Jambo ambalo sijawahi kulielewa maisha yangu yote kuhusu jamii yetu ni hili, ni kwa nini huwa mnafurahia sisi kushindwa? I mean, ukiangalia jamii yetu ni kama watu wamekaa wanasubiri ushindwe wakucheke na kukukebehi, kwangu mimi sisi Watanzania ni watu childish sana, so immature, maisha hayako hivyo, watu wengi waliofanikiwa Duniani ni kwa kujaribu, kuchukuwa risks ndiyo unaweza kwenda mbele!
Bill Gates aliacha Chuo Harvard na kuanzisha Microsoft kama Wazungu wangekuwa childish na immature kama sisi kukaa kusubiri ushindwe ili wakucheke asingepata support, lkn wazazi wake na nchi nzima iko nyuma yake na kama microsoft ingeshindwa angerudi Chuoni na hakuna ambaye angemcheka au kumkebehi!
Sasa Raisi Magufuli amejaribu kama ameshindwa hatupaswi kumcheka wala kumkebehi bali tunapaswa kujipanga na kuanza upya, bila kubadilisha hii tabia hakuna tutakapoenda, kwa kifupi mnawarithisha hata Watoto wenu negativity na watashindwa pia maishani na ku-compete na Dunia kwani mnawajaza woga na misemo kama sijui tulikwambia acheni huo ujinga vinginevyo tutaendelea kubakia masikini maisha yote !
Ukitaja pangaboi utaliza watu!Kwako Pascal Mayalla hivi kuna riba wanayochajiwa hawa wazungu kwa kuchelewa kulipa ile pesa? Maana ile pangaboi riba ina accumulate kila siku.
Nakumbuka siku moja tukiwa ziarani na mkwere nchi fulani bwana mmoja aliuliza "hivi tukiamua kuachana na ununuzi wa madini ya Afrika mtayatumia kufanya nini?"
Swali hili linaungana na kauli yako kuhusu umuhimu wa elimu kwa watu wetu nchi hii inahitaji sana elimu.
Si madini tuuu tuna resources nyingi bado hazijatusaidia.
Pole zake bwana Ngosha anatakiwa apewe elimu shibishi ya the " corporate world"
Zile zilikuwa nishani za utiifu. Yaani kukubali kuweka weledi pembeni, kukubali kujidhalilisha na kuwa tayari kuimba wimbo uliokaririshwa na mtu ambaye hana uelewa wowote wa fani uliyoisomea.Watu walipewa mpaka nishani/tuzo za heshima kwa kazi iliyotukuka na mkuu wa nchi... Ndio aina na uongozi tuliochagua, mambo ya "font ferd" kwenye kila kitu..
Hakuna malipo nje ya mkataba,
Cha muhimu ni srikali kuweka wazi nikataba ijadiliwe kwa uwazi ili kuondoa au kupunguza mambo ya asilimia kumi. Botswana na Ghana waliweza kutikana na uwazi na uzakendo was mamlaka husika (parliament na rais)
Pia ni lazima wabunge na watz wore tuacge siasa za kubaguana kwa vyama Bali tufanye siasa za hoja kuhusu rasilimali zetu. I
Haiwezekani wabunge wanazomeana kisa tu mcgango umetolewa na mpinzani
Hatustahili/tunastahili kulipwa kutokana na mikataba na si mazungumzo ya kupata public support
Hapa porojo tupu Na hasira za mkizi zilizokuwa zinamwongoza MKULU, mm nilikuwa moja ya migodi hiyo, kila mwezi wanazalisha ziada, Na wanaongeza target, alikuwa anatoa bonus lkn sasa hatoi! Huyu jamaa ni mshenzi Na alipaswa kufukuzwa km mbwa koko ili ajifunze! Saivi kashabinafsisha kitengo cha ulinzi kwa migodi Yake kwa kupewa ushindi Na CMA Kanda ya Shinyanga! Alafu unasema utaweza kupambana nae? Its naked zero (negative)
Kwa sasa tunaacha muda uongee.Ngoja aje Salary slip!
Mimi si miongoni mwa wajinga. Nina uelewa usio na mashaka na unaokubalika mahali popote Duniani. Na toka mwanzo tulisema ripoti ya Mruma ilikuwa ni upuuzi mtupu.Paskali, hayo makorokocho yoote uliyoandika sijayaelewa/sitaki kuyaelewa.
Haimaanishi na yale tuliyoelezwa na kamati niliyaelewa, hasha!
Mlituambia kuwa yale Makinikia si kitu, ni vivumbi tu vya dhahabu...kamati ikasema TUNAPIGWA, mmapinga.....mkatoa makorokocho meeengi ya kupinga.
Leo, hao hao wanakuaminisha kuwa wanapata hasara kwakuwa VIVUMBI vimezuiwa, wewe unajitoa ufahamu kuwa unawaelewa sana?
SIEIJII alisema hao jamaa walikuwa wanajiendesha kwa hasara, sasa kama watu wanakaa miaka ishirini sehemu na kusema wanapata hasara tuuu na hawaondoki, leo wanakwambia ABC...unakuja hapa na kujiona wewe ndo ulioumba maandishi jinsi unavyoyaelewa.....
Mi sielewi chochote yani, FUKUZA tu....si wanapata hasara, waondoke......wasomi wetu hawa wanaochanganya maneno, wanachoweza ni kutuchanganyia lugha tu wakidhani ndio uerevu au kuendelea.....
Sheria ya madini ni kitu kimoja na mikstsba ya madini ni kitu kingine kabisa! Mikataba ya madini huingiwa kwa kuzingatia sheria iliyopo ya madini! Mikataba iliyopo iliingiwa chini ya sheria ya madini iliyopitishwa kwa hati ya dharula na INA mianya mingi ya ufisadi! Hiyo mikataba iliyoingiwa kipindi hicho ndiyo imebaki siri na ni ya kifisadi kwelikweli! Hiyo mikataba ndo tunataka iwekwe wazi bungeni tuone tulivyopigwa na tuamue kusuka au Kunyoa!Kwani Sheria ya mpya ya Madini haikupelekwa Bungeni?
Ukitumia gold mining data, za Acacia na duniani kwa ujumla, utapata conclusion kwamba, sio tu Acacia bali hata hao Barrick Gold Mine hawana uwezo wa kulipa zile pesa... I repeat, HAWANA UBAVU. Data zetu zipo so irrelevant!
Look, according to USA Gold, total gold produced duniani in 2016 ni tani 3100.
Tani 3100 ni sawa na 3,100,000 kg
Kwa mujibu wa mtandao wa GoldPrice, bei ya dhahabu at 14:15 EAT ilikuwa 1,333.01 per ounce. Anyway, sijui pametokea nini manake pamekuwa na sharp decline in price from around US$ 1342 to 1,333.01 lakini wametoa best price as $1356 per ounce (for gold bar).
1 oz ni takribani 28.5 grams.
3,100,000 kg = 3,100,000,000 grams = 109 M ounce (maximum)
Thamani yake ni 109,000,000 x $1356 = $ 148 Billion (maximum)
Hii maana yake ni kwamba, dhahabu iliyozalishwa duniani kote mwaka 2016 ina thamani ya takribani $150 Billion wakati pesa tunayodai sisi ni $190 Billion!
Yaani, Acacia/Barrick kulipa ile pesa ina maana waachiwe dhahabu YOOOOOOTE duniani kwa mwaka mzima. Aidha, wazalishe dhahabu hiyo at ZERO cost ndipo wanaweza kulipa deni (assuming uzalishaji na bei vinabaki constant)!!!
Look again, hoja ni kwamba ni tunaabiwa kupita kiasi.
Ina maana na Australia wanaibiwa kupita kiasi?
Mwaka 2016 Australia walizalisha 270 tani za dhahabu! Remember, Australia ni among top gold producers duniani!!!!
Tani 270 = 270,000 kg = 270,000,000 grams = 9.5M ounce (Maximum)
Thamani yake kama ingeuzwa leo, ingekuwa 9,500,000 x $1356 = $13 Billion (maximum).
Hii maana yake ni kwamba, endapo Australia wataamua kuwalipia deni Acacia, basi watalazimika kutumia dhahabu yao yooooooooote kwa takribani miaka 15 (190 billion/13 Billion) ndipo wanaweza kumaliza deni lote la Acacia na hapo tuki-assume, Australia wanazalisha dhahabu hiyo at ZERO cost na kila mwaka wanazalisha tani 270.
Kwahiyo kwa data zisizo-make sense kama hizo TUSAHAU eti kwamba Acacia au hata Barrick watakuja kulipa hata 25% ya kile wanachodaiwa! Na hili nilisema tangu awali.
Na ukweli ni kwamba, sioni uwezekano wa kulipa hata 10% ya kile wanachodaiwa!
BONUS: According to Bloomberg, New York Stock Exchange walifunga soko tarehe 12.01.2018 wakati Barrick Gold wakiwa kwenye position ifuatayo:
View attachment 677012
Unaona hapo chini, Market Cap ni 17.64 Billion. Na tunaposema Barrick ina maana na hesabu za Acacia zipo ndani yake bila kusahau hesabu za kampuni zao zingine zote.
So, with Market Cap ya 17.64, ina maana endapo shareholders WOOOOOOOTE wa Barrick Gold wangeamua kutoa shares zao zoooooooooote free of charge kwa Barrick kisha Barrick wakauza shares zooooooote na kuamua kutumia mapato ya uuzaji wa hizo share, bado wangeweza kulipa ONLY $17.64 Billion wakati tunawadai $190 Billion na huku pia tunaiacha Barrick Gold mikono mitupu!!!
Hii maana yake ni kwamba, deni husika HALILIPIKI kwa sababu takwimu zilizotolewa ni za UONGO... simple and clear!!
Hivi hata kwa kutumia akili ya kawaida, miaka miwili imeisha hata kijiji kimoja hakijapata hata nusu ya ahadi hiyo, kuendelea kusubiri kuzipata kwa siku isiyojulikana! Vinginevyo watuambie ratiba ya utekelezaji wake! Mbona hiyo ahadi haiongelewi kabisa na wanaoiongelea wanaonekana kama wachochezi fulani hivi!!!!Hilo la Mikataba siwezi kuliongelea kwa maana sina uelewa, lkn la ahadi za kwenye kampeni njuavyo waliahidi kutimiza 2015-20 na leo hii ni 2018 hivyo muda wa kuhukumu kwa hilo bado, subiri ikfika 2020 na hawajatimiza hapo ni sawa kuhukumu!
Hivi hata kwa kutumia akili ya kawaida, miaka miwili imeisha hata kijiji kimoja hakijapata hata nusu ya ahadi hiyo, kuendelea kusubiri kuzipata kwa siku isiyojulikana! Vinginevyo watuambie ratiba ya utekelezaji wake! Mbona hiyo ahadi haiongelewi kabisa na wanaoiongelea wanaonekana kama wachochezi fulani hivi!!!!