Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?


Tukiitwa lile jina la Trump tunakuwa wakali kama pilipili.

Rafiki hao watawala wameshatuona Wadanganyika ni mazuzu,maana wa Kwanza ndiye aliyewapa madini,wa pili akapunguza mrahaba baada ya kuona wawekezaji wanapata hasara.

Watatu amekuja amesema zile vumbi zina madini 80%,leo ati wamepata hasara sasa nani amewekezwa sisi au wao?

Jamaa yetu alisema kwa njia hiyo hao jamaa hatuwawezi tupite njia hii japo ni ndefu tukasema siyo Msalendo sijui,sasa tunalalamika nini wakati aliyemtoa Mwali ni yule tuliyempa nyumba atulindie?
 
Unasahau kama Magufuli ni Raisi wa nchi hivyo kila anachokifanya ani lazima kitapata media coverage, hilo halikwepeki, sasa nashindwa kuelewa unaposema hiyo ulioiita ,,hauhitaji media power "unamaanisha nini?
Baada ya matangazo ya kutosha kuhusu makabidhiano ya Report za Makinikia na ile ya Almasi nje ya Bunge, kuna kipindi kimefanyika.
Kama sio cheap popularity kutafutwa ni nin.

Wakawatibua Acacia kwa mbwembwe, tukaambiwa kila MTU ataweza pata Noah, wakaja ni USD 300 mpaka sasa holla.
 
Kwanza nianze na masahihisho kwa Paskali:

Umetaja kuwa bei ya dhahabu ni $779. Nadhani hapo umechanganya vitu vitatu tofauti:
1. Kwanza kuna kitu wanaita AISC (all-in sustaining cost). Sina neno sahihi la Kiswahili, lakini hizi ni gharama za uzalishaji kwa ounce moja zikijumlisha na gharama nyingine za kusustain biashara ya uchimbaji kama vile exploration, nk.

2. Costs per ounce produced...imetajwa kuwa ni $581. Hizi ni gharama za kuzalisha ounce moja lakini bila kujumlisha hizo zinazoitwa sustaining costs. Na ndio maana inashuka toka $779 mpaka $581.....

3. Gold price per ounce...hii hawajataja na huwa inafluctuate kama $. Ila on average kwamuda wa miaka miwili sasa haijawahi kwenda chini ya $1,150. Ya leo nadhani iko around $1,300. Sasa hii ndiyo bei ya dhahabu kwa ounce (wakia) moja.

NB: Ounce moja ni sawa na gramu 31.1035. Tukumbuke tu kuwa ounce inayotumika kupima madini kama dhahabu ni tofauti na ounce ya uzito wa kawaida, ambayo ni gramu 28.3495. (Troy ounce for gold, and Avoirdupois ounce for normal measurements).

At least tumewekana sawa kwa hili.
 
Kwani alichaguliwa ili ajaribu?


Bila ya kujaribu huwezi kwenda mbele, Angola wamerusha Satellite ikapotea hivyo jaribio lilishindwa, lkn haimaanishi kwamba wanapaswa kuchekwa na kukejeliwa kama mlivyo ninyi, huo ni mwanzo watajifunza kujipanga na mara ya pili au ya tatu hata nne satellite itaingia orbit na kufanikiwa!
 


Ni kipi kingefanyika ambacho kwako kisingekuwa ni ,,mbwembwe"? Unajua nini inaelekea hauna cha kufanya maishani mwako na maisha yako ni boring sana ndiyo maana umekaa kusubiri fulani ashindwe uje na misemo na kucheka na kukebehi, amini usiamini mtafute mtu yoyote ambaye yuko busy na maisha yake kama hata anakumbuka hiyo wewe unayoiita mbwembwe!
 
Uhuru wa kujieleza na kuhoji ndio msingi wa maendeleo ya kweli. Nchi ikiwa na "wajuaji" wachache wanajiona wana mawazo ya "kimungu" haiwezi kwenda mbele. Acha tuwe "wananchi" tuwaachie "wenyenchi" nchi yao waiongoze watakavyo.
 
Hajajaribu!!! Aliwahi kuahidi mikataba ya madini itapelekwa bungeni ili watanzania wajue kilichomo, mikataba haijapelekwa!!!! Bila mikataba kupelekwa bungeni na kupitiwa upya unatarajia nini? Tunakataa kudanganywa mchana kweupe!!! Hivi wewe uliamini kuwa faida ya biadhara ya madini tutakuwa tunagawana nusu kwa nusu?

Hakuna ajuaye kiasi cha faida wanayopata wawekezaji wa madini! Ripoti yao inaonesha tofauti ya mapato ya 2017 na 2016!! Kupata pesa pungufu 2017 kuliko 2016 si ushahidi kuwa hukupata faida!

Mwisho wa siku sisi kama watanzania tumefaidika vipi na matokeo ya hizi kamati mbili za makinikia zaidi ya kupewa ahadi hewa za Noah na kishika uchumba $300 milioni za kuonesha nia njema na kudanganywa kugawana faida ya biashara ya dhahabu nusu kwa nusu!
 
Naona umeshindwa kwa nguvu ya hoja sasa umenigeukia personally.
Usijaribu kuwasingizia watu uhalisia wako wa maisha.
Kama maisha yako yanaboa haimaanishi na yangu yapo kama yako.

Naona huna hoja nyingine tena.
 


Kwani Sheria ya mpya ya Madini haikupelekwa Bungeni?
 
Mkuu hata wachawi manatunukiana PHd tujiulize elimu yetu chini ya CCM na phd lukuki bado tu hatujajigundua kuwa ni mambumbumbu.
 
Naona umeshindwa kwa nguvu ya hoja sasa umenigeukia personally.
Usijaribu kuwasingizia watu uhalisia wako wa maisha.
Kama maisha yako yanaboa haimaanishi na yangu yapo kama yako.

Naona huna hoja nyingine tena.


Hiyo ni dalili ya kwamba maisha yako ni boring na ndiyo maana umewekeza muda kusubiri Binadamu xyz ashindwe umecheke na kumkebehi, Binadamu ambaye yuko busy na ana Maisha yake hawezi kukumbukba vitu kama hivyo unavyokumbuka wewe, kwani hana huo muda!
 
Hiyo ni dalili ya kwamba maisha yako ni boring na ndiyo maana umewekeza muda kusubiri Binadamu xyz ashindwe umecheke na kumkebehi, Binadamu ambaye yuko busy na ana Maisha yake hawezi kukumbukba vitu kama hivyo unavyokumbuka wewe, kwani hana huo muda!
Its called long-term memory (LTM) brother.
 
aliambiwa amtafute lisu ampe ushauri akajifanya mjuaji, kwa hili watz wazalendo halisi hatuko naye
 
Paskali umekuwa mchawi.
Wachawi ndio mabingwa wa kufukua makaburi.
Unatunukisha harufu bwana!Lione!

Namfurahia Pascal anavyotukumbusha Noah zetu tulizoambiwa mchana kweupe hadharani! Kishika uchumba tulichoahidiwa baada ya majadiliano marefu dola 300 milioni, na MKUU alisema kije mapema!!!!

Vinginevyo hawa watu warudishe nishai tulizowapa maana mpaka sasa hakuna tija!!!
Tunakaribia kuhoji gharama kiasi gani ilitumika kwenye kamati mbili za makinikia na kwenye mazungumzo hayo marefu!!!! Ndiyo !!!!!
 
Kamtie moyo wewe na ukoo weee[emoji57] [emoji57]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…