KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
Yakhe karibu Sheia yetu tumchague mwakilishi pasipo tatizo.Huo uchaguzi unahusu wakazi wa mtaa au kijiji
Hata mgeni raia wa nje ruksa kupiga kura mradi mkazi wa huo mtaa au kijiji
Anayechaguliwa ni kiongozi wa mtaa
Tunajuaje kama ni WA hapo? Je kama umewatengeneza?
Uchaguzi gani? Bongo hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Kama huamini nenda kaangalie. Idadi ndogo ya watu waliojotokeza kujiandikisha. Watu wameshastukia huo upuuzi uitwao uchaguzi.Ndio, nyie endeleeni kuandamana tu, mkimaliza uchaguzi huu hapa, mnaanza kulia matokeo
Maigizo mengine bana, kwamba rais wa Tanzania anaweza kusimama kwenye mstari asubiri zamu yake ifike?!
Hao Hao ndio watachaguaUchaguzi gani? Bongo hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Kama huamini nenda kaangalie. Idadi ndogo ya watu waliojotokeza kujiandikisha. Watu wameshastukia huo upuuzi uitwao uchaguzi.
Ni sawa, na hizo kura chache ndio huwa za ccm, lakini huiba za wapinzan!Hao Hao ndio watachagua
hata wangekua na vipeperushi vya mwenyekiti wa CUF au chadema, haina shida wala athari zozote kwenye zoezi hilo, kwasbabu hapakua na kampeni na wala huyo anaeonekana kwenye hivyo vipeperushi si mgombea wa nafasi yoyote kwenye serikali za mitaaZoezi la kujiandikisha katika Daftari la Mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu limeanza leo Oktoba 11, 2024 nchini nzima na litaendelea hadi Oktoba 20, 2024.
Rais Samia na yeye ametimiza haki yake ya Kikatiba, hapa akiwa kwenye foleni na wakazi wa Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma katika zoezi la kujiandikisha lakini baadhi ya Wapiga kura wameenda kujiandikisha wakiwa wameshikishwa vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM.
Tujiulize. Je, ni sawa Wananchi kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wakiwa wameshikishwa vipeperushi vya mwenyekiti wa CCM?
Soma, Pia:
+ Rais Samia Kuzindua Rasmi Zoezi la Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa Oktoba 11, 2024
+ Tofauti ya Daftari la Kudumu la Wapigakura na Daftari la Wapigakura wa Serikali za Mitaa