Dodoma: Rais Samia azindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza

Dodoma: Rais Samia azindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Msalato jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo tarehe 25 Machi 2022.

RAIS SAMIA: HATUWEZI KUAJIRI WATU WAPYA KILA MWAKA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake haina mpango wa kutoa ajira mpya katika Jeshi la Magereza kwa kigezo kuwa wengi waliopo wamepanda vyeo.

“Tulitoa ajira ya watu 700 ambao naambiwa niliwapandisha cheo kwa mapendekezo yenu, nina hakika kuna watu wanazurura tu kwenye korido za ofisi hawana kazi, warudi wakasimamie wafungwa.

“Hatuwezi kuajiri kila mwaka, tuna kiwango kikubwa cha mishahara tunayolipa, haina maana mtu ukipandishwa cheo basi ukae ofisini tu, kama una cheo au hauna rudi kwenye ‘field’ ukasimamie wafungwa, hicho cheo chako utabaki nacho,” - Rais Samia.

Uzinduzi undeleeeee....

Kama mtu unakasirika basi ng'ata pua yako au jisaidie Boga.

Alisikika mwana Lumumba akisifia.
 
2025 atachoka sidhani Kama atautaka rais.kazi nyingi
 
Kuna msoma risala anaupiga mwingi
🤓🤓😂😂🤠🤠
 
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Msalato jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo tarehe 25 Machi 2022.

Safi,wapi picha za miradi.
 
Haahahha naona anapambana na mkuu wa magereza. Ila mama Samia aisee[emoji1787]
Nimeanza kuamini huyu Mama ni figure Head tu na ameanza kuwa na kaujuaji fulani.

Mkuu wa Magereza ameungana Rasmi na Sirro kumshangaa Huyu mama soon na Mabeyo atatema Nyongo
 
Back
Top Bottom