Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

Mood humu kuna nyuzi nyingi tu zinazomuhusu Pole Pole mmeacha zijitegemee bila kuziunganisha na uzi mungine, lkn wa kwangu ndo mmeona wa kuunganishwa. Kama hamuhitaji baadhi ya watu tuwe tunaandika chochote ni bora mkatutahadharisha mapema ili tuachane na jukwaa lenu kuliko kufanya jambo bila kushauriana na anaefanyiwa. Naomba muufute kabisa uzi wang maana sioni sababu au faida ya kuendelea kuachwa hapa. Mbaki na hizo mnazozitaka zisomwe hapa jukwaani.
 
Kwakuwa amekiuka miiko yenu haupo nyuma ya huo mpango wa kumnyamazisha kweli?
 
1) Polisi huwa hawana taratibu za kukamilisha uchunguzi kwa haraka kiasi hicho- Tukio lilitokea usiku wa jana mara leo hii uchunguzi umekamilika.
2) Hata mimi ukiniuliza bei ya TV yangu na, suti ya harusi na jiko la kupikia sijui. Kwa vile nilipewa zawadi na shemeji yangu wa Afrika kusini. Na kutokana na tamaduni zao, zawadi kamwe husemi bei wakiamini kuwa zawadi hutolewa toka moyoni na si kutokana thamani ya kitu.

Hivyo kwangu kutojua bei ya TV wala sio ishu.
 
Hivi Tafsiri ya Nyumba siku hizi imebadilika? Si angesema tu watu wamevania chumbani kwake na kukuta mafuta ya KY?
 
Mbona Lissu hamkutoa wito ajibiwe kwa hoja?
kwahyo unaafiki kunyamazishana kwa njia ya vitisho sio.

Je huo ni msimamo wako au ni wa taasisi unayoishabakia?

Kwa maneno mengne unapingana na peter msigwa kuhusu hili la kujaribu kumnyamazisha polepole kimaguvu.

Hv katika akili ya kawaida, ni polepole himself ndiye unaamini aliyewaziba midomo wapinzani!
 
Sawa tu walivyofanya mara nyingi nimekuwa nikijisea ningekuwa mods, miongoni mwa ambao wangekula ban nyingi acha kuunganishiwa nyuzi ni pamoja na anayelialia.
 
Pole pole anavuruga nyumba yake mwenyewe halafu anaichafua serikali yetu. Polepole ni mhuni.

Kinachoenda kwa kuzunguka kinarudi kwa kuzunguka.
 
Ikiwa hivyo vitu alipewa sawa nakubaliana na ww, lkn kama alivinunua mwenyew afu leo ashindwe kujua thaman yake basi hili litakuwa ni tukio la kutengeneza.
 
Hivi Pole pole hana mke? au alienda Manyara na mke wake?? Kama hana mke basi kwa tafsiri ya kiswahili Polepole bado ni mhuni !
 
Afadhali umeandika. Nilihisi jambo kama hilo mtu mwenye akili zake eti akupekue aibe tv?????
 
kweli wabaya hulipwa hapahapa malipo yameanza pole pole utaelewa tu,aliyofanyiwa lisu nani atamlipia bwana kiroboto,ewe kiroboto unakumbuka mlichomfanyia mbowe nani nayeye atamlipia
 
Maisha yapo kasi sana
 
Huko Malawi tetesi uvumi bila cheti cha chanjo COVID huingii,
Je, mheshimiwa balozi mteuliwa, atachanja??
Au atakuwa muungwana na kuukacha ubalozi ili asimamie msimamo wake??

Njaaa bana😁
Kama yule Bashiru aliyesema hatakubali tena uteuzi mwingine
 
Madaraka ni kitu cha kupita , huyu alikua miongoni mwa watu walioogopeka ila miezi michache tu baada ya aliyempa kiburi na kumjazia walinzi kuondoka kuondoka akabaki kama kinda la ndege.

Nyie machawa wa sasa mpite hapa mjifunze.
 
Madaraka ni kitu cha kupita , huyu alikua miongoni mwa watu walioogopeka ila miezi michache tu baada ya aliyempa kiburi na kumjazia walinzi kuondoka kuondoka akabaki kama kinda la ndege.

Nyie machawa wa sasa mpite hapa mjifunze.
πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Kidogo Apasuliwe Speaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…