Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

Si wakati wa kuwashindanisha Nape na slow slow! Tushukuru kujua kuwa serikali bado ni kijambazi kwa jina la wasiojulikana!
 
Kumbe nani kawatuma? Tena tunataka atume kuwafanyinzia makatili wote waliokuwa pamoja na Magufuli ili waione karma.
Kwa hiyo Samia nae ni dhalimu kama Magufuli na hivyo kawatuma kumfanyia hivyo polepole
 
Kumbe nani kawatuma? Tena tunataka atume kuwafanyinzia makatili wote waliokuwa pamoja na Magufuli ili waione karma.
Kwahiyo nae ni dhalimu?

Vipi kwanza gaidi anatoka lini?
 
Acha porojo za kutetea uhuni wa serikali ya Magufuli dhidi ya Lissu, twambie nani mwenye mamlaka aliyeamrisha cctv camera kuondolewa kama siyo serikali.
 
Ndiyo akome
 
Abdu Nondo alijiteka, Pole pole amejiibia.
CCM hoyeeeee!!! Chama ni kikubwa kuliko polepole, aache ujinga hilo ni onyo la kwanza akiendelea yatakayomkuta asiseme hatukumwambia.
Mwenzie Gwaji boy alipigwa mkwaea na Ndugai akatulia tuli anatii mamlaka.
Pole pole nenda kasome kasome kitabu cha "kesi ya Sokreti ".
Utajifunza kutii mamlaka.
 
Dodoma kunani tena palee!?
Alianza Tundu Lissu kumiminiwa risasi, ikaja suala la Mbowe kuvunjika mguu!
Ikatokea minong'ono vifo vya Mahiga na Mfugale.
Sasa ni Polepole kuibiwa na kuharibiwa mali zake.

Sasa kituo kinachofuata ni...,
 
CCM wako pazuri kuelekea hatima yao.
Hili tukio katengeneza
Hakuna mwenye ujasiri kwa hili
Kuna mtu anatafutiwa kesi
Nape asijiamini saaaana
Kwa ufupi wote wahuni seeking attention
Kwanza hii ni nyumba au guest room au ofisi
Huu mchezo wa kipumbavu kabisa

Watu wasitoke kwenye mstari
Katiba Mpya uwe wimbo
 
Hapo nyumbani anaishi peke yake? Hana mke, hana watoto huyu jamaa?
 
Pole pole katubu kwanza ,alafu nitafute nikupe Upako wa gusa unate for free,ACHA kulia Lia ,hata mlipo mvunja mguu mh Mbowe mlikua mnacheka ,

Sasa timiza Ayo kwanza nimekwambia
 
KAVUNJA MWENYEWE KUTAFUTA HURUMA. AISAIDIE POLISI HUYO POLEPOLE.
 
Kafanya mwenyewe huyo actor....Hiyo ni fake hakuna ukweli hapo. Polisi mkamateni kwa uhuni anaoufanya, Kwanini hajaripoti polisi kama hatua ya kwanza? Analeta kwenye media ili apewe huruma, tapeli huyo
 


Watanzania wanapenda drama. Polepole ana umuhimu gani hivyo😂😂😂 anatengeneza mambo
 
Sasa utashirikiana vipi na unaowahisi ndio wamimina risasi? Au kichwa chako kibovu Nini? Kwahiyo Lissu na Dereva wake wangelikufa uchunguzi usingelifanywa? CCTV Camera Zina ushahidi wote na ziliondolewa ili wafanye yao.
 
ha! Kumbe ni zamu kwa zamu.
Kuna mengi ya kujifunza katika tukio hili
Ningefurahi sana kama M Mungu angewapa CCM fikra za kujifunza. Ila ninawasiwasi kama wanaweza kuzipata leo, kesho au keshokutwa. Hapa ndio tatizo lilipo.

Nilimsikiliza Rais Mwinyi (Z-zibar) akieleza tusahau yaliyotokea kwenye uchaguzi Z-zibar 2020, anawasihi wa Z-bari wasonge mbele bila kukumbushia hayo yaliyotokea. Sikumuelewa kwa kweli! Hivi hawakujifunza yaliyotokea 2000, 2005, 2010, 2015..... Na hakuna kipindi wahusika wamefikishwa mahakamani.... Hii ndio CCM, kila siku ni darasa la kwanza mnaanza kujifunza ALFABETI
 
Habari zenu wakuu. Baada ya kufuatilia maelezo ya polisi kwa kina, nimeamini kuwa hili tukio la ndugu yetu "taratibu" lilipangwa eidha na mwenyewe au na watu waliopo karibu yake ili kujaribu kujibust kidogo baada ya kuona kila analoongea huko mitandaoni watu hawana muda nalo. Nimeshangaa kusikia mtu alieibiwa TV Screen 1, na Sub-woofer 1, eti hajui thamani yake. Yani mtu uende dukani kununua viatu siku moja uvifue na kuvianika afu wezi wavipitie, baadae utoe taarifa kwa watu afu wakuulize thamani ya viatu ulivyoibiwa afu ww useme haujui? Ama kweli njia ya muongo ni fupi sana. Ngoja hili lipite tuone atakuja na lipi tena lingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…