Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
katafute state ya kwako. wananchi kutoa malalamiko yao kwa viongozi wao wa kitaifa ni jambo la kawaida halijaanza leo wala jana lilikuwepo na litaendelea. we ndio failing person. Ktu kidogo tu mtu anakimbilia kuisema vibaya serikali. we ndio umefeli umejaa frustrations.
Wewe unayetetea habari za wananchi kutoa malalamiko yao ya kuibiana simu na TV, kupigana, kwa viongozi wa taifa hujui hata hesabu kuna wananchi wangapi, malalamiko mangapi kama hayo, na viongozi wa kitaifa wangapi. Utakubali mpaka kesi ya mtu kuibiwa kuku imsubiri rais na waziri mkuu, wakati kuna polisi na mahakama.
Halafu huelewi kwamba, jambo kuwa la kawaida haimaanishi ni zuri. Jambo linaweza kuwa ni baya na la kawaida, watu wamelizoea. Kulizoea hakufanyi lisiwe baya.
Serikali itasemwa vibaya tu, hiyo ni haki ya watu ya kikatiba. Ukinilalamikia kwa kuisema serikali vibaya, unanionesha huna elimu ya uraia na hujui haki za kikatiba ni zipi.
Zaidi, umeshindwa kujibu hoja, unanishambulia mimi mtoa hoja kwa ad hominem attacks, hii ni ishara ya mtu asiye na hoja.