Dodoma: Serikali yasitisha mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa kati unaopita kata ya Nkuhungu

Hiyo miradi ya mihemko bila kupitishwa na bunge ...

Mh samia piga chini tuu...

Hatuwezi kuendesha nchi kwa mihemko ya mtu mmoja ..

Mh raisi tunakuamini sana
natamani mngeijua Dodoma vizuri na mahitaji yake, ni mji wa kimaskini ambao mradi kama huu huwenda ungefungua fursa kwao. hakika nawaambia msingependa mradi huu usitishwe sisi tunaelewa msaada wake.
wauzaji wa vifaa vya ujenzi wengi watakuwa wamechanganyikiwa kwa kuwa ulikuwa unaenda kuongeza wateja sio kidogo na kufungua fursa mpya kiukweli ulikaa vizuri hata kwangu barabara ilikuwa haipiti mbali na moja site zangu unafikiri wenye hela wangenitoa kwa shilingi ngapi na mimi ningesubiri nini kubaki hapo. acha kabisa!
 
Sasa unataka miradi ya kupeleka maendeleo Chattle kwa upendeleo nayo iendelee? Au miradi ambayo ilianzishwa wakati hali ya kiuchumi hairuhusu iendelee? Watu mna wazimu.
 
pole punguza hasira wangu japo hata mimi huu mradi nimeumia nilivyouzungumzia jana kuna mtu akanitukana lakini hatimaye leo ameona kilichotokea.
kwa hili wagogo hawatawasamehe ccm.
 
JPM hakuwa na akili,mradi kama wa airport ya Chato ulikuwa hauna maana kwa sasa,alikurupuka tu,
Hivi kama una akili timamu unawezaje kuweka international airport kwenye wilaya kabla ya makao makuu ya mkoa,yaani ujenge airport Karagwe kabla ya Bukoba mjini,au Hai kabla ya Kikimanjaro,au mpwapwa kabla ya Dodoma mjini.
 
Vijamaa vya dsm huwa vinajiona nchi ni yenu...pakijengwa kwingine ni upotevu wa pesa eeee
#Triumvirate Dodoma ndio nyumbani kwangu,lakini hahiitaji ring road na hapo chako ni chako ndio ilikuwa sehemu yangu ya mambo yetu,japo kama imekufa vile, Hakuna ubize unaohitaji ring roads
 
Mi nadhani huu uzi kuna kitu hakiko sawa,hii barabara imepita sehemu mbalimbali za jiji la Dodoma na huko Nkuhungu ni sehemu tu ya hiyo barabara,pia ukisoma hiyo barua kule Nkuhungu kulikuwa na mjadala/mgogoro wa jinsi ya kulipa wamiliki wa viwanja inapopita, kwahiyo nina matumaini kuwa sehemu nyingine ujenzi utakuwa unaendelea kwani hizo Barabara kwa jiji la Dodoma ni muhimu sana,tofauti na mtoa mada ulivyoelezea kwenye uzi wako...
 
hivi nauliza ukiwekeza fedha zote kwenye afya zikiisha unazipata wapi? lakini hivi ni kweli tuna taifa la wagonjwa kiasi kwamba tukipatacho tuwaze kila siku kuwekeza kwenye hospital huku tukisahau jinsi ya kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji ili yalete kodi zitakazoiwezesha nchi kuendelea kuboresha huduma bora?
kweli!?!
 
#Triumvirate Dodoma ndio nyumbani kwangu,lakini hahiitaji ring road na hapo chako ni chako ndio ilikuwa sehemu yangu ya mambo yetu,japo kama imekufa vile, Hakuna ubize unaohitaji ring roads
Ni makao makuu projection za yajayo ilitaka kuwa na miundombinu hiyo..unataka 20 yrs baadae pawe congested kama dsm?
 
Sasa Dodoma unawekeza nini??
Mvua hakuna, madini hakuna,utalii hakuna, ardhi imejaa chumvi na magadi wewe Mgogo vipi. Dar kuna barandari , dar kuna shughuli za Uvuvi, utalii n.k.
mhn! haya ndugu Muulize Malkia Elizabeth Gold nzuri ya Tanzania iko wapi?
  1. zaidi ya 65% ya mji wa Dodoma una madini.
  2. mvua inatosha tuna wastani wa 500mm-800mm ambazo zinatutosha ikiwa serikali itatusaidia katika kutuelimisha na kuweka mfumo wa uvunaji maji tuna mvua nyingi kuliko Israel wanaoongoza kwa kilimo cha matunda
  3. chakula kinacholimwa Dodoma ni salama kwa kuwa hakitumii mbole za viwandani
  4. tuna zabibu tamu Dunia nzima ila haijafanyiwa soko la kutosha na inazaa mara mbili.
 
Kama mnataka isibomolewe itungieni sheria. Inaweza kuitwa "An Act to protect the Legacy of the anointed Supreme John Joseph Pombe Magufuli".
Tulishauri itungwe sheria, tena mimi nilitaka yafanyike mbadiliko ya katiba ili kulinda mali zote za kudumu za uma (serikali) zisiweze kuuzwa, nikajibiwa kuwa katiba si kipaumbele.

kuwa katiba ni kikaratasi tu nk. Lengo langu ilikuwa ni kulinda mali na hasa miradi mikubwa ambayo JPM aliyoanza kuijenga isije kutekwa na wachache baada ya yeye kuondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…