DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Mara nyingi huwa tunaangalia matokeo ya vitu ba kuacha kuangalia mizizi.

Kabla ya kufika kwa aliyepiga risasi, rais wa Tanzania kwa kauli zake mbovu za kuhalalisha wapinzani waandamwe, amechangia kuwepo kwa hali hii.

Kabla ya rais kuwa rais, chama tawala kilichomuwezesha huyu rais kuwa rais, kimetuangusha.

Wazee wa Chama tawala waliompendekeza huyu rais kuwa rais wametuangusha.

Wapiga kura waliotupa huyu bungeni wametuangusha.

Marais waliomteua ubunge wametuangusha.

Bunge lenyewe ambalo amekaa bungeni miaka yote bila kujifunza mengi, limetuangusha.

Vyuo vya elimu ya juu na shule za elimu ya awali vimetuangusha.

Kanisa lililomlea limetuangusha.

Familia iliyomlea imetuangusha.

Jamii nzima ya Tanzania iliyoshiriki kutufikisha hapa imetuangusha.
Akili yako mbovu imekuangusha
 
IMG_20170913_110059.jpg


Je wajua Tundu lissu aliwatoa gerezani bure wananchi 466 wa tarime waliofungwa kwa kupinga mwekezaji asiwanyangnye ardhi yao.

Je wajua Tundu lissu aliwaikuwa mwalimu wa shule ya secondari bondeni aliyopo mkoani Arusha.

Je wajua Tundu lissu alipambana na kaka take alute lissu mahakamani kwenye kesi ya kupinga ubunge wa Lema, Alute lissu akitetea CCM na Tundu lissu CHADEMA.

Je wajua Tundu lissu hutumia chupa tatu za maji ya Kilimanjaro kama MTO akina rumande, ndio maana akitoka rumande huonekana ameshika chupa.

Mr mkiki.
 
Niliposikia umepigwa risasi , sikuamini nilihisi niko ndotoni.

Tangu tukio limetokea nimekuwa naota ndoto za ajabu ajabu tu, sijui ni kwa nini?

Wewe ni mtu mwema , tena unapenda haki , umetoa maisha yako kuwatetea watu.

Mungu amekujalia kipaji ambacho watu wengi hawana.

Tabasamu lako huonesha ukarimu na upendo kwa wanyonge.

Sasa hivi uko kitandani ukiwa na maumivu , usijali kaka LISU huku nyumbani maelfu ya watu wanakuombea. Hakika naamini hutakufa bali utaishi.

Pole LISU ,watanzania wanakupenda , Afrika inakupenda na dunia nzima inakupenda. Mungu akurudishie afya yako urudi nyumbani uwatumikie watu wako.
 
Back
Top Bottom