Ukiangalia hutuba ya Mama sikuona akipongeza kwa yaliyofanyika , zaidi ameeleza mapungufu aliyoyaona/ kusikia na kuelekeza/kushauri cha kufanya.
Nikiangalia nje ya box kuna uwezekano mkubwa huyo mkuu wa Magereza akapangiwa kazi nyingine. Sina maana kuwa hajafanya vema, laah hasha, jamaa kafanya makubwa sana ambayo hayakuwepo awali.
Moja ya maoni yangu ni kwamba huyo Mkuu wa Magereza kiutendaji yupo vizuri sana sema ni mtu ambaye ni matata sana, very tough katika maamuzi na hapindishi jambo, kiujumla ana misimamo yake fulani hivi.
Sasa kwakuwa waziri wa mambo ya ndani kabadilika ni Mh Masauni hatujui ni mtu wa namna gani maana wengine hawataki mtu wa chini yake avume kuliko yeye. Waziri ana nafasi kubwa sana kwa Rais KIUSHAURI ktk taasisi zilizopo kwenye wizara yake