Dodoma: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Dodoma: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Attachments

  • giphy (1).gif
    giphy (1).gif
    2.3 MB · Views: 4
hapa najiuliza je waliuliwa au ni mmoja kati yao alifanya yake kisha akajitoa uhai
Faza hausi anasema mlango ulikua umefungwa anavunja ubao wa juu ndio akaingia.

Inamaana walimalizana ndani.
 
Kwanini mshukiwa wakwanza asiwe mwenye nyumba?
Huyu naye kuna mahali anajichanganya. Kwa nini akimbilie peke yake eneo la tukio! Alishindwa kabisa kuita na majirani!!

Yaani mpaka anavunja ubao wa mlango (vent), akaingiza mkono na kufungu kitasa (hapa hata sijaelewa kabisa eti) na kuingia ndani, alikosa kabisa mtu wa kusaidiana naye!!

Hivi isije ikawa alikuwa anamkula mpangaji wake! Na baada ya mpangaji siku hiyo kuingiza njemba nyingine, akaingiwa na wivu uliopitiliza! Na kuamua kuwamaliza eti!!

Polisi wafanye uchunguzi wao wa kina kubaini chanzo hasa cha mauaji.
 
Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki dunia huku mwanamke akiwa amechinjwa na mmwanaume ambaye hajafahamika jina akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 katika Mtaa wa Oysterbay, Kata ya Dodoma Makulu kwenye chumba ambacho mwanamke aliyeuawa Samira Mathias alikuwa amepanga.

Akizungumza na Mwananchi katika eneo la tukio mwenye nyumba hiyo, Donald Nhembelo amesema alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye chumba cha mpangaji wake (Samira) saa 7.00 usiku.

Amesema baada ya kufika kwenye chumba hicho alisikia sauti ya mwanaume akiomba msaada ndipo alipouliza Samira yuko wapi na kujibiwa kuwa hawezi kuongea na yeye hawezi kusimama.

“Aliniomba nivunje mlango ili nimsaidie. Nilivunja ubao uliopo juu ya mlango (Venti) na kuingiza mkono kwa ndani na kufungua mlango na nilipowasha taa ndipo nilikuta Samira yuko juu ya kitanda amenyamaza,”amesema.

Amesema damu zilikuwa zimetapakaa kitandani na sakafuni huku mwanaume aliomba msaada ambaye hamfahamu akiwa amelala chini huku utumbo wake ukiwa nje.

Amesema baada ya kuona hali hiyo, aliripoti polisi ambao walifika kwenye eneo hilo ambao baadaye waliondoka na miili ya watu hao.

Balozi wa mtaa wa Oysterbay, Isaya Mabigiri amesema amepata taarifa za uwepo wa tukio kutoka kwa mwenye nyumba hiyo na alipokwenda alikuta miili ya watu.

MWANANCHI
mlango umefungwa kwa ndani? Hapo alieomba msaada ndo mtekelezaji wa mauaji na kisha kujiua mwenyewe
 
Hii habari ina ukakasi, kichwa cha habari na story vinamvurugano maana sijaona sehemu inayoelezea mwanaume kufariki.
 
Back
Top Bottom