Pre GE2025 Dodoma: Wapiga Kura wakiwa na Vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM Wakati wa Kujiandikisha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu limeanza leo Oktoba 11, 2024 nchini nzima na litaendelea hadi Oktoba 20, 2024.

Rais Samia na yeye ametimiza haki yake ya Kikatiba, hapa akiwa kwenye foleni na wakazi wa Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma katika zoezi la kujiandikisha lakini baadhi ya Wapiga kura wameenda kujiandikisha wakiwa wameshikishwa vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM.

Tujiulize. Je, ni sawa Wananchi kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wakiwa wameshikishwa vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM?

Soma, Pia:
+
Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024
+ Tofauti ya Daftari la Kudumu la Wapigakura na Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa
 
Hakuna foleni hapo hao wote ni watu wa Ikulu
 
Ndio, nyie endeleeni kuandamana tu, mkimaliza uchaguzi huu hapa, mnaanza kulia matokeo
 
Huo uchaguzi unahusu wakazi wa mtaa au kijiji

Hata mgeni raia wa nje ruksa kupiga kura mradi mkazi wa huo mtaa au kijiji
Anayechaguliwa ni kiongozi wa mtaa
Hatuandiki mitaa tunayoishi, ni jina tu na umri tu.
 
Usipoteshe, tuliokwenda tumeandikwa majina na umri tu.
 
Viko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…