DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Taarifa inayoeleweka ni kwamba Mungu anampigania,yupo na ataendelea kuwepo hadi pale Mungu atakapoamua mwisho wake..

Vipi, unataka habari nyingine?
Hata wewe Mungu atakapoamua ndio utakuwa mwisho wako, au hufahamu hivyo?
 
Hii inasikitisha sana ila bado kuna maswali yananisumbua kichwa mpaka sasa kwa mfano hivi huyu mpigaji risasi ni kwamba alikuwa anafyatua risasi hovyo maana naona nyingine amezipiga mpaka kwenye usawa wa mlango kwa chini ya kiti cha abiria au alikuwa anataka kumlenga unyayo? Risasi nyingi sana zinaonekana kama zilipigwa eneo la usawa wa mabega, kifua na shingo, je Lissu alikuwa anaendesha au alikuwa abiria? Kwa uwingi wa risasi zilizopigwa na zilizompata ambazo nimesikia ni zaidi ya tano ni kweli kwa nguvu ya silaha za risasi hizo damu haikuweza kuruka au kusambaratika mpaka kufika kwenye kioo? Na je, baada ya ajali hiyo Mh Lissu alitoka nje ya gari kupitia mlango upi wa dereva au wa abiria? Hii ni kwasababu naona mlango wa abiria hauna kabisa hata tone la damu lililodondokea au michirizi ya damu kutiririka? Hakuna mdau yeyote ambaye alifanikiwa kuzipata picha za ndani ya gari ilivyokuwa tuone kilichotokea? Inanisumbua sana akili yangu hii kabla hatujaanza kutupia shutuma kwa ndugu zetu wa mlango wa kati..
 
Baada Ya Sakata La Lissu Kupigwa
Risasi Na Watu Wasiojulikana Mapema Leo Hii Watanzania Wengi
Mno Ikiwemo Na Mimi Tumekuwa
Karibu Mno Kujua Nje Ndani Ya Mkasa Mzima Huu Ambapo Kila
Ukipita Ni Lissu, Mitandaoni Ndo
Hakufai, Simu Zinapigwa Kama
Kumetokea Vita Ya Tatu Si Vijijini
Wala Mjini. Kwa Kweli Nimevutiwa
Na Spirit Hii Ya Watanzania.

Habari Ya Lissu Imefika Pahala
Mpaka Ile Ripoti Ya Madini Imesahaulika Kabisa.

Habari Ya Lissu Imeibua Mjadala
Mzito Sana Kuhusu Hali Ya Usalama Nchini.

Habari Ya Lissu Imepunguza Imani
Kubwa Kwa Serikali Iliyopo.

Habari Ya Lissu Imempa Umaarufu
Mara Dufu .

Habari ya Lissu Imethibitisha Lissu
Ni Mkweli Kwa Kauli Zake.

Habari ya Lissu Imetangazwa Na Mastaa Kuliko Kawaida.

Na Huu Ni Ukweli Kwamba Haijawahi Kutokea
Isipokuwa Kwa Lissu.

Hawa Ni Baadhi Ya Mastaa Walio Guswa Na Issue Ya Lissu 583769[/ATTACH]


Hadi Kimataifa.

 

Attachments

  • Screenshot_2017-09-07-23-47-41.png
    116.4 KB · Views: 68
  • Screenshot_2017-09-07-23-44-01.png
    60.2 KB · Views: 67
get well soon Mp Tundu Lissu

*Akifa shekhe kazi ya Mungu*
*Akifa mlevi sababu ya Pombe*
 
Nilikua airport ya dodoma usiku huu ndio Tundu Lissu kabebwa na ndege binafsi. Ndege ilitua majira ya saa 23:12 usiku na imepaa sasa hivi saa 00:21 usiku.

Zile picha zilizokua zimesambaa mchana za helikopta nyekundu sijui nani alipotosha. Na hii ndege imenyanyuka uelekeo ni Dar es salaam.

Magari na watu ni wengi waliokua wamekuja kumsindikiza airport, kwa mliopo dodoma mtaona magari mengi ya wabunge ndio yanatoka airport.

Source; mimi mwenyewe nilikua airport.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kokote atakakopelekwa saw a,naomba UZIMA juu take. Nimeumia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…