Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Kesho tutakaza macho kuona itifaki, taratibu, kanuni, sheria na mazowea ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa yaleyale kwa CHADEMA mjini Dodoma kama ilivyokuwa kwa mwenyekiti wa CCM ambaye ni mtia nia Urais aliyowasili ktk Ofisi ya Tume kuchukua fomu

Tujikumbushe jinsi Tume ya Uchaguzi walichofanya kwa Magufuli jana :

Hizo ndinga ni za Ikulu ccm wamepaka rangi eee.
 
Nimeona ndege za kijeshi zimewasili asubuhi na mapema[emoji2]
 
Lissu aliutangazia ulimwengu kuwa Tanzania kuna Corona na Serikali haisemi ukweli na haichukui tahadhari ya kujilinda. Yeye amejipanga vipi kuhusu social distancing, kunawa maji tiririka na kuvaa barakoa? Au ATAMUIGA Rais Magufuli kutovaa barakoa kwa kuwa HAKUNA Corona!?
Hakuna muda wa kujibu maswali ya kipuuzi, tuko busy muda una taradadi!
 
Kwani tume wanaona shida gani kusema kama leo hawatakuwepo ili wasiwape cdm hayo matukio? Sehemu zote kwenye watu au taasisi zenye nia njema, huwataarifu wadau wao kuwa siku fulani hawatafungua ofisi, na huweka sababu ya kutofungua ofisi. Unaposema Membe alienda jana, kwani cdm wanafanya mambo yao kwa kuwaiga ACT?
Hao watu wakuonea huruma. Kila wakifungua kinywa kujisafisha ndio wana haribu zaidi!
 
Kwani tume wanaona shida gani kusema kama leo hawatakuwepo ili wasiwape cdm hayo matukio? Sehemu zote kwenye watu au taasisi zenye nia njema, huwataarifu wadau wao kuwa siku fulani hawatafungua ofisi, na huweka sababu ya kutofungua ofisi. Unaposema Membe alienda jana, kwani cdm wanafanya mambo yao kwa kuwaiga ACT?
Nimesema Membe alishauriwa na NEC sijui hujaelewa nini? Tatizo letu Watanzania hasa wapenzi wa vyama wanapenda kutetea hata matatizo. Hilo wanalo ccm na wapinzani pia ndiyo maana wanasiasa wetu hawawezi kuwajibishwa sababu tupo nyuma yao hata kwa mambo ya kipuuzi. Hapa nilikua nalalamika Magufuli kuwanyima wapinzani haki ya kikatiba kufanya mikutano watu wa ccm waliniita nyumbu. Hata nilipolalamika kwanini Mbowe bado ni mwenyekiti wakati chama chake kimeshindwa chaguzi 4 ama tano chini ya uongozi wake niliitwa book saba. Watu wanataka utoe maoni wanayoyapenda wenyewe kuyasikia halafu tunataka demokrasia wakati sisi wrnyewe tunanyimana hiyo demokrasia unadhani wanasiasa watatusikiliza?
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati Area C Mtaa wa Makongoro.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.

#NiYeye2020
Acha uongo, watu wametoka sehemu mbali mbali wakalala kwenye mahoteli afu unasema wakazi wa Dodoma?
 
LISU UYO
IMG_20200808_071452_519.jpeg
 
Basi kaa na kura yako nyumbani kwako, sisi tunataka taifa linaloongozwa kwa sheria na katiba na Lissu ndio tumaini la kutupeleka huko.
Niliotoa ni ushauri sio sheria, anaweza kuuchukua au kuuacha
 
Back
Top Bottom