kama ivyo tunaona wapo bize kupigania matumbo yao.
Wasitukorofishe,wameshindwa kwa muda mrefu kuwasaidia wenye njaa,wakati wao hawakuwahi kupatwa na njaa.Tena kuwakumbusha tu wapo walionyiwa haki za msingi,miaka 6,kuelekea saba,wengi wao kwanza wasitake tuwakumbushe wamefikaje hapo na kuona Wana haki ya kujiombea maslahi bora,wakati wapo wengi wasiojua maslahi japo ya kawaida ni yapi,licha ya liyokuwa bora.
 
Habari za jioni Wana JF Mimi binafsi nimefedheheshwa,nimekelwa pia nimeumia baada ya kumsikia mbunge mmoja huko Dodoma akilalamika kwamba maslahi yao Ni madogo kwaio serikali iangalie namna ya kuwaongezea.Naamini hili swala limetushtua wengi tunaofuatilia Mambo ya kisiasa nje na ndani ya nchi hii ya Tanzania.Wote tunajua ubunge ndo nafasi ya kisiasa yenye mshahara,posho nzuri na marupurupu mengine.kwakua wananchi ndo tumewachagua wakatuwakilishe Kama wameona mishahara haitoshi basi waachie izo nafasi Mara moja maana mpaka Sasa hatulioni bunge Kama chombo muhimu kinachoisimamia serikali Kama nchi zingine zaidi ya kuona ubabaishaji tu ukiendelea huku Kodi za wananchi wa Tanzania zikiendelea kutumika vibaya.kwa vile Rais wetu alituambia tukikosoa tutoe na mapendekezo .Basi Mimi napendekeza kwenye dunia hii sayansi na teknolojia Basi utengenezwe utaratibu mzuri kila mtu awasilishe maoni yake kwenda kwa katibu tawala wa wilaya DAS then DAS atapeleka kwa RAS then RAS atapeleka kwenye wizara zinahusika kulingana na jinsi changamoto za wananchi zilivyo chambuliwa .maana wawakikishi ndo Kama ivyo tunaona wapo bize kupigania matumbo yao.
Kwa kilichofanyika kwa kilichoitwa chaguzi,wanajiwakilisha wao.
 
Tusiwaogope Wananchi kasema! alafu anasema siku zimebaki chache arejee jimboni wananchi wanajua anahela hivyo anawaogopa... Bunge lifanane kimasilahi kama la South Africa aisee... hivi uchumi pia aseme ufanane pia basi
 
Wabunge hela zote hizo bado tu hawatosheki? Mbunge anayeona fedha ndogo aache ubunge, kwani huo ni ufisadi
 
Watu wanapigania masilahi yao nyie mnawaona wabaya sasa sijui mlitaka wasipiganie masilahi yao.
 
Kweli wanalipwa kidogo sana:-

Mashahara - 12m
Posho - laki 3 kwa siku
Posho Kamati - Laki 5
Mkopo - Mil 600
Lobbying - 3m mpaka 10m
Kiinua Mgongo - 250m
Kifuta Jasho cha gari - 90m
Fedha ya Jimbo - 250m

Napendekeza waongezewe mshahara wawe wanalipwa 100m kwa mwezi na Posho kila kikao 2m.
 
Wabunge waanze kuchangiwa posho kutoka majimboni kwao, ili wapunguze kujikombakomba kwa serikali kuhusu malipo....matokeo yake wamegeuzwa kuwa rubber stamp ya serikali kwa kuendekeza njaa...
 
"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga

====

Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.

Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.

Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.

Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”

Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”

Chanzo: Mwananchi

HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
Sasa huyu mbona anakosa akili na maarifa basi alinganishe Tanzania na Afrika Kusini kiuchumi, kama mishahara haitoshi si aache ubunge? kama analinganisha mishahara basi hata walimu,waganga na waajiriwa wengine walinganishiwe mishahara yao na Afrika Kusini na si wabunge peke yao, hapo ndipo nitazidi kumkumbuka mwendazake kwa kuwapuuza waleta upuzi bungeni.
 
Kweli wanalipwa kidogo sana:-

Mashahara - 12m
Posho - laki 3 kwa siku
Posho Kamati - Laki 5
Mkopo - Mil 600
Lobbying - 3m mpaka 10m
Kiinua Mgongo - 250m
Kifuta Jasho cha gari - 90m
Fedha ya Jimbo - 250m

Napendekeza waongezewe mshahara wawe wanalipwa 100m kwa mwezi na Posho kila kikao 2m.
Sawa tu kwani kuna tatizo. Maana nchi ni yao wengine sisi ni wahamiaji tu.
 
Back
Top Bottom