DODOMA: Rais Samia kuunda Kamati Maalumu kufuatilia mwendo wa Majeshi yote nchini

DODOMA: Rais Samia kuunda Kamati Maalumu kufuatilia mwendo wa Majeshi yote nchini

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuunda kamati ya watu 12 na sekretarieti ya watu watano kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini humo.

Rais Samia ametangaza kuunda kamati hiyo Jumatano Juali 20, 2022 mara baada ya kumuapisha Camillus Wambura kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nafasi ambayo ameteuliwa Ramadhan Kingai ambaye awali alikuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kigoma.

Rais Samia amesema kamati hiyo itakayooongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othumani Chande na makamu wake atakuwa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambayo itakuwa ikimshauri njia bora ya kuleta mabadiliko ya utendaji kazi wenye matokeo bora kwenye vyombo vya haki jinai.

“Kwa hiyo tutaanza na polisi, wakimaliza wakileta ripoti tutafanya marekebisho, tunakwenda majeshi mengine, tunakwenda magereza, hivyoo mpaka tumalize,” amesema Rais Samia

Amesema kwa ufupi serikali inakuja na jicho jingine ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama na kubainisha kamati hiyo itakuwa ikimpelekea mrejesho kila Jeshi linapomalizwa kuchunguzwa na kufanyiwa maboresho.


“Tutakuja na miundo inayofaa sasa hivi ili kuja na jeshi linalofaa na bora kutumikia Watanzania,” amesema Rais Samia

Mbali na IGP Wambura kuapishwa, wengine walioapishwa ni, aliyekuwa IGP Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Luteni Jenerali, Mathew Mkingule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Dk. Suleiman Haji Suleiman kuwa Balozi.
Nalia na Ramadhani Kingai kuwa DCI, alienda kujisaidia mara tatu kila akiulizwa na Jaji swali gumu la GPO.
 
Si kama kile kikosa kazi nacho ni ulaji tupu na wakati kuna maoni/rasmu ya Warioba yapo wazi
Tatizo mfano wa jeshi la police tz, ni katika kutumia SHERIA za mkoloni, sasa WENDA tokana na SHERIA hizi Kuna asilimia kubwa hata Katika mwongozo wao kwenye vyuo vyao imejikita huko, Sasa unatengenezaje, au weka Mambo sawa bila KATIBA MPYA, haiwezekani, ni lazima kukubali kwamba katiba ni sasa.

Mfano hona watu ambavyo hawaelewi uteuzi huu, na mimi nikiwemo, maana yake haki ndani ya taifa hakuna,
Na niseme hata sio wote ndani yao kwa wao wamependa,wanapenda ichi kimetokea, ila sasa ndo hivyo katiba imetoa ufalme kwa Rais wa nchi hii, sasa umafikaje huko bila Katiba.

Kwamba unaunda tume bila katiba Ayo ma SHERIA mengine unayarekebiasha vipi pitia Bunge, kwangu naona ni changa la macho, huwezi penda matunda wakati mti hutaki tengeneza, ila yapo yaliyo moyoni kati ya tz na Mungu ni makubwa Sana, nilisema, niliandika hum JF enzi za Mwendazake, wengi hawakuelewa, ila hatuna makanisa na sio wachungaji Mungu ananena makubwa na wateule wake, Mungu ibariki Tz.
 
Mimi ningependekeza iundwe Joint Service Unit(JSU) itakayohusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama jw,Polisi,Tiss,Magereza,Takukuru,Immigration,Jeshi la zima moto na uokoaji na Taasisi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kazi iwe kuratibu na kukusanya taarifa kwa siri kuhusiana na utendaji kazi na nidhamu ya vyombo vya ulinzi na usalama na haki ya Watanzania
Nawasilisha
 
Tatizo mfano wa jeshi la police tz, ni katika kutumia SHERIA za mkoloni, Sasa WENDA tokana na SHERIA hizi Kuna asilimia kubwa hata Katika mwongozo wao kwenye vyuo vyao imejikita huko, Sasa unatengenezaje ,au weka Mambo sawa bila KATIBA MPYA, haiwezekani, ni lazima kukubali kwamba katiba ni Sasa
Mfano hona watu ambavyo hawaelewi uteuzi huu,na mimi nikiwemo, maana yake haki ndani ya taifa hakuna,
Na niseme hata sio wote ndani yao KWa wao wamependa,wanapenda ichi kimetokea,ila Sasa ndo hivyo katiba imetoa ufalme KWa Rais wa nchi hii, Sasa umafikaje huko bila katiba

Kwamba unaunda tume bila katiba Ayo ma SHERIA mengine unayarekebiasha vipi pitia Bunge, kwangu naona ni changa la macho, huwezi penda matunda wakati mti hutaki tengeneza, ila yapo yaliyo moyoni Kati ya tz na Mungu ni makubwa Sana, nilisema,niliandika hum jf enzi za Mwendazake, wengi hawakuelewa, ila hatuna makanisa na sio wachungaji Mungu ananena makubwa na wateule wake, Mungu ibariki Tz
Ni mambo ya hovyo sn
 
kama amepata baraka za wakubwa atende... kama anafanya kwa utashi wake asithubutu
 
Majeshi yote ya invest kwenye High-Technology
Hili ni la msingi, lakini juhudi zielekezwe kumiliki technolojia zetu kwanza. Yaani mfano tuwe na "Ant Virus made in Tanzania", tuwe na robots na IoTs zinazo endeshwa na mifumo yetu tunayoimiliki.

Vinginevyo, naunga Mkono hoja yako.
 
Back
Top Bottom