Doing Business in Mozambique

Wakuu wote wafanyabiashara wa Moza

kwa nini msiunde umoja wenu wa wafanyabiashara watanzani wa huko moza ili kuweza kusaidiana katika nyanja zote, hii itasaidia pia kutoa dira na mwongozo kwa wafanya biashara wengine wanotaka kujumuika nanyi huko moza,

kwa vinginevyo mnaweza mkashirikiana na umoja wa wafanyibiashara mbali mbali wa huku tanzania hivyo basi wakati mwingine bidhaa inapokuwa hadimu na kuhitajika moza basi inakuwa ni kupeana taarifa tu kwa simu au mitandao na bidhaa husika kutumwa haraka bila wahusika kusafiri, nadhani hii inaweza kuwa network nzuri sana ya kibiashara

haya ni mawazo na maoni yangu binafsi

tupo pamoja wakuu wa moza
 
Wewe upo maputo au wapi?
 
hivi jamani mozambique ni sehemu nzuri ya kusoma vyuo au bora nibaki humuhumu bongo? Nisaidieni jamani...
 
hivi jamani mozambique ni sehemu nzuri ya kusoma vyuo au bora nibaki humuhumu bongo? Nisaidieni jamani...

nadhan bora ubaki nyumban coz wenyewe kwenye upande wa elimu wako nyuma
 
mkuu LAT sisi huku Nampula tuna kaumoja ketu sio mbaya wakati wa shida tunasaidiana japo wabongo tunauzito fulani.lakn tunasonga!
 
mkuu LAT sisi huku Nampula tuna kaumoja ketu sio mbaya wakati wa shida tunasaidiana japo wabongo tunauzito fulani.lakn tunasonga!

mkuu dickson, safi sana, hayo ndiyo mambo mazuri ya kimaendeleo kwani network na kushirikiana huleta nguvu katika jambo lolote, leo mimi kesho wewe and visa versa

tuwasiliane mkuu kwa lolote lile

pamoja
 
mkuu LAT sisi huku Nampula tuna kaumoja ketu sio mbaya wakati wa shida tunasaidiana japo wabongo tunauzito fulani.lakn tunasonga!

Dah bora nimekupata. Nambie hapo nampula paoo(mikate) Ile migumu inatoka? na Vipi mtu ukitengeneza ya kama tz Inaweza toka? Mie niko Pemba, Ila nasikia nampula panalipa sana.
 
Mi naomba kujua zaidi kuhusu nguo na accessories na cosmetic ni mji gani inalipa na je ni njia gani nzuri ya kufanya. Asante
 
Mkuu Edgartz, nimeangalia kwenye google earth inaonekana Tete ni mbali sana toka Mtwara usafiri wa kuja huko ukoje? mnapitia wapi?
 
Jamani mlioko huko Moza hasa Maputo, gharama za kufika huko toka Dar zikoje kwa kupitia Mtwara? Na plan kuja huko kuona nini cha kufanya miaka michache ijayo. Ulaya nimechemsha,ubavu wa kufanya vitu Ulaya kwa sasa sina,ila Moza naweza kumudu.
 
kutoka dar mpaka mtwara ni 18000. Mkifika mtwara lala gest flan inaitwa chilindima kusudi asubuh uwah gar za boda. Kutoka mtwara mpaka boda n 5000. Kuvuka mto huwa inaenda mpaka 15000 Ila kama ukinegotiate n 5000 masika, kutoka boda mpaka wilaya flan inaitwa mocimbou n MT 350. sasa hapa unaweza amua kwenda nampula au Pemba kwa ajili ya kupata basi za Maputo. Ukienda Pemba nauli n MT 270. Gharama za gest ziko juu sana Ila kuna hotel flan inaitwa cabo delgado range huwa n kama Mt. 300-500 bila msos. Kutoka Pemba mpaka Maputo kwa basi n MT 2800 Ila bas kama ckosei zipo mara mbili kwa wiki na ni safari ya siku mbili na nusu kwa ndege n MT 9000.
 
Mi naomba kujua zaidi kuhusu nguo na accessories na cosmetic ni mji gani inalipa na je ni njia gani nzuri ya kufanya. Asante

kama unataka fanya kwa rejareja Ili uvune faida kubwa Njoo Pemba Ila kama Unataka jumla nenda nampula. Karibu
 
mkuu LAT,kuhusu agro product kaburu kamaliza kila kitu,vitu kama njugumawe/choroko tunazila sie wageni kwahiyo soko lake sio kubwa kihivyo. Hawa jamaa wanapenda sana nyama ya nguruwe/ng'ombe/kuku/samaki na mboga zao za majani.
 
Msumbiji kiufupi huduma nyingi ni mbaya. Ndiyo maana chochote unachofanya kinalipa. Huduma za afya ndiyo usiseme.. Dhaifu sana!
 
Msumbiji kiufupi huduma nyingi ni mbaya. Ndiyo maana chochote unachofanya kinalipa. Huduma za afya ndiyo usiseme.. Dhaifu sana!
 
kama unataka fanya kwa rejareja ili uvune faida kubwa njoo pemba ila kama unataka jumla nenda nampula. Karibu
ila lugha ni issue speedy,lizzard. Full kireno.na hela nazo ni changamoto nyingine. Namba iliyoandikwa sio thamani yake kama huku tz unavyotafsiri hela kirahisi. Mfano noti ya 200 thamani yake sina hakika ni kama elfu kumi ya tz na ni kama elfu arobaini mitkash..ila watu wengi wanatoka kimaisha huko mi niko mtwara naona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…