Dodoma: Waziri Mkuu aagiza Mwanajeshi, maarufu kama HK akamatwe kwa udhalilishaji

Dodoma: Waziri Mkuu aagiza Mwanajeshi, maarufu kama HK akamatwe kwa udhalilishaji

Ad hominem attack, umekosa hoja, unamshambulia mtoa hoja.

Nishaandika kujibu swali lako kabla hujaliuliza, soma post #21

Tatizo, unajua kusoma kwa ufahamu?
wewe kafiri kweli sasa hebu nikuambie matukio kama hayo yapo mengi sana na ni vizuri yakitatuliwa kwa njia hiyo ili nawengine nao wasikie
 
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Nzuguni katika maadhimisho ya miradi iliyozinduliwa katika kilele cha sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kikiwamo kituo cha Zimamoto na Uokoaji.

Kijana huyo alitoa tuhuma hizo, baada ya Waziri Mkuu kutoa nafasi kwa wananchi kuzungumza kero zinazowakabili ili waweze kupata msaada.

Alipopata nafasi hiyo, alidai mwanajeshi huyo aliyemtaja kwa jina maarufu la HK, kunyanyasa vijana wa eneo hilo na yeye akiwamo kwa kuchukuliwa TV yake kwa madai kuwa kuna mtu amemuambia kuwa amemuona na simu ya mke wake.

“Alikuja nyumbani kupekua vitu vya nyumbani kwangu zikiwamo nguo za ndani za mke wangu kwa kuziinua huku akizinyanyapaa, alipokosa simu aliamua kubeba TV na kuondoka nayo na jana amenipigia simu kuniambia kuwa kero yangu hata nikipeleka kwa Rais Samia haitatatulika…naomba Waziri Mkuu nisaidiwe afuatiliwe,” alilalamika.

Waziri Mkuu alimuagiza Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Martin Otieno, kumsaidia kijana huyo na kumtafuta mwanajeshi huyo ili akamatwe.

“Pia nitazungumza na CDF (Mkuu wa Majeshi) kama anavyoeleza kijana huyu kama ndivyo kamanda yeyote wa jeshi lolote hapaswi kuwafanya hivyo Watanzania, jeshi lipo kwa ajili ya kuwalinda wao, maisha yao, vifaa vyao na mali zao zinakuwa salama sio kwenda kuchukua mali zao,” alionya.

“Huyo kijana apatikane na kama atakataa tutapata taarifa zake kwenye kikosi alipo na tutamtafuta CDF atatupa mawasiliano ili tujue kwanini amechukua TV ya huyu kijana. Huyu kijana apewe ushirikiano anaweza kupata matatizo na huyo kamanda akisikia ametamkwa hadharani, huyu kijana alindwe asipate madhara.”

Alisema taarifa ya kijana hiyo ichukuliwe kama taarifa kamili na ifanyiwe kazi ili apate haki yake ya msingi.

Chanzo: Nipashe
Yanayotokea mitaani ni taswira ya yanayofanywa na Serikali. Anza na serikali yako.
 
Jamaa hana Makosa ni ujanja tu amechezewaView attachment 2602006
Naam ni ndipo uzuri wa kufanyia kazi taarifa za pande zote ulivyo na sio kuegemea upande mmoja na mihemko ya kisiasa matokeo yake kuumiza upande mmoja
Ona Sasa HK Kakaa ndani bila sababu na sijui huyo jamaa atachukuliwa hatua gani kwa kumdanganya waziri mkuu na kuumiza na kuchafua taswira ya HK
 
wewe kafiri kweli sasa hebu nikuambie matukio kama hayo yapo mengi sana na ni vizuri yakitatuliwa kwa njia hiyo ili nawengine nao wasikie
Matukio kama hayo kuwa mengi yatatatuliwa vipi na Waziri Mkuu mmoja?

Unaizidishia nguvu hoja yangu kwamba mifumo ya ku deal na matukio haya imeanguka, ndiyo maana watu wanaona bora wampelekee matatizo yao ya kuibiana na kupigana mtaani Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu atasuluhisha mpaka migogoro ya kifamilia kwa mtaji huu.
 
Hata kama nikiwa Mwalimu ila hatuwezi kuzifanya tuhuma kama ndio ushahidi usio na mashaka.

Ni tuhuma tu unless kuwe na ushahidi ulio wazi
Uko sahihi Kamanda.
 
Tukiachana na hilo mana huna hoja 7bu WAZIRI mkuu ameagiza akamatwe SHERIA ichukue mkondo wake ajamuhukumu na wala hajasema afukuzwe kazi au ahukumiwe kifungo ameagiza akamatwe na mwenye TV yake arudishiwe na akome KUSHIKASHIKA CHUPI ZA WAKE ZA WATU 7BU ANALIDHALILISHA JESHI

Sasa Nitajie sehemu moja tu ambayo hakuna AMANI kwenye mapigano fujo mauaji ambapo watu wanapakimbia achana na hizo nyingi ulizosema nitajie tu sehemu moja
Mheshimiwa, Je HK kakutwa na hilo kosa?
Aibu tutaweka wapi na matamko?
 
Sawa sawa
Basi ndugu yangu sisi tunajivunia TANZANIA yetu
Na namna Viongozi wetu wanavyosikiliza kero zetu DIRECT na kutupatia MAJIBI chanya papohapo
Na tulijivunia sana MAGUFURI mana yeye alikuwa mpk anatoa alichonacho kusaidia
Kabla ya MAGUFURI hata kikwete alikuwa anasikiliza kero zetu DIRECT mara chachechache

Hvyo kama hujapenda WAZIRI MKUU alivyoagize awajibishwe huyo MWANAJESHI mjingamjinga anayelitia doa JESHI letu imara
Nenda uhamie SUDAN
Ok rpc kaona mjeda hana kosa, mkosaji ni huyu dogo. Sura mtaziweka wapi?
 
Kwa mujibu wa nani? Wapi nilisema hivyo?

Watanzania wengi kama wewe wana mawazo ninayoyaita "one track mind".

Mawazo yao ni kama yanafuata reli ya treni, hawawezi kufikiri nje ya reli.

Wakimuona mtu kakosoa Waislamu, basi mara moja wanafikiri huyu lazima atakuwa Mkristo.

Wakiona mtu anakosoa serikali ya Samia, basi mara moja wanafikiri huyu lazima atakuwa team Magufuli.

Wakati kuna watu wengine Waislamu na Wakristo tunawaweka fungu moja, na hao Magufuli na Samia hatukubali kwamba wana tofauti kubwa kama wengi wanavyosema.

Sasa unaniuliza swali hilo la Magufuli kwani wapi nilimtetea Magufuli hapa mimi?
Mkuu unashusha nondo sana ndio maana Kila siku lazima nisome comments zako.


Upo neutral na open mind

Big up!!
 
Back
Top Bottom