Dodoma: Serikali yasitisha mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa kati unaopita kata ya Nkuhungu

Njia zake zipi? Amekopa na kutuachia deni kubwa sana kwa mabeberu.
Magufuli tu ndiye alijua namna ya kukusanya pesa kwa njia zake .....!!

Huo ni mwanzo. Miradi mingi tu itasimamishwa kwa uhaba wa pesa ....... Siyo rahisi kufanya kazi Kimagufuligufuli!!
 
Hakukwa na haja ya kuhamia Dodoma, kuhamia Dodoma ilipaswa kuwa kipaumbele cha mwisho kwa Rais yeyote makini.
 
Dodoma haitakaa ijae kama Dar, serikali itaendelea kufanyia mambo yake mengi Dar es Salaam zaidi ya Dodoma, labda aje jiwe mwingine.
Hapa wamefanya makosa sana, Dodoma itakuja kujaa kama Dar ishindwe kupitika
 
JK ndiye aliyeacha alama kubwa zaidi ya Rais yeyote katika ujenzi wa miondombinu nchi hii
 
Mwacheni mama afanye kazi. Pegeni kelele mpate katiba mpya ...hapa washngton tunaraha tu hayupo aliye juu ya sheria
 
Ni vyema kwanza tukaambiwa kwanini ujenzi huo umesitishwa, kabla ya kupinga au kuunga mkono.

Sio haki na sio sahihi kabisa kuwaambia watu wasitishe ujenzi wa nyumba zao kwa sababu kuna ujenzi wa barabara halafu ghafla unakuja kuwaambia waendelee na ujenzi wa nyumba zao!!
 
Hakukwa na haja ya kuhamia Dodoma
Orodhesha sababu kwa mpangilio.

Kwamba serikali haikupaswa kuhamia Dodoma kwa sababu moja, mbili, tatu....

Ukiandika tu kama nyumbu aliyekatwa kichwa, tutaaminije hayo unayoyasema?

Hoja za kuitetea Dodoma zipo na zinakubalika:

Kwanza, Dodoma ni makao makuu ya nchi, kisheria na kiutaratibu.

Pili, Dodoma ipo katikati ya nchi, kwahiyo shughuli zote za kiofisi zitafanywa kwa ufanisi bila kuathiriwa na umbali.

Tatu, Dodoma ni sehemu salama kwa ajili ya makazi ya Rais kutokana na jografia yake.

Nne, serikali kuhamia Dodoma kumesaidia kupunguza ujazo wa watu Dar es salaam. Maofisi mengi na shughuli nyingi za kibiashara zimeanza kuwekezwa Dodoma.

Tano, kuhamia Dodoma kumesaidia kuupanua mji wa Dodoma na kuujenga kiuchumi.

Yaani wewe mtu mmoja wa mtandaoni usiyejulikana hata jina, unawezaje kusema hayo yote si kitu tena kwa kisentensi kimoja tu?

Unaitwa nani wewe?
 
Kwanza, Dodoma inaweza kuendelea kubaki kuwa makao makuu ya serikali, kisheria na kiutaratibu katika makaratasi ili kuwaridhisha wanaopenda kuganda katika mawazo ya Nyerere na kuona anaendelea kuheshimiwa.

Pili, Dodoma kuwa katikati ya nchi haifanyi shughuli zote za kiofisi kufanywa kwa ufanisi bila kuathiriwa na umbali.Nairobi, Kampala, Washington, London,Beijing n.k haziko katikati ya nchi zao.Ni ushamba kuamini mji mkuu unapaswa kuwa katikati ya nchi.

Tatu, Dar es Salaam na miji mingine pembeni ya bahari ni sehemu salama zaidi kwa ajili ya makazi ya Rais kutokana na jografia zake.Rejea jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 na jinsi Nyerere alivyoweza kiwatoroka waasi.

Nne, serikali kuhamia Dodoma hakujasaidia kupunguza ujazo wa watu Dar es salaam. Ukiacha Maofisi ya serikali tu shughuli nyingine nyingi za kibiashara bado ziko Dar es Salaam.

Tano, hatupaswi kupanua miji kama Dodoma na kuijenga kiuchumi kwa kuhamishia makao makuu ya nchi katika hiyo miji. Kama hivyo ndivyo tunavyofanya, tuhamishie makao makuu mji mwingine baada ya Dodoma ili kuukuza?
 
Umenijibu au umekanusha hoja zangu?

Umepiga chabo na kupesti kama yale magoigoi ya darasani.

Hebu tuambie, ni kwa nini serikali haipaswi kuhamia Dodoma?
 
Kwa sababu kuhamia Dodoma ni kupoteza pesa za walipa kodi wanyonge bila sababu za msingi. Hizo pesa za kuhamia Dodoma zingeweza kufanya mambo mengine muhimu.
Umenijibu au umekanusha hoja zangu?

Umepiga chabo na kupesti kama yale magoigoi ya darasani.

Hebu tuambie, ni kwa nini serikali haipaswi kuhamia Dodoma?
 
Kwahiyo mkuu wewe unasubiri mpaka kuwe na foleni ndiyo ujenge barabara nyingine!!??

Lakini ninachojua mimi barabara ya ring road ya Dodoma bado ipo na inaendelea kwenye process ya kujengwa hiyo inayotajwa hapo kwenye barua ni nusu ring road siyo inayojulikana hata pesa walishapata toka Benki ya Afrika kama sikosei.
 
(Acha maneno machafu)
 
(Acha maneno machafu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…