DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

View attachment 583477

Kama kweli Mungu yupo, ni hai, halali, ni hakimu, ni msikivu, na mwenye uwezo uliopitiliza tutamuona sote kwenye suala hili. Tulieni ninyi wote wenye kuamini juu ya Mungu mmoja Mkuu, mwenye haki atapewa haki yake na mwenye kudhulumu atapewa malipo yake, nyie hamjui lakini Mungu ndiyo kazi yake.
 
Katika hali ya kumtakia Uzima mpambanaji Tundu Lissu kutokana na shambulio la risasi lililompata Leo huko Dodoma.


Get well soon Mh Lissu
 
Mungu muweza wa yote, mponye ndugu yetu Lissu. Amen.
 
Mungu,Wewe ni kila kitu ktk uhai wa Lisu.onekana mfalme,tetea roho yake,asife huyu mtu.Ulimjua tangu kuumbwa kwa dunia,na vivyo uliijua ccm.Mungu mponye,ili ccm iabike.hata yule aliyeomba aruhusiwe kumuua Lisu,ajue Mungu hufananishwi na raisi,wala yeyote.ruhusa ya kufa kwa mtu inatoka kwako tu.sina neno zuri la kukupendeza Mungu wanagu,nakuita tu umponye Lisu,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu yupo nae

bunge la tanzania ni "rubber stamp" ya serikali ya magufuli
 
Back
Top Bottom