DOKUMENTARI - Usaliti kwa MAGUFULI Hadi Saa Yake ya Mwisho

Hii movie ni nzito,
Ina characters wengi wa mifumo.
Mpaka Magufuli kukimbia Ikulu na kuhamishia makao Chato ujue vita ilikuwa ngumu, tega nikutege.
Lakini walioliingiza Taifa katika uozo tuliomo sasa ni pamoja na Magufuli mwenyewe na wengine wengi ambao bado wako hai.
 
Dokumentari ya Samia Suluhu Hassan nayo itakuwa imejaa matukio gani ya kukumbukwa ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania ?

Hasa pale Samia atapokuwa amesimama kizimbani kujibu mashtaka yake pale mahakama ya kimataifa ICC The Hague
 
Tanzania tutaendelea kuchapwa mpaka tukome,tulipewa mtu sahihi hatukumthamini.
Wacha tutembezewe bakora barabara
 
Lakini walioliingiza Taifa katika uozo tuliomo sasa ni pamoja na Magufuli mwenyewe
Bila ya shaka yoyote.
Anaomchango mkubwa sana katika hali mbovu iliyopo sasa.
Na hili ndilo linalotakiwa kujadiliwa kwa utulivu, bila kujali hayo mazuri aliyoonekana kuyafanya.
 
Hapana.
Magufuli hakuwa "mtu sahihi" hata kidogo kwa taifa hili.

Hayo mazuri aliyoyafanya yote aliyachafua kwa mabaya kabisa aliyotenda.
Kila kiongozi ana mazuri yake na mabaya yake.
Ila kama kichwa chako kipo hakifungamani na upuuzi wa kisiasa,
Kwangu Magufuli alikuwa sahihi zaidi ya maraisi wote Tanzania
 
Kila kiongozi ana mazuri yake na mabaya yake.
Ila kama kichwa chako kipo hakifungamani na upuuzi wa kisiasa,
Kwangu Magufuli alikuwa sahihi zaidi ya maraisi wote Tanzania
Utakuwa na sababu zako binafsi, pengine zisizozingatia mtangamano wa taifa.
Sitakuuliza hizo sababu zako za kumchukulia Magufuli kama ulivyoandika hapa; ila nina mashaka sana kama hazihusiani na hiyo unayoiita wewe siasa!

Magufuli angekuwa rais mzuri sana kwa yale aliyojaribu kufanya kuiinua Tanzania kwa miundo mbinu; lakini kumbuka maisha ya nchi na wananchi wake siyo miundombinu pekee.

Huko kulinda raslimali za taifa nako kungemwinua sana, lakini njia alizotumia zilikuwa za kishamba kiasi cha kuiingiza nchi kwenye migogoro ya mikataba, na mwisho wa siku hasara.

Labda kwako, kama ulivyobainisha, lakini kamwe Magufuli hana hiyo sifa ya kuwa rais bora kati ya wote tuliowahi kuwa nao.
 
Hasa pale atapokuwa amesimama kizimbani kujubu mashtaka yake pale mahakama ya kimataifa ICC The Hague
Hivi haiwezekani tukajifurahisha hapa wenyewe kwa mahakama yetu badala ya huko nje. Mbona itakuwa ( burudani?} nzuri zaidi!

Nasitak kutumia neno hilo "burudani", kwa heshima ya waTanzania wote waliouawa na kuumizwa na mtu huyu.
 
Ok, ni raisi yupi kwako unadhani alikuwa Bora zaidi ya wengine
kwa hapa kwetu
 
Ok, ni raisi yupi kwako unadhani alikuwa Bora zaidi ya wengine
kwa hapa kwetu
Hilo ni swali 'subjective', sidhani kuwa unaelewa maana ya swali kama hilo.

Rais bora kwa vigezo vipi, uzuri wa sura; kuchekacheka kila mara; ulaghai; kufanya mambo kwa kutafuta sifa,......?

Ainisha vigezo unavyotaka kuwalinganisha hao ma-rais; halafu wawekee alama kwa kila kigezo ulichoweka; na hakikisha wewe mwenyewe huathiriwi na "uchawa" wakati unawapa alama hizo.

Utaiweza wewe kazi hiyo?

Sihoji "wewe" kumwona Magufuli katika mwonekano huo uliompa kwa vigezo vyako ulivyotumia kufanya hivyo.
 
Hilo ni swali 'subjective', sidhani kuwa unaelewa maana ya swali kama hilo.

Rais bora kwa vigezo vipi, uzuri wa sura; kuchekacheka kila mara; ulaghai; kufanya mambo kwa kutafuta sifa,....
Kuchekacheka,uzuri wa sura,ulaghai sio vigezo vya ubora kwa raisi.Ubora upo katika usimamiaji wa katiba kwa maendeleo ya nchi.
Hivyo swali langu lipo palepale
 
Kuchekacheka,uzuri wa sura,ulaghai sio vigezo vya ubora kwa raisi.Ubora upo katika usimamiaji wa katiba kwa maendeleo ya nchi.
Hivyo swali langu lipo palepale
"...usimamiaji wa Katiba..." Magufuli alikuwa sifa hii au kuna Magufuli mwingine huko ulikokuwa wewe?

Ukichukulia hiki kigezo pekee, ambacho ni kikuu zaidi pengine kuliko vingine vyote, Magufuli hatakuwa mbali na kundi la Samia. Hawa watakuwa wa mwisho kabisa kati ya marais wote waliowahi kushiika nafasi hiyo.
 
Kuna Magufuli mmoja TU,naye ni John Pombe.
Elewa maana ya neno "kwangu Mimi"
Na hayo uliyoyaandika hapo ni mtazamo wako binafsi sio wa watanzania wote,
Vilevile nimesema kila raisi ana mazuri yake na mabaya yake,
Ninaposema kwangu Magufuli alikuwa Bora haimaanishi kuwa hawa wengine ni wabaya,au kwamba Mabaya ya Magufuli sikuyaona.
Nasisitiza huu ni mtazamo wangu tu
 
Mkuu uozo ulikuwepo muda TU kabla hata ya Magufuli,ila sema nyakati zile utandawazi haukuwepo.
Na hii yote hakuna mwingine anaesababisha ni kile chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…