Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia inakula hasara, has no capacity to pay! Tumedanganywa?

Flash Huna? Nikuazime ya Kwangu ''Do you remember the drama used with the so called Flash ''
 
Una access na account ya serikali na kujua kilichoingia na kutoka?! Instead of being conclusive why dont you ask? ‍♂️! Watanzania bana
 
Ni mikataba ya kipindi kipi ambacho haijawa ya siri?!
 
Una access na account ya serikali na kujua kilichoingia na kutoka?! Instead of being conclusive why dont you ask? ‍♂️! Watanzania bana
Ina maana zile USD 300 Million tulizoahidiwa watu walienda kuangalia kwenye akaunti ya serikali?!
 
Hahaha Paskali bana, wasomi gani wa madini zaidi ya Prof.Mruma na prof.Mrosso ma undercover waliosimamia tume mbili za kukamata wezi?!Bila, kumsahau beki tano prof.kaduri mzee wa makanuni?!

Why do you care about 300mil, walituambia Tanzania inavuta 70% regardless, hatuna hata koleo letu mgodini, wazee wa kazi tu lakini hatufanyi kazi yoyote mgodini tunalipwa 70% halafu unaulizia 300mil?! Nchi hii ilikuwa inaibiwa na kuchezewa sanaa tumepata super watchman kakaba kona zote hatuibiwi tena hahaha don't worry about 300mil.

Mkalimani wa Thompson alituambia wamekubali kulipa 300mil na kukubali kulipa 70% ya mapato halafu wewe unauliza nini eti kishika uchumba?! Nani anaolewa?! Tanzania ni changudoa haolewi tena labda mtoto wake hahaha.

Hivi uliisha shuhudia mtu kafumaniwa huku uswahilini kwetu?! Ngoja ni kwambie, anaitwa sheikh, ubani na mkeka. Inapigwa ndoa ya mkeka,hapo mwanaume unakubali kila kitu. Hahaha jiulize ukiachiwa hapo jasho unaenda kulifutia mbalii, shati utalivalia mbali sana, kandambili hizo utazisahau hahaha.

Duh paskali uneniua mbavu na kishika uchumba chako. Hahaha mchumba aliisha isha thamani labda m renegotiate mkuu. Tuendelee kusubiria ndege ya Thompson muoaji wetu pale bandarini na kitita cha 300mil hahaha.
 
Umenena vyema umesema mmenunua ndege vp kuhusu ndege yetu iliyo kamatwa canada au mlidhan tumesahau mnaingia mwaka wa tatu sasa kila kitu mnafanya nusunusu tu bora hata kikwete alijitahidi sana kwenye kilimo na kauli mbiu yake ya kilimo kwanza
 
Hiyo 300bn alisema sizonje ila tra wao walisema wanadai kodi ya makinikia 400bn yani baba anaongea yke watoto nao wanaongea yao..hii familia ya awamu hii kila mtu msemaji anasema yke..ila mwisho wa siku wataumbuka kwa uwongo wao yani wamekua watu wa fiksifiksi tu badala ya kufanya kazi tuone maendeleo
 
MKishindwa lazima tushangilie kwa maana tunapokuwa tunawashauri mnakuwa viburi nakutuzomea huku mkitanguliza u sisiem wenu
 
Umenena vyema umesema mmenunua ndege vp kuhusu ndege yetu iliyo kamatwa canada au mlidhan tumesahau mnaingia mwaka wa tatu sasa kila kitu mnafanya nusunusu tu bora hata kikwete alijitahidi sana kwenye kilimo na kauli mbiu yake ya kilimo kwanza


Bado uko kama wenzako, mnakebehi na dharau!
 
Kwani Sheria ya mpya ya Madini haikupelekwa Bungeni?

Wewe hii mada kwako ni nzito, na tatizo unalokumbana nalo umejiingiza kwenye kusifia sana serekali hii kiasi kwamba hata kwenye makosa ya wazi unajifanya kutetea. Halafu kibaya zaidi huwa unajiingiza kwenye ushabiki wa kejeli bila kujua huko unakotetea kuna makosa mengi ya wazi. Huyo jamaa kukuambia mikataba kupelekwa bungeni, wewe unasema sheria haikupelekwa bungeni. Fahamu chenye tatizo ni mikataba ya madini na sio hizi sheria mpya zilizopelekwa. Sasa kama rais ana nia nje ni kipi kinamfanya agome kupeleka hiyo mikataba ya madini bungeni ifahamike inasema nini?

Hili suala alitaka kupatia mtaji wa kisiasa, na nyie ndio mkaingia kichwakichwa kwamba jamaa ni mzalendo mpaka mkawa mnahalalisha wengine kufanyiwa ukatili eti kisa anamkosoa mmnayeamini ni mzalendo. Sawa tuseme ni mzalendo, akina Chenge, Karamagi na Yona wote wametajwa kwenye hiyo mikataba michafu na rais kaagizwa wakamatwe na kuhojiwa. Je umeona wakikamatwa na kuhojiwa? Tatizo la kutokukamatwa kwao ni hiyo mikataba ambayo Lissu alisema shida imo kwenye mikataba. Leo yale yalikuwa yanafanywa live ili kujipatia mtaji wa kisiasa mbona hatuoni mrejesho wake kama sio siasa nyepesi tu?
 
Usichokielewa au unachokifumbia macho ni kuwa hizo data ulizotumia ni sehemu ya udanganyifu wa makampuni ya madini duniani! Hawajawahi kuweka wazi data halisi za uvunaji na faida ya dhahabu!!! Nikuulize kitu! Mtendaji wa barick alikuja DSM na ndege binafsi lakini miaka yote hapa nchini hawajawahi kulipa kodi itokanayo na faida zaidi ya tozo ndogo ndogo kama mirahaba! Miaka yote wanadai wanapata hasara, kwa nini hawafungashi virago? Mbona wanahisa wanapeana gawio kila mwaka? Mbona wanatembelea ndege binafsi ili kutetea mgodi unaozalisha hasara? Ukweli ni kwamba tunapigwa sana!!!
 

Huna facts kabisa ndugu, unatumia hisia tu! Unahisi makampuni ya madini yanajifanyia mambo kadri yanavyopenda yenyewe sio??? Makampuni haya yanabanwa na sheria na kanuni ngumu sana katika masoko ya hisa yalikojisajili, lengo kuu likiwa ni kuwalinda wanahisa ambao wanaweza kuwa mimi na wewe, financial reports za makampuni haya sio taarifa za siri, ni taarifa za wazi kwa umma na zinafanyiwa auditing na third parties. Kama unahisi kudanganya ni rahisi kiasi hicho basi fungua kampuni ya madini usajili kwenye soko la hisa halafu urudi hapa kutuambia unavyoiba!
 
Ngoja aje Salary slip!

Jana ule upuuzi aliokuwa anaongea Polepole pale Channel 10 badala yake alipaswa aongelee mambo mazito kama haya. Nchi iko kwenye sintofahamu, muenezi anaongelea upuuzi wa kuhama wanachama toka chama cha upinzani kwa rushwa. Siku za nyuma wakati zile ripoti zimeteka anga Polepole alikuwa kwenye kila kipindi kutaka kuaminisha sasa tumepata muarobaini wa matatizo yetu. Lakini sasa hivi unaona anaongepea mambo mepesi, sijui mambo ya rais kukaa miaka 7. Sikufichi ule mrahaba wa madini aliokuwa anaongelea Kabudi wengi hatujaelewa ni nini alikuwa anasema. Mara anasema tutapata 50/50. Mara sijui 16% kama mrabaha.

Nimejaribu kuangalia wala sielewi nini ni nini. Mimi nimejumlisha hiyo 50 na 16 nikapata kwenye madini tutapata 66% na wawekezaji iliyobaki. Sasa kama sasa hivi tunapata hiyo sijui 50% na mchangano mwingine ndani yake mbona wafanyakazi wanapunguzwa kwenye hiyo migodi? Nilitarajia Polepole jana azungumie inakuwaje serekali iliongea tena kwa mbwembwe kwamba Acacia haijasajiliwa hapa nchini na wala hawaitambui lakini mpaka leo ipo na inachimba madini? Yeye anadhania sisi ni wajinga wa kuogopa kusikia eti wapinzani wengine anawapokea tarehe 18 wakati kuna mambo ya msingi hadhubutu kuyaongelea. Mwambie hakuna wajinga bali watu wanawasoma tu na lazima mtaingia patamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…