Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Nzuguni katika maadhimisho ya miradi iliyozinduliwa katika kilele cha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kikiwamo kituo cha Zimamoto na Uokoaji.
Kijana huyo alitoa tuhuma hizo, baada ya Waziri Mkuu kutoa nafasi kwa wananchi kuzungumza kero zinazowakabili ili waweze kupata msaada.
Alipopata nafasi hiyo, alidai mwanajeshi huyo aliyemtaja kwa jina maarufu la HK, kunyanyasa vijana wa eneo hilo na yeye akiwamo kwa kuchukuliwa TV yake kwa madai kuwa kuna mtu amemuambia kuwa amemuona na simu ya mke wake.
“Alikuja nyumbani kupekua vitu vya nyumbani kwangu zikiwamo nguo za ndani za mke wangu kwa kuziinua huku akizinyanyapaa, alipokosa simu aliamua kubeba TV na kuondoka nayo na jana amenipigia simu kuniambia kuwa kero yangu hata nikipeleka kwa Rais Samia haitatatulika…naomba Waziri Mkuu nisaidiwe afuatiliwe,” alilalamika.
Waziri Mkuu alimuagiza Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Martin Otieno, kumsaidia kijana huyo na kumtafuta mwanajeshi huyo ili akamatwe.
“Pia nitazungumza na CDF (Mkuu wa Majeshi) kama anavyoeleza kijana huyu kama ndivyo kamanda yeyote wa jeshi lolote hapaswi kuwafanya hivyo Watanzania, jeshi lipo kwa ajili ya kuwalinda wao, maisha yao, vifaa vyao na mali zao zinakuwa salama sio kwenda kuchukua mali zao,” alionya.
“Huyo kijana apatikane na kama atakataa tutapata taarifa zake kwenye kikosi alipo na tutamtafuta CDF atatupa mawasiliano ili tujue kwanini amechukua TV ya huyu kijana. Huyu kijana apewe ushirikiano anaweza kupata matatizo na huyo kamanda akisikia ametamkwa hadharani, huyu kijana alindwe asipate madhara.”
Alisema taarifa ya kijana hiyo ichukuliwe kama taarifa kamili na ifanyiwe kazi ili apate haki yake ya msingi.
Chanzo: Nipashe