DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

SAFI, APELEKWE KWA WASHUA, KUOKOA MAISHA YAKE.

KWA AINA HII YA KUVIZIANA KUTAKA KUUANA BILA SABABU ZINAZOELEWEKA ITATUCHUKUA MIAKA 500 KUFIKIA MAENDELEO YA MAJIRANI ZETU WA KENYA
Siungi mkono lissu kupigwa lisasi Ila hii ya kusema Kenya Wana demokrasia sana napinga, uchaguzi wa Kenya kufutwa maana yake ulikuwa na kasoro kwamba demokrasia ya uchaguzi haikufuatwa, pili mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Kenya aliuawa hata uchunguzi wa kudanganyia watu haukufanyika toka kwa huyo mnayemuita Baba wa demokrasia.
Karibuni tupambane na hali zetu.
 
Shusha bunduki chini tubishane kwa hoja.
Sisi sote tunajenga Tanzania moja.
[HASHTAG]#Roma[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Zimbambwe[/HASHTAG]
 
Tundu Lissu amepelekwa Nairobi huku akitoka chumba cha upasuaji mjini Dodoma akiwa ana fahamu!
 
Ee Mungu uwe pamoja na lisu
Sijawahi kutoa machozi lakini taarifa ya mtu huyu imenitoa machozi
Nikuhakikishie tu ndugu machozi yako hayatopotea bure, mie binafsi naona huu ni mwanzo wa mapambano dhidi ya wadhalimu na mafia wakubwa wa taifa hili ambao wamejivika kilemba cha 'watawala'.
 
Hivi hiyo sheria au mikataba mibovu siku mnasaini mlikuwa pande zote mko meza moja, leo unataka kuvunja uko mwenyewe kisa tu wewe ni serikali na hatimaye hata ukishindwa kesi hulipi wewe

Kuna tatizo lolote kwa mikataba mibovu mkikaa meza moja pande zote zinazohusika kueleweshana katika hilo ili kubadilisha mikataba?
 
Hats Nyerere hakuua wazungu ili hoja zake zikubalike. Huyu mwenzetu vipi kulazimisha hoja zake kwa risasi?
Bombadia wee nakupenda sana nipo tayari kuua kwa ajili yako
 

Kama public figure aina ya lissu,anashambuliwa kwa risasi hadharani,vipi kuhusu sisi? Hii dhima inamuangukia Amiri jeshi mkuu kwa kutengeneza mazingira ya uadui.
 
Naogopa hata kusema maana nikitoa ya moyoni nitatafutwa kesho !! Mungu amponye Kiongozi wetu, My President Lisu. Bado muda wa kuondoka haujafika, najua kazi uliyoitiwa na mungu bado aijakamilika...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…