Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Habari iliyopo kwa sasa ni kwamba nyumba ya mbunge mheshimiwa Polepole mkoani Dodoma imevamiwa na watu wasiojulikana wameharibu mali za thamani na kuacha ujumbe mzito wa kuwa aache kuichafua serikali ya sasa

FB_IMG_1639334173985.jpg

=====

WATU WASIOJULIKANA WAVAMIA NYUMBANI KWA MBUNGE HUMPHREY POLEPOLE,

Watu wasiojulikana wamevamia nyumbani kwa mbunge Humphrey Polepole (Dodoma) wakati akiwa safarini, na hii ndio hali ya nyumbani kwake palivyo kwa sasa kama video inavyoonesha

Mbunge Polepole amethibitisha kuwa nyumbani kwake jijini Dodoma, pamevunjwa na watu wasiojulikana na kuibiwa Television pamoja na kuharibiwa vitu mbalimbali siku ya Desemba 12, 2021 akiwa safarini Manyara ambapo amerejea usiku huu na kukuta hali hiyo

"Hali nilivyoikuta nyumbani kwangu Dodoma muda huu, Nakwenda kuripoti Polisi. Yeyote aliyefanya haya Mungu atanilipia" amesema Humphrey Polepole.



PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
WASIOJULIKANA BADO WAPO TU? Si mlisema walikuwa watu wa Magufuli. This is government intimidation ambayo serikali yenyewe inapaswa kukalipia.

Mjibuni Polepole kwa hoja na sio vitisho kwani hayo matendo yenu yanaweza kuja kuwarudia na nyinyi pia kama yanavyomrudia Polepole!!! You should learn by now that there is nothing that is permanent!
 
Karma is a bitch .

Wakati kina Nape wanashikiwa bastola alikuwa anachekea, kina Lissu wanapigwa risasi anaona poa.

Ni funzo kubwa, alisema kwa kejeli Lissu anakaa na bwana zake kakimbia nchi, Mbowe alivunjwa mguu akasema alikuwa amelewa faru John akaanguka. Hata kama ni serious kweli sisi tunasema umelewa Double Kick ukavuruga sebule ili useme umevamiwa.
 
Back
Top Bottom