Dodoma: Rais Samia awatunuku Kamisheni Maofisa wa JWTZ

Dodoma: Rais Samia awatunuku Kamisheni Maofisa wa JWTZ

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Atawatunukia Kamisheni Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi Tanzania. Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma.

Matangazo yataanza saa nane kamili mchana leo tarehe 17 Aprili 2021.

====

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatunuku kamisheni maofisa wanafunzi 386 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kundi la kwanza la mwaka 2017 lilitunukiwa shahada ya sayansi ya kijeshi na kundi la pili namba 68 walitunukiwa kozi ya mwaka mmoja.

Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi Aprili 17,2021 Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Hii ni mara kwa kwanza kwa Samia kutunuku kamisheni tangu aapishwe kushika wadhifa huo Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kundi la kwanza lina askari 158 na wote ni Watanzania na kati yao wanaume ni 150 na wanawake wanane.

RAIS SAMIA KATIKA SHUGHULI ZA KUTUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ INAYIFANYIKA MUDA HUU CHAMWINO JIJINI DODOMA.


s1.jpg
s2.jpg
s3.jpg
s4.jpg
s6.jpg
s5.jpg
 
Leo rais wa JMT atawatunuku kamisheni maafisa wanafunzi wa JWTZ tukio ambalo litarushwa live na vyombo vya habari kupitia televisheni kuanzia muda wa saa nane mchana.View attachment 1754382
Raisi wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza vizuri, na atamaliza vizuri insha allah. Rest in Peace shujaa wetu hayati Magufuli. Dunia, Africa na Tanzania nzima tutakukumbuka daima
 
Akimaliza aje atueleze hawa wasaidizi aliowateua wanakazi gani kama mawaziri wapo,Masarani unaweka masaidizi wa maendeleo ya jamii,wakati kuna waziri wa kada hiyo,au msaidizi wa diplomasia,wakati una waziri wa mambo ya nje.

Kwa nchi kama USA,kuna mshaurj mmoja tu wa mambo ya usalama,na waziri wa ulinzi/defense secretary,hakuna mshauri wa mambo ya nje,wakati yupo foreign affairs secretary.
 
Back
Top Bottom