Hivi chadema wangekua wamechukua majimbo yote kasoro mawili kwenye uchaguzi, halafu CUF na CCM wakapata kitu kimoja kimoja mngesema CCM waachiwe baadhi ya majimbo ili kuweka balance bungeni?
Chadema tafuteni mlipokosea mtengeneze..... manenomaneno, matusi, uasi, ukimbizi hautamsaidia mtanzania yoyote zaidi ya hao viongozi wenu wabinafsi na wanaojifikiria wenyewe.
Chama mlikinajisi wenyewe kwa kumwita mliyemtuhumu fisadi kugombea urais, tena mbaya zaidi mlimkaribisha baada ya chama chake kumwambia hawawezi kumpa nafasi ya kuongoza dola sababu sio muadilifu.
Nyie sababu ya tamaa zenu za pesa mkamsafisha bila haya ili mshirikiane nae kufisadi nchi.
Hamkujifunza kwa Lowasa 2015........
Na ilipofika 2020 mkakinajisi tena chama kwa kumuweka mgombea mtetezi wa mataifa ya nje asiyejali maslahi ya wananchi. Eti mgombea wenu akaanza kampeni awe mbwembwe huku akiwatukana watanzania wasomi na wasio wasomi hadi maJaji kuwa hawajui kiingereza, eti mkawadharau police na kuwaambia wamechoka na wana hali mbaya, mgombea wenu akawa mjuaji wa kila kitu akamdharau hadi baba wa taifa Nyerere. Kwa kampeni zake hakuna kilichofanyika Tanzania tangu wazungu waondoke.... analazimisha eti hata kwenye reli hakuna kilichofanyika ila reli imejengwa na mjerumani
Juu ya yote akawaahidi waliomtuma hadi kwenye ilani ya chama chenu kwamba akiingia ikulu ataweka madini kama dhamana kwao ili wampe pesa.
Kampeni mwanzo mwisho mgombea wenu alikua akituringishia nguvu ya wazungu, akijidai wakili wake anafuatilia kitu. Watanzania walijiuliza hivi tukimpa kura atatuongoza yeye au atatuongoza kwa amri ya hao mabwana aliowaahidi kuweka mali zetu rehani kwao?
Hivi kweli hadi Karne hii bado kuna wasomi wa Tanzania tunatumia elimu tuliyo nayo kuweka rehani nchi yetu kwa wazungu badala ya kutumia ujuzi na elimu yetu kuvuna rasilimali zetu kwa faida? Tundu amelifedhehesha sana taifa
Hivi mlifikiri watanzania ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama huyo kuwa rais wa nchi?
Wafuasi wa Tundu ambao ni wachache sana wana mienendo kama ya Tundu.
Tuliwashauri mapema mkawe mawakala ili mkasimamie haki mnayoiimba hapa jf hamkuskia, tena badala yake chama chenj kikatafuta ambao hadi leo hakijawalipa posho zao.
Matokeo yake kila siku mnarudi hapa kulalamika kwamba mmeibiwa kura, hivi hamjisikii aibu kila uchaguzi mnalalamikia tatizo lilelile kama sababu ya kushindwa? Hamuoni kama nyie ni chama kisichoweza kutatua matatizo ya chama wala ya wananchi?
Haya sasa wananchi wamewakataa kwenye kura, wamewakataa kwenye maandamano, wamewakataa kwenye kuigomea serikali....... na hii inaonyesha chama chenu sio cha wananchi bali ni cha viongozi ndio maana mmebaki wenyewe mkihangaika.
Ingekua wananchi wanawapenda kungekua na maandamano yasiyozuilika kama maji ya jangwani kipindi cha mafuriko ila wananchi wana raha na amani tele, hata wale mliowaandaa kwa malipo sasa wanajuta na hawawezi rudia
Kwa tamaa zenu 2015 mliua kile chama tulichokipenda, Ile chadema ya wananchi, chadema iliyokua tumaini la wanyonge, chadema ya Mzee Ndesamburo na Dr Sla na wale viongozi wengine makini. Laana itawaandama kama hamtawaambia wananchi mliwakosea ili muanze upya
Maisha sio rahisi kwa mtanzania yoyote hata kwa Rais, huu ni muda wa kujenga uchumi wetu tuliouharibu na huduma za kijamii kwa maslahi yetu wote. Acheni kulalamika sasa
Mods msidelete