Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

Dodoma: Nicodamus Maganga (Mbunge) adai Mishahara na Posho haiwatoshi Wabunge. Ashangiliwa...

Kuna yule mbunge wao aliyesema kuwa ubunge ni mtamu sana Yuko tayari kuuwa ili asikose ubunge
 
"Kuna manung'uniko maslahi ya Wabunge ni kidogo, wakati sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha, nimeangalia Mabunge mengine wanalipa kwa dola, tusiwaogope Wananchi kwenye Ubunge hakuna kitu tunatukanwa tu mitandaoni”—-Mbunge wa Mbogwe, Maganga

====

Dodoma. Mbunge wa Mbogwe (CCM), Nicodamus Maganga amewataka wabunge kuwaeleza wananchi ukweli kuwa mishahara na posho wanazolipwa hazitoshi.

Maganga aliyasema hayo jana Jumatatu Juni 21, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Nikiwa bado sijaingia humu nilikuwa nafikiria kuna posho za kutosha. Nimeangalia mabunge mengine Afrika ya Kusini pamoja na Kenya pamoja na mabunge mengine wanalipa kwa dola,” amesema huku akipigiwa makofi na wabunge wengine.

Amewataka wabunge kueleza ukweli wananchi kuhusu malipo yao, “tumekuwa tukitukanwa kwenye mitandao. Waziri na mimi hii kazi niliiomba kwa roho yangu moja na mimi nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko. Pesa inayolipwa posho, mishahara haitoshi,” amesema.

Huku akiitaka Serikali kuwaangalia ili wafanane na mabunge mengine amesema, “tusiwe wajanjawajanja, ninaujua utapeli wa kila aina lakini sitaki niwe tapeli wananchi wajue wana mbunge mwenye hela huku hakuna kitu kinachoendelea.”

Amesema Bunge la bajeti limebakiza siku tisa kumalizika na wananchi wanapoona wabunge wamerejea majimboni wasidhani kuwa wana fedha akisisitiza, “bungeni hakuna kitu.”

Chanzo: Mwananchi


HUYU ANATAKA AONGEZEWE MSHAHARA , UNAMSHAURI NINI ?
Atuambie baada ya miaka mitano zile milioni500 hazikatwi kodi ni hela kidogo hiyo? Atuambie lile gari atalopewa je? muambie je mshahara wa mbunge unakatwa kodi? atuambie toka awamu ya tano mishahara imeongezeka kwa kiasi gani? akae akijua asijilinganishe maisha na jirani yake kila nyumba ina style yake ya kula kutokana na walichojaliwa
Kulipwa dola sio ufahari hata hiyo mishahara yao inaweza kubadilishwa ikawa dola thamani iko pale pale.Bunge la Kenya huwezi kuleta mifano yake hapa Kenya iko juu kiuchumi kuliko Tanzania.
Huyu mbunge anaonekana ana njaa na ana tamaa hakwenda kwa nia ya kuwakilisha wananchi ni tumbo lake limemfikisha huko kipindi kijacho huyu asipewe kura.
 
Mbuge wa ajabu sana, Kama anataka fedha/hera jibu ni Kujitoa afanye biashara. Kazi yoyote ya Kuajiliwa haina fedha za Kutanulia. Hata hivyo kama anaona aliburge steps arudishe Jimbo watu ni wengi wa kuwatumikia watanzania. Mbuge wa ajabu sana, kumbe aliwaambia wananchi wake kuwa atarudi kwao na hera...bure kabisa sijui anatoka Chama gani???
Kwani kuna chama gani humo chief,si ni kikao cha CCM tupu humo? Hao wameshiba mpaka wanaanza kucheua sasa,hawajui walimu,wanaishi kwa mshahara mdogo kiasi gani huku wakipigika na kazi kubwa na mazingira mabaya
 
Au kama vipi Corona impitie na yeye.
Yaani inauma mno hadi nimekumbuka tweet ya Jamaa mmoja anamwambia Mama Samia "hivi hakuna namna ya kubana hewa mle bungeni ili wote waliomo humo wote wafe?

Kwa haraka unaweza kudhani anachuki ila kauli kama hizi za hawa wabunge ni matusi ya nguo kwa wananchi
 
Humo bungeni kasukumizwa, kama alivyosukumizwa mwendazake kwenye urais?
 
Mwendazake ametuachia kilio kikubwa sana,hawa wabunge wana laana
 
Hata ukiwa na pesa ndefu kiasi gani haikutoshi tu, labda uwe na matumizi madogo
Hela haiwezi kukutosha kama ni mpenzi wa anasa! Sie tuliozoea maisha ya kawaida nikipewa 11M+ its a fortune! Maana nakula nini cha kumaliza 11M nzima mie zaidi ya mafuta ya gari labda sidhani kama hata familia yangu inamaliza 500K kwa mwezi!
 
Katumia muda mwingi kuongea ujinga.Uko mbongwe kwenye kumepauka kama nini alafu yeye anatumia muda kujiwazia ujinga.bure kabisa.
 
Je hayo ndio aliyotumwa na wananchi wake??Au amekwenda kutetea masirahi yake badala ya kutanguliza masirahi ya watu wa jimbo lake.
Huyu mbunge akipita 2025 nitakunya kuanzia Msata mpaka Magogoni😂😂
 
Awa watu WAMEFANYA wananchi TUANZE KUOGOPA kabisaa

Wengine atukuwahi Kujua wanacholipw
kwakuwa wamelalamika tumeanza Kujua wanacholipwa kiukweli n hatarae Sanak
tunaomba mama YETU MPENDWA Apunguze HIZI POSHO pesa zingine zikajenge zahanati vijijini

 
Wanasihasa si hasa
Madam wetu ni zao la wanasiasa
Itoshe kusema mwache afanye maendeleo
Mambo mengine mnamjazia inzi tu
 
I
Awa watu WAMEFANYA wananchi TUANZE KUOGOPA kabisaa

Wengine atukuwahi Kujua wanacholipw
kwakuwa wamelalamika tumeanza Kujua wanacholipwa kiukweli n hatarae Sanak
tunaomba mama YETU MPENDWA Apunguze HIZI POSHO pesa zingine zikajenge zahanati vijijini
Inbox mkuu hiyo document
 
Back
Top Bottom