Fabolous
JF-Expert Member
- Sep 23, 2010
- 3,689
- 5,409
Yes, vise versa is true...Na kinyesi ukikiweka kwenye dhahabu hakibadiliki thamani yake.š¤£
Yes, vise versa is true...Na kinyesi ukikiweka kwenye dhahabu hakibadiliki thamani yake.š¤£
Hii movie ni nzito,Kuna mengi sana ya kuchangia hapa.
Lakini kwanza:
Kichwa cha mada kinazungumzia "Usaliti kwa Magufuli".
Natumaini hili la usaliti litajadiliwa kwa kina kinachostahiki.
Binafsi kwenye "Documentary" hiyo ningependa kuona maoni ya kutosha kwa 'characters' muhimu wa movie hii muhimu sana.
Ukimuweka pembeni Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa kweli simpi uzito katika movie hii ya usaliti, wacheza movie hiyo wenye mchango mkubwa wa kuinogesha sidhani kuwa kutakuwepo na wengi zaidi ya akina Kabuti Kalamaganda. Character itakayochezwa kumwakilisha huyu mtu mwenye mijicho kama ya bundi ni kati ya wanogeshaji wakuu wa sinema hii.
Nitashiriki kumjadili 'stelingi' mkuu wa sinema yenyewe, ambaye ni JIWE mwenyewe; kwa mazuri yake, na mabaya maovu kabisa ya utawala wake.
Bila ya shaka yoyote.Lakini walioliingiza Taifa katika uozo tuliomo sasa ni pamoja na Magufuli mwenyewe
Hapana.Tanzania tutaendelea kuchapwa mpaka tukome,tulipewa mtu sahihi hatukumthamini.
Wacha tutembezewe bakora barabara
Kila kiongozi ana mazuri yake na mabaya yake.Hapana.
Magufuli hakuwa "mtu sahihi" hata kidogo kwa taifa hili.
Hayo mazuri aliyoyafanya yote aliyachafua kwa mabaya kabisa aliyotenda.
Utakuwa na sababu zako binafsi, pengine zisizozingatia mtangamano wa taifa.Kila kiongozi ana mazuri yake na mabaya yake.
Ila kama kichwa chako kipo hakifungamani na upuuzi wa kisiasa,
Kwangu Magufuli alikuwa sahihi zaidi ya maraisi wote Tanzania
Hivi haiwezekani tukajifurahisha hapa wenyewe kwa mahakama yetu badala ya huko nje. Mbona itakuwa ( burudani?} nzuri zaidi!Hasa pale atapokuwa amesimama kizimbani kujubu mashtaka yake pale mahakama ya kimataifa ICC The Hague
Ok, ni raisi yupi kwako unadhani alikuwa Bora zaidi ya wengineUtakuwa na sababu zako binafsi, pengine zisizozingatia mtangamano wa taifa.
Sitakuuliza hizo sababu zako za kumchukulia Magufuli kama ulivyoandika hapa; ila nina mashaka sana kama hazihusiani na hiyo unayoiita wewe siasa!
Magufuli angekuwa rais mzuri sana kwa yale aliyojaribu kufanya kuiinua Tanzania kwa miundo mbinu; lakini kumbuka maisha ya nchi na wananchi wake siyo miundombinu pekee.
Huko kulinda raslimali za taifa nako kungemwinua sana, lakini njia alizotumia zilikuwa za kishamba kiasi cha kuiingiza nchi kwenye migogoro ya mikataba, na mwisho wa siku hasara.
Labda kwako, kama ulivyobainisha, lakini kamwe Magufuli hana hiyo sifa ya kuwa rais bora kati ya wote tuliowahi kuwa nao.
Hilo ni swali 'subjective', sidhani kuwa unaelewa maana ya swali kama hilo.Ok, ni raisi yupi kwako unadhani alikuwa Bora zaidi ya wengine
kwa hapa kwetu
Kuchekacheka,uzuri wa sura,ulaghai sio vigezo vya ubora kwa raisi.Ubora upo katika usimamiaji wa katiba kwa maendeleo ya nchi.Hilo ni swali 'subjective', sidhani kuwa unaelewa maana ya swali kama hilo.
Rais bora kwa vigezo vipi, uzuri wa sura; kuchekacheka kila mara; ulaghai; kufanya mambo kwa kutafuta sifa,....
Makonda na sabaya waliishi Kishua mno kwakuwatesa watu na magufuli hakuwafanya chechote kile....inatia mashaka mno
Mtu sahihi asiyetaka Katiba mpya?Tanzania tutaendelea kuchapwa mpaka tukome,tulipewa mtu sahihi hatukumthamini.
Wacha tutembezewe bakora barabara
"...usimamiaji wa Katiba..." Magufuli alikuwa sifa hii au kuna Magufuli mwingine huko ulikokuwa wewe?Kuchekacheka,uzuri wa sura,ulaghai sio vigezo vya ubora kwa raisi.Ubora upo katika usimamiaji wa katiba kwa maendeleo ya nchi.
Hivyo swali langu lipo palepale
Kuna Magufuli mmoja TU,naye ni John Pombe."...usimamiaji wa Katiba..." Magufuli alikuwa sifa hii au kuna Magufuli mwingine huko ulikokuwa wewe?
Ukichukulia hiki kigezo pekee, ambacho ni kikuu zaidi pengine kuliko vingine vyote, Magufuli hatakuwa mbali na kundi la Samia. Hawa watakuwa wa mwisho kabisa kati ya marais wote waliowahi kushiika nafasi hiyo.
Mkuu uozo ulikuwepo muda TU kabla hata ya Magufuli,ila sema nyakati zile utandawazi haukuwepo.Hii movie ni nzito,
Ina characters wengi wa mifumo.
Mpaka Magufuli kukimbia Ikulu na kuhamishia makao Chato ujue vita ilikuwa ngumu, tega nikutege.
Lakini walioliingiza Taifa katika uozo tuliomo sasa ni pamoja na Magufuli mwenyewe na wengine wengi ambao bado wako hai.