DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Hali tete sana aiseee vijiwe vimepooza watu wana uzuni

Kumbe ndio maana Tanzania ndio nchi ambayo watu wake hawana furaha"
 
Mie pia nimejaribu kucheki sehem sehem wengi wanamaindi na hii ni ishara watu wamechoka na kiki za mkuluu hata walio kuwa jana attention kumsikiliza walikua wachache sana wengi weshaona ni ubabaishaji sasa uki+ na hili duh
 
Wananch tunasubiri tupate taharifa kuwa kapoteza dunia. Aliyewatuma tunamjua yani hatafika hata chalinze

[emoji124]‍♂️naenda zimbobo.
f31eb55209ab1919bafc84a28b0329bc.jpg
 
Mkuu kwakua amekua akifuatiliwa toka siku za nyuma bila madhara yoyote,nafikiri ata pale dereva wake alipomuambia kua anahisi kuna gari inawafuatilia haikumtia wasiwasi sana aliamini huenda ni walewale jamaa wanaomfuatilia hivyo hawakua na sababu ya kuanza kukimbia hovyo.

Sijui gari ile iliyofanya tukio ilisimama umbali gani na gari ya TL lakini wasiwasi uliwapata baada yakufika na ndio pale dereva akamueleza kua asishuke kwanza kuangalia upepo wa gari ile inayowafuatilia ina malengo gani.

Kwakua yeye ni mtu wakukamatwa kila siku huenda pia alijua ni askari tu waliotumwa tu hivyo hakushuka ili kuwasubiri labda wametumwa kuja kumkamata.
Hiyo kutoshuka ndiyo iliyo muokoa na hiyo yote ni kuonyesha kuwa mungu siyo Athuman
 
Mkuu huwezi kuongoza nchi kwa chuki za kutisha na visasi, kudharau katiba, Bunge na sheria za nchi kufanya uharamia dhidi ya Maalim Seif na CUF na kuwa kauli za kufoka foka kila mara na undumilakuwili kwenye maamuzi kwa mfano kuwafukuza waliofoji vyeti lakini Bashite mkolomije kumkingia kifua etc.

Huyu mtu nchi imeshamshinda na Watanzania wengi wameshahitimisha hafai kabisa kuongoza nchi.

Mie pia nimejaribu kucheki sehem sehem wengi wanamaindi na hii ni ishara watu wamechoka na kiki za mkuluu hata walio kuwa jana attention kumsikiliza walikua wachache sana wengi weshaona ni ubabaishaji sasa uki+ na hili duh
 
Kama kuna mtu aliyekuwa ANAPIMA MAJI KWA MTI , basi ni vema akajua kwamba haya ni MAJI YA SHINGO .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
UPDATES:

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

CCM imetoa pole

Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole

UPDATES: 2235HRS
Ndege iliyokuja kumchukua Tundu Lissu ndo inatua Uwanja wa Dodoma. Ni ndege binafsi, imetoka Dar Es Salaam na itampeleka Mh. Lissu Nairobi Kenya kwa matibabu zaidi.

TunduLissu akipakiwa kwenye ndege usiku huu tayari kwa safari ya Nairobi kwa matibabu zaid

*Rais wa Chama cha Mawakili Kenya(LSK), Isaac Okero amesema Lissu amelazwa Hospitali ya Aga Khan, Nairobi.

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

doctor lisu.jpg
lowasa.jpg


Kwa Updates nyingi zaidi Download App ya Chadema News ilikuweza kuwa wa kwanza kujua kila kinacho endelea kuhusu Tundu lisu au Click apa kuweza kui download Chadema News – Програми Android у Google Play
 

Attachments

  • lisu6.jpg
    lisu6.jpg
    6.4 KB · Views: 34
Back
Top Bottom