Dodoma: Rais Samia anazindua Mkakati wa Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi 2022

Nchi inahitaji pesa kwa ajili ya mambo mengi muhimu, sensa siyo ya muhimu sana kwa sasa.
Lakini pia inawezekana kutrack idadi ya watu kwa ufanisi bila kulazimika kufanya zoezi ghali la sensa kila baada ya muda fulani
Viongozi wa vitongoji, Clinic etc wanatosha kuripoti watu wapya
 
Fedha ya sensa iko ila inapotakiwa ya kujengea madarasa, vituo vya afya inabidi twende kwa wananchi tuwakamue kupitia t.ozo. Kama taifa sijui vipaumbele vyetu ni nini? Tulichoma mabillioni ya shilingi kuendesha mchakato wa Katiba mpya ukafia njiani.

Bora tungepiga kura kujua mitazamo ya watanzania kuhusu serikali hii inavyo jiendesha.
 
Sensa ni muhimu kwani inasaidia serikali kupanga maendeleo kutokana na idadi ya watu. Hata kama hakuna hela mikopo unaweza kupatikana ili zoezi kifanyike.
 
Hawa watu hata haya hawana. Wanasema kuna corona na wanapiga marufuku mikusanyiko huku wenyewe wakiendelea kukusanya watu bila ulazima wowote. Hivi angekaa kwenye tv na kutoa hotuba yake huku luninga na online media zote zikionyesha asingesikika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…