Dogo amenikera mpaka nahisi kumchukia mazima

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Ipo hivi, kuna mdogo wangu mtoto wa mama mkubwa kaolewa Arusha, sasa akikwama mambo ya hapa na pale huwa namsaidia maana tumezoeana sana kwahiyo haonagi shida kunishirikisha akikwama.

Sasa kilichonikera ni kwamba alinipigia simu akaomba nimsave kiasi fulani hivi, nikamwambia kwasasa nipo mbaya sina kitu.

Nikamuuliza kwani hujamuomba kaka j akusaidie? Maana huyu ndo kaka yake wa damu, aisee alichojibu sasa, akasema kwamba si unajua tena kaka j anafamilia yake anaihudumia, mtoto mke wake. kwahiyo siwezi kumuomba ntamharibia mipango yake.

Aisee nikawaza kwahiyo Mimi ambaye sina mke ndo fala ni za kuchota tu na bado namuwaza vibaya mno. Halafu mbaya zaidi ananiforce kwamba nitumie mbinu zote nimtumie hiyo hela ana shida ya muhimu sana.

Daaaaah simmalizi kabisa kenge yule
 
What is this?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…