DOKUMENTARI - Usaliti kwa MAGUFULI Hadi Saa Yake ya Mwisho

DOKUMENTARI - Usaliti kwa MAGUFULI Hadi Saa Yake ya Mwisho

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
02 Agosti 2026

Dokumentari - Usaliti kwa MAGUFULI Hadi Saa Yake ya Mwisho


View: https://m.youtube.com/watch?v=de8Zv6MMh8c
🔴MUHTASARI WA VIDEO ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ Rais John Pombe Magufuli alikuwa nani, na ni nini hasa kilitokea katika siku za mwisho za maisha yake?

Makala hii inachunguza maisha ya ajabu, uongozi, mafanikio, utata, na kifo cha Rais wa tano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, maarufu kama "The Tingatinga."

Kuanzia mwanzo wake kutoka katika Kijiji cha Chato hadi kuwa mmoja wa viongozi wanaozungumziwa zaidi barani Afrika, makala hii inafuatilia safari yake kupitia kampeni kubwa za kupambana na ufisadi, mageuzi ya serikali, miradi mikubwa ya miundombinu, sera za kiuchumi, na majibu yake yenye utata kwa janga la COVID-19.

Makala hii pia inachunguza simulizi rasmi ya kifo cha Magufuli pamoja na maswali, mijadala, na mitazamo tofauti iliyoibuka kote Afrika na kimataifa.

Inaonyesha simulizi iliyomo katika makala hii ikiibua mambo huku ikikiri kwamba baadhi ya madai yake bado zinapingwa.

Ndani ya makala hii:
• Maisha ya awali ya Magufuli na kupanda kwake madarakani
• Mapambano yake dhidi ya ufisadi na wafanyakazi hewa
• Mageuzi makubwa ya miundombinu na kiuchumi
• Migogoro ya mikataba ya madini na sera za utawala •
Tanzania wakati wa COVID-19
• Matukio yaliyopelekea kifo chake
• Legasi ya Urithi wake na athari kwa Tanzania na Afrika pia.

Makala hii ipo wazi kwa maoni Iwe unampongeza Magufuli, unamkosoa uongozi wake, au unataka tu kumwelewa mmoja wa marais wa kisasa wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, makala hii inatoa maelezo ya kina kuhusu mtu huyo, awamu ya urais wake, na mijadala inayoendelea baada ya kifo chake
1785785693463.png
 
Kuna mengi sana ya kuchangia hapa.

Lakini kwanza:

Kichwa cha mada kinazungumzia "Usaliti kwa Magufuli".

Natumaini hili la usaliti litajadiliwa kwa kina kinachostahiki.

Binafsi kwenye "Documentary" hiyo ningependa kuona maoni ya kutosha kwa 'characters' muhimu wa movie hii muhimu sana.

Ukimuweka pembeni Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa kweli simpi uzito katika movie hii ya usaliti, wacheza movie hiyo wenye mchango mkubwa wa kuinogesha sidhani kuwa kutakuwepo na wengi zaidi ya akina Kabuti Kalamaganda. Character itakayochezwa kumwakilisha huyu mtu mwenye mijicho kama ya bundi ni kati ya wanogeshaji wakuu wa sinema hii.

Nitashiriki kumjadili 'stelingi' mkuu wa sinema yenyewe, ambaye ni JIWE mwenyewe; kwa mazuri yake, na mabaya maovu kabisa ya utawala wake.
 
Kumjadili Magufuli ni lazima kuanzia kwenye mambo machache kama yafuatayo.fa na majivuno
1. Kujituma kufanya mambo anayotakiwa kuyafanya. 'Discipline' ya kuyatekeleza, hata kama siyo kwa usahihi.

2. Kukiuka taratibu/sheria katika adhma ya kutimiza anayoona yeye ni ya muhimu

3. Kutumia mabavu, pale anapoona uwezo wa kufanya hivyo anao; lakini pia kunyamaza na kuumia ndani kwa ndani pale mambo anayotaka hayaruhusiwi na wakuu walio juu yake. Mfano; Jengo la Tanesco.

4. Kupenda kusifiwa na majigambo

5. Inawezekana Magufuli aliguswa na hali ya waTanzania maskini, na pengine hata kuchukia rushwa. Mtindo wake wa kuyafanyia kazi haya inatatiza na kufanya kuwa vigumu kujuwa hasa dhamira yake ya kweli ipo wapi.

Ila ni wazi kwamba alichukizwa juu ya raslimali za Tanzania kuporwa na mafisadi wakishirikiana na watu kutoka nje ya nchi.

6. hakujuwa kutumia sahihi madaraka makubwa aliyokuwa nayo, kiburi, vyote ni sehemu iliyopelekea umauti wake.
Mtu unayetarajiwa kujuwa taratibu za kisayansi, kutokana na kisomo alichokuwa nacho; halafu ubishie kijinga vile uwepo wa COVID-19; na kuhimiza watu wakajifutike?
Unapeleka sampo za mapapai na vitu vya ajabu ku-evaluate vipimo vya kisayansi, na kuadhibu watu kwa matokeo mabaya ya vipimo? Hiyo sayansi ya kemia ilimfundisha nini yeye?
 
02 Agosti 2026

Dokumentari - Usaliti kwa MAGUFULI Hadi Saa Yake ya Mwisho


View: https://m.youtube.com/watch?v=de8Zv6MMh8c
🔴MUHTASARI WA VIDEO ▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬▬ Rais John Pombe Magufuli alikuwa nani, na ni nini hasa kilitokea katika siku za mwisho za maisha yake?

Makala hii inachunguza maisha ya ajabu, uongozi, mafanikio, utata, na kifo cha Rais wa tano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, maarufu kama "The Tingatinga."

Kuanzia mwanzo wake kutoka katika Kijiji cha Chato hadi kuwa mmoja wa viongozi wanaozungumziwa zaidi barani Afrika, makala hii inafuatilia safari yake kupitia kampeni kubwa za kupambana na ufisadi, mageuzi ya serikali, miradi mikubwa ya miundombinu, sera za kiuchumi, na majibu yake yenye utata kwa janga la COVID-19.

Makala hii pia inachunguza simulizi rasmi ya kifo cha Magufuli pamoja na maswali, mijadala, na mitazamo tofauti iliyoibuka kote Afrika na kimataifa.

Inaonyesha simulizi iliyomo katika makala hii ikiibua mambo huku ikikiri kwamba baadhi ya madai yake bado zinapingwa.

Ndani ya makala hii:
• Maisha ya awali ya Magufuli na kupanda kwake madarakani
• Mapambano yake dhidi ya ufisadi na wafanyakazi hewa
• Mageuzi makubwa ya miundombinu na kiuchumi
• Migogoro ya mikataba ya madini na sera za utawala •
Tanzania wakati wa COVID-19
• Matukio yaliyopelekea kifo chake
• Legasi ya Urithi wake na athari kwa Tanzania na Afrika pia.

Makala hii ipo wazi kwa maoni Iwe unampongeza Magufuli, unamkosoa uongozi wake, au unataka tu kumwelewa mmoja wa marais wa kisasa wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, makala hii inatoa maelezo ya kina kuhusu mtu huyo, awamu ya urais wake, na mijadala inayoendelea baada ya kifo chake
View attachment 3642765

Utangulizi maridhawa.... ngoja tusubri yaliyomo yamo?
 
Anaweza kuwa na mabaya mengi, ila sifa ya ubaya hata ufanye kwa udogo wa hali ya juu huonekana kubwa sana kiasi cha kufuta mengi sana mazuri yake.

Lakini kwa Magufuli yeye ameendelea kuwa kielelezo cha uongozi bora kiasi cha kuto onekana kuwahi kuwa na baya.

Na ukweli ulio halisi hata kama leo hii asingekuwa madarakani kama asingefariki , historia itamkumbuka kwa muda mrefu wa kutosha kwamba alikua rais bora kwa kizazi chetu.
 
Back
Top Bottom