Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Uchaguzi 2020 Dodoma yazizima kwa Maandalizi ya Lissu kuchukua fomu 8.8.2020

Lissu kuwa Ikulu ndiyo heri ninayo itaka,kwa hiyo dalili zote zote hasa za kitoto zinazoashiria kukwamisha heri hiyo ndizo ninazozichukua.
Endelea na uparoko sisi utatuka mbele ya safari,hata biblia ilisema ukipigwa la kushoto geuza la kulia,ila wakakuachia mwenyewe ujiongeze baada ya kupigwa la kuliq uchukue hatua gani
 
Inawezekana kabisa Rais ajaye wa JMT amechukua fomu leo trh 08/08/2020.

Nilipomwona wakati anaingia ndani ya jengo la Tume ya uchaguzi nikawaza kwa madhira aliyokutana nayo kwa akili za kibinadamu asingekua anapanda zile ngazi, inawezekana kabisa angekua kimya futi6 ndani ya ardhi lkn Mungu alikuwa na mpango mwingine kabisa.

Kama ambavyo wako waliodhani hataiona siku hii basi binafsi naamini lolote linawezekana october 28.
 
Tunashukuru Molemo kwa kuleta hii habari. Kuna uzito fulani kwenye kitengo cha habari cha cdm, kiasi kwamba kuna uzi humu jukwaani unaohimiza kitengo cha habari kuamka. Kuna ushauri pia kuhusu Tundu Lisu jinsi ya kufanya siasa zake bila kupoteza credibility yake. Ni vyema kama chama mkakaa na Lisu na kumfunda. Kuna baadhi ya maneno anaongea yanampotezea haiba yake.
Uko sahihi mkuu.
 
Mkuu Unaona sasa ninyi wafuasi wa CHADEMA tunaposema elimu yenu ni ndoto hamuelewi,haujui tofauti ya basic needs na social services

Ngoja nikupeni ilimu shekhe,basic needs ni tatu tu chakula,malazi na mavazi, wakati social services ni kama umeme ,maji elimu,huduma za afya nk

Jioange unapojibu hoja humu maana unaonekana kituko
Kama kusoma ndiyo huku basi bora kutoenda shule...Yaani karne hii unaongelea basic hizi tatu....daaah
 
Nimesema Membe alishauriwa na NEC sijui hujaelewa nini? Tatizo letu Watanzania hasa wapenzi wa vyama wanapenda kutetea hata matatizo. Hilo wanalo ccm na wapinzani pia ndiyo maana wanasiasa wetu hawawezi kuwajibishwa sababu tupo nyuma yao hata kwa mambo ya kipuuzi. Hapa nilikua nalalamika Magufuli kuwanyima wapinzani haki ya kikatiba kufanya mikutano watu wa ccm waliniita nyumbu. Hata nilipolalamika kwanini Mbowe bado ni mwenyekiti wakati chama chake kimeshindwa chaguzi 4 ama tano chini ya uongozi wake niliitwa book saba. Watu wanataka utoe maoni wanayoyapenda wenyewe kuyasikia halafu tunataka demokrasia wakati sisi wrnyewe tunanyimana hiyo demokrasia unadhani wanasiasa watatusikiliza?

Nadhani hoja yangu iko wazi, kama NEC walimshauri Membe, kwanini wasiishauri cdm hivyo hivyo? Maelezo yako ni mazuri na marefu, ila hayakuwa na ulazima wowote. Ndio maana tunahitaji tume huru vya uchaguzi, sio hii iliyojigeuza taasisi ya kisiasa dhidi ya baadhi ya vyama.
 
Nadhani hoja yangu iko wazi, kama NEC walimshauri Membe, kwanini wasiishauri cdm hivyo hivyo? Maelezo yako ni mazuri na marefu, ila hayakuwa na ulazima wowote. Ndio maana tunahitaji tume huru vya uchaguzi, sio hii iliyojigeuza taasisi ya kisiasa dhidi ya baadhi ya vyama.
Huwa hawajielewi wanataka nini
 
Mambo ni moto dodomaa
20200808_115730.jpg
20200808_115701.jpg
20200808_115609.jpg
20200808_115537.jpg
20200808_115501.jpg
 
Toa sababu, au ndio sera za kumuachia Mungu.

Kama yule binti wa kimarekani asingerusha clip ya George Floyd, wale polisi leo wangekuwa wanakula bata tu.
Hatutegemei kura za huruma bali tunataka mtuchague kwa sera zetu
 
WanaJF

Dodoma Inazizima.Ndivyo tunavyoweza kusema kwa Sasa.

Mapokezi kabambe yanamsubiri mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Antipass Lissu ambaye atachukua rasmi fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho siku ya Nane Nane.

Inatarajiwa mgombea huyo kusindikizwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Dodoma katika kile kinachoonyesha Imani kubwa waliyo nayo kwa kiongozi huyo.

Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu ametoa wito rasmi kwa wakazi wa jiji la Dodoma na mikoa jirani kumsindikiza mgombea huyo Safari itakayoanzia makao makuu ya Chadema Kanda ya Kati Area C Mtaa wa Makongoro.

Katika mahojiano na wakaazi kadhaa wa jiji Hilo wameonyesha shauku kubwa ya kutaka kumuona Tundu Lissu ikiwa ni miaka mitatu alipoondolewa katika jiji Hilo akiwa nusu mfu baada ya kupigwa risasi kumi na sita na watu wasiojulikana na Sasa anarejea jiji Hilo Hilo akiwa mzima wa afya na akitembea kwa miguu yake miwili huku wabaya wake waliotaka kumuua wakifichama kusikojulikana.

Hapo Jana wanafunzi wa vyuo vikuu vya UDOM, CBE na Mipango walikuwa katika vikao vya namna ya kumsindikiza Lissu ambaye walimwita shujaa wao.

Tundu Lissu amejizolea uungwaji mkono na umaarufu mkubwa kutokana na sera yake ya kuwapa watu Uhuru wa kusema na kutoa maoni yao bila kuingiliwa na vyombo vya Dola endapo atachaguliwa kuwa Rais.Na pia kuruhusu vyama vya siasa. NGO's na vyombo vya Habari kufanya kazi zake kwa Uhuru Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Chadema leo inatarajiwa kutoa ratiba njia atakazopita mtetezi huyo wa wanyonge na Msemaji wa wasio na sauti ili walau watu kujipanga manjiani kumsalimia na kumsindikiza.

#NiYeye2020

Updates leo tarehe 8/8 Jumamosi

Tayari mgombea wa Urais Tundu Lissu amewasili katika ofisi ya Chama Kanda ya Kati na amesaini kitabu Cha wageni na kupata ukaribisho na maelezo mafupi kutoka viongozi wa Kanda.

Kwa Sasa msafara wa kuelekea Tume ya uchaguzi umeanza ukiongozwa na pikipiki nyingi, magari makubwa ya mabasi na madogo huku wananchi wengi wakiwa kandokando ya Barabara waliounga mikono

Live Millard Ayo na UTV ya Azam

Saa 5 kamili Jumamosi

Mgombea wa Urais Tundu Lissu ndiyo anaingia hapa Time ya Taifa ya Uchaguzi akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama wafuasi na wananchi.

Chadema imetii masharti ya Tume ya Uchaguzi kwamba wafuasi na mashabiki wabaki nje na ndani wameingia viongozi wachache kumsindikiza Lissu.Viongozi waliomsindikiza Lissu ndani kwenye ukumbi ni Godbless Lema,Peter Msigwa,John Heche,Suzane Kiwanga na Baraka Mwago wote wakiwa Wajumbe wa Kamati Kuu.

Hamasa ni kubwa Sana na hapa ukumbini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi yupo na meza yake Kuu wakisubiri kuingia mgombea Urais na Mwenza wake

Saa 5.20

Lissu akiwa na mgombea Mwenza wake wameingia kwenye ukumbi na Mkurugenzi wa uchaguzi ndiyo anatoa maelekezo kwa wagombea

Mheshimiwa Lissu anasikiliza kwa umakini mkubwa na kwa utulivu maelekezo ya Mkurugenzi wa Tume.

Sasa Mkurugenzi amemaliza kuongea na amemkaribisha Mwenyekiti Jaji Kaijage kukabidhi fomu kwa wagombea.Mwenyekiti anatoa maelezo mafupi ya nyongeza

Saa 5.27

Rasmi Sasa Tundu Lissu anakabidhiwa fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano baada ya kukamilisha mambo yote muhimu.Mgombea Urais na Mgombea Mwenza wanapokea kwa Pamoja huku makofi yakipigwa.

Saa 5.32
Shughuli zimekamilika rasmi hapa ndani ya ofisi ya Tume na kuagana rasmi Kati ya viongozi wa Tume na Chadema.

Umati mkubwa Sana wa wafuasi wa Chadema unasubiri nje ya ofisi ya Tume huku watu wengi wakiwa wanafuraha kubwa isiyoelezeka
Molemo hata picha wala video?? Duuh mnatuangusha mazee.kwani mmezuiliwa??
Chadema swala.la Tehama mko nyuma sana sijui kwanini. Nyie ndio mnataka tuwape nchi?? You are so slugish. Shame on you!
 
Hao wapiga zumari tu wala sio watendaji, watu wapo ila nikichokiona wengi sio wa mitandao yaani wa kupost post tu.
Molemo hata picha wala video?? Duuh mnatuangusha mazee.kwani mmezuiliwa??
Chadema swala.la Tehama mko nyuma sana sijui kwanini. Nyie ndio mnataka tuwape nchi?? You are so slugish. Shame on you!
 
Back
Top Bottom