DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Nimejiuliza sana kuhusu ule mwaliko wa Lissu kwenda Marekani na kuwa atakuwa mtoa mada katika mkutano ule wa Wanasheria mahiri duniani.
Kulikuwa na tetesi kuwa zinaweza kutumika njama kama zile za kwenda Rwanda kuzuia asiondoke. Lakini Lissu amekwepa mtego huo kwa kukaa kimya.
Jee yawezekana lililotokea ilikuwa njia mbadala kuhakikisha haendi huko aliko alikwa? Just thinking aloud
Hauna uhusiano
 
Naam Mkuu Nape naye hakuwa na kosa lolote lile la kutishiwa bastola. Kama isingekuwa hadharani labda hadithi ingekuwa ya huzuni. Kisa cha kudhalilishwa na kutishiwa uhai wake ni kumkingia kifua yule jambazi na mfoji vyeti Bashite wa Kolomije.

Hakika mkuu,Jamaa ndio katufikisha hapa,ukiwa kinyume na mkuu wewe ni adui,nikikumbuka tukio la Nape,mbele ya macho ya waandishi na camera mtu wa usalama alithubutu kutishia kwa bastola,Mambo kama yale yanareflect negative energy ya watawala wetu inavyowatafuna watendaji ktk mamlaka zetu za usalama
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

View attachment 583477

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

3b0c289593c46e591d17070adda48d11.jpg


CCM imetoa pole

31c0c74743877f774b093e84c0906232.jpg


Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole

12d9f3126c463d0b2305ab6ada291270.jpg

MPENDA HAKI,TUNDU LISU. MPENDA NCHI YAKE, MUNGU AKUPE UZIMA BABA,
IMENIUMA SANA.
 
Barua ya Agasti 7
Anyway labda ni errors ingawa unaweza kuwa INA maana
 
chukua tokeo la bashite kuingia na watu wenye silaha clouds,,unganisha tokio la nape kutolewa silaha na muhusika hajulikani,,unganisha na kupigwa bomu kwa ofisi za mawakili pale upanga..baada ya hapo yachunguze majibu ya vyombo vyetu vya dola kuhusu matukio hayo..hapo kama unafikiri kwa kutumia kichwa basi utapata ni serikali ya aina gani inayotuongoza kwa sasa,( Pia fuatilia maelezo ya serikali kuhusu maiti zinazookotwa kwenye viroba)
 
hii hatar sasa.. walianza kwa kutishia hadharani na bunduki sasa wameanza kupiga kweliiii.... get well soon kamanda
 
Back
Top Bottom